Wajua sababu ya Japan kuingia WW-I na WW-II?.

Wick

JF-Expert Member
Dec 19, 2012
8,313
12,123
Kuamka kwa Japan na matendo yao yote toka mwaka 1852 kuelekea mwaka 1945 yalikuwa ni matamanio yao ya kutopitia hali aliyokuwa ameipitia China karne ya 19 na pia kuhakikisha na wao wanatambulika kama nchi yenye nguvu duniani (Super Power country).
*************************************************************************************************
Kuingia rasmi kwa Japan [Nihon/Nippon] au "The Origin of the Sun" kwenye Vita ya Pili ya Dunia (WW II) kulisababishwa na moja ya matatizo yaliyopelekewa kwa vita iliyotambulika kama The Second Sino-Japanese War. Kabla ya Second Sino-Japanese War kuanza kulikuwa na migogoro wa mipaka kati ya Japan na China iliyokuwa imeanza toka mwaka 1931 baada ya Japan kuvamia eneo la uchina liitwalo Manchuria. Sasa basi ili kuweza kuielewa nia, sababu na tabia za Japan kwenye vita ya 1941-1945, inabidi tuelewe kwanini Japan aliivamia Manchuria mwaka 1931 ambapo sababu nzima tunaiona inaanza mwaka 1853.
Kabla ya mwaka 1852, Japan ilikuwa ni nchi iliyojitenga na mataifa ya magharibi (isolationist country). Hii ilitokana na mapinduzi yaliyojulikana kama The Shimabara Rebellion ya mwaka 1863 yalokuwa yamefanywa na wakulima wa mji wa Minamishibara, Nagasaki ambao wengi walikuwa wakatoliki (dini mpya Japan). Toka hapo muingiliano wa wajapan na nchi za magharibi (wazungu) ulikuwa ni mdogo sana ambapo zaidi ulikuwa ni kwenye biashara na waDutch kwenye visiwa vya Dejima, Nagasaki pekee. Wazungu hawakuruhusiwa kuingia eneo jingine lolote la Japan kufanya biashara zaidi ya Mji wa Nagasaki, hii ilifanya kusiwe na uhusiano mkubwa kati ya watu wa Japan na Mataifa ya Magharibi.
Mwaka 1853 Jemedari Matthew C. Perry wa jeshi la Maji la Marekani alitia nanga kwenye bandari ya Tokyo, ambapo baada ya kufika wajapan walimfukuza wakamwambia aende mji wa Nagasaki. Kwa kiburi yeye hakutaka kuwasikiliza na matokeo yake akawa amezungukwa na majeshi ya wajapan. Akawaambia ana barua toka kwa Rais wa Marekani wa wakati huo, Rais Millard Fillmore kwenda kwa mtawala wa wakati huo wa Japan The shogun (kiongozi wa kijeshi). Baada ya wajapan kumuwekea ngumu wakimlazimisha aende akaipitishie mji wa Nagasaki kama walivyomuelekeza, jamaa kuwaonyesha nguvu ya Marekani akalipua baadhi ya majengo yaliyokuwa pale bandari ya Tokyo kisha akawaachia barua akaondoka zake, ikabidi wajapan wawe wapole wachukue barua waipeleke kwa mtawala wao.
Baada ya Mwaka Jemedari Perry akarejea tena Japan kufuatilia wamefikia wapi maelekezo ya barua aliyowaachia (kumbuka kipindi hicho hakuna simu so unaweza peleka barua china halafu unajiwekea muda kwenda fatilia majibu yako). Jamaa baada ya kurudi wakasaini mkataba uliojulikana kama The Convention of Kanagawa, mkataba uliokuwa unataka wajapan wafungue bandari ya Shimoda (mji kati ya Kyoto na Tokyo ya sasa iliyokuwa inajulikana zamani kama Edo), pia bandari nyingine ikafunguliwa mji wa Hakodate (kaskazini mwa visiwa vya Hokkaido) ambapo bandari zote hizi zilifunguliwa ili Japan ifanye biashara na Marekani. kumbuka Japan alikuwa amefanya mji wa Nagasaki pekee ndio mji wa biashara na mataifa mengine kuzuia muingiliano nao lakini akatokea mbabe kumforce afungue na miji yake mingine ifanye biashara. Masharti ya biashara sio kwamba Japan na Marekani walikaa kuyajadiri ni kwamba Marekani alikuwa ameyaweka kabisa kwenye mkataba na wajapan wakawa hawana jinsi wakiangalia wamezidiwa kiteknolojia, kijeshi na mwenzao, so kila kitu ikawa ni ndiyo tu.
Kutokana na ubabe Japan aliokuwa ameletewa na Marekani ndipo pakapelekea historia kuandikwa upya. Kabla ya hapo Japan ilikuwa inajiona ni taifa lenye nguvu kulingana na mataifa yaliyokuwa yameizunguka lakini baada ya kukutana na mbabe wao ikabidi warudi mezani kuangalia wanafanyaje kuhakikisha hawafanywi wanyonge tena kwenye nchi yao wenyewe. Ukiangalia walizuia kuingiliana na mataifa mengine wakizani itasababisha waogopwe chokozwa na kufanyiwa alichokuwa amefanyiwa China wakati huo.
Kuogopa fanyiwa kama mwenzao China alichokuwa amefanyiwa na mataifa ya magharibi, ikabidi mfumo wa mambo Japan ubadilishwe. Mwaka 1868 wakaleta mfumo ulioitwa The Meiji Restoration, pia Shogun alivuliwa nguvu zake zikawekwa chini ya Mfalme ambapo kiuhalisia nguvu ilikuwa chini ya washauri wa mfalme. Ndani ya muda mfupi sana Japan ikabadilika ikaanza fata njia kuelekea nchi ya Viwanda. Wajapan walijua njia pekee ya kufikia nguvu za mataifa ya magharibi ni kuhakikisha wanakuwa kama mataifa ya magharibi, so wakajiweka kama wazungu na wao. Uvaaji ukawa kama wa wazungu, Jeshi likawekwa kwenye mfumo wa kizungu hadi Bunge la Japan likawa kama la wazungu pia.
Katika karne ya 19 ili uweze tambulika na wazungu kama mmoja wao ilibidi na wewe uweze kuwa na makoloni yako sehemu fulani duniani. Lakini kutokana na udogo wa Japan yenyewe isingeweza kusafiri kuja Aafrica so walichofanya wakaanza yaangalia mataifa madogo katika bahari ya Japan mojawapo ikawa Korea. Mpaka miaka ya 1890 Korea haikuwa nchi ya kumtisha mtu na pia haikuwa imeendelea kama Japan, so Japan akaamua ataanza nayo kuimiliki. Kwanza kwa kuitawala Korea, japan anajihakikishia kutoweza vamiwa na mataifa mengine kupitia upande wa korea ambao ni rahisi zaidi kuingia Japan zaidi ya pande zingine, pia Korea ilikua ina madini kibao kama Chuma na Makaa ya Mawe ambayo yalikuwa ni muhimu kwa wakati huo ukitaka kuendelea kiviwanda.
Tatizo pekee likabaki kwa wakati huo Korea ilikuwa chini ya uangalizi wa China, Mfalme wa Korea alikuwa anailipa China kumlinda. Ingawa wakati huo huo pia kuna mkataba mwingine wa Japan na Korea uliokuwa umeingiwa ina maana upande mmoja Korea inalindwa na Japan upande mwingine na China. Mwaka 1894 kulitokea machafuko Korea ambapo China akatuma vikosi kwenda yatuliza bila kumwambia Japan kwamba ametuma vikosi Korea, hii ilipelekea Japan na wenyewe watume vikosi Korea. Matokeo yake kukatoa vurugu zilizopelekea vita kuzuka ikajulikana kama The First Sino-Japanese War iliyokuwa mwaka 1894-1895.
Wachina wakapigwa kwenye ile vita na matokeo yake ukasainiwa mkataba ulioitwa The Treaty of Shimonoseki, ambapo Korea akaacha kumlipa China na matokeo yake akawa koloni la Japan. Japan ikaenda mbali zaidi ikavibeba na visiwa vya Taiwan kama koloni lao pamoja na kuingia makubaliano na China kulipwa na kufanya nao mikataba ambayo ilikuwa ni mibaya kama ile ya wazungu. Pia jamaa wakaichukua na ghuba ya Liaodong ambayo wazungu walikuwa wanaikalia na kuwaamuruu waondoke; waRussi wakati huo ndio walikuwa wameikodi ghuba hiyo. Hapo sasa Japan akawa katengeneza maadui watatu kwa wakati mmoja (Korea, China na Russia) huku wazungu wakianza muangalia kama nchi hatari (Rogue nation). Russia wakati huo ndio alikuwa na nguvu ya usemi Korea na Manchuria sasa kunyanganywa ikawa ugomvi mwingine umeamka.
Ugomvi huu ukapelekea vita kati ya Russia na Japan iliyoitwa The Russo-Japanese War ya mwaka 1904-1905. Wajapan wakashinda kwenye ile vita!, wazungu vichwa moto kuona kuna kanchi kameamka kanatangaza ushindi kila sehemu!. Ushindi huo ina maana China iliyokuwa imeikodisha ghuba ya Liaodong kwa warussi, ikabidi wawaachie wajapan bure, ina maana mkataba uliojulikana kama The Kwantung Leased Territory ukawa umekufa. Pia mkataba wa kutumia mali za Manchuria ukawa chini ya Japan na mwaka 1910 Korea ikatangazwa rasmi eneo la Japan.
Kwenye vita ya kwanza ya dunia (WWI) Japan akaingia upande wa wazungu (Allied Powers) akichagua kuipiga Ujerumani ili ayapate makoloni yake Bahari ya Pacific. Hadi hapo Japan kashakuwa kama wazungu kwenye njia zote na haogopi nchi yeyote, akiwa na nguvu na ujuzi kama wao!. Kutokana na vita hivi na vingine Japan alivyokuwa anaanzisha kupata maeneo mataifa mengine Ulaya ambayo kwa muda mrefu yamekuwa kwenye vita hadi yanajua madhara ya kupigana vita wakaanza ichukia Japan ambayo yenyewe ndio kwanza imeanza kupigana. Mfano Ufaransa na Ubelgiji badala ya kupigana na Japan wakawa wanamtekelezea anachohitaji maana wao wamepigana sana vita vikawa vimewachosha.
Wakati huo huku nyumbani China nae kaanza jipanga upya, Uongozi wa Kuomintang ukijaribu iunganisha China upande wa kusini huku upande wa kaskazini napo kwenye mji wa Nanjing napo kundi la Nationalist wakijipanga nao. Hapo Japan machare yakamcheza kuwa iwapo China ikijipanga inaweza rudi kuidai Manchuria na na Kwantung iliyokuwa imezichukua. Japan hawakuwa tayari kupoteza maeneo haya kwa China ukiangalia tena wametumia zaidi ya miaka 50 kuhakikisha hawakuwi wanyonge kama China. Kufikia lengo lao, mwaka 1931 wakapeleka jeshi kukaa rasmi Manchuria ili kulinda mali walizokuwa wamezipata pia wakajenga mpakani mwa china mji wa kulinda makazi yao ulioitwa Manchukuo mji ambao haukuwa unatambulika kiserikali popote pale, ina maana hakuna taifa ambalo lilikuwa tayari kuisaidia kutuliza ugomvi wao wa mipaka na China.
Mwaka 1937 wachina wakarudi kilingeni kupigana vita na Japan wakitaka mali yao. Hii vita iwapo igekuwa fupi yawezekana Japan angeweza shinda lakini kutokana na kuchukua muda huku China ikikataa mkataba wowote zaidi ya kupewa eneo lao basi ikawa vita ya muda mrefu zaidi ya ile ya kwanza.
Urefu wa vita ukapelekea Japan ambayo ni kanchi kadogo kaanze pungukiwa maliasili za kuendelea pigana vita na uchumi wao ukayumba ukichangia haikuwa na rafiki yeyote ndani ya eneo la Asia kutokana na tabia iliyokuwa imezifanyia nchi jirani. Pia kimataifa ilikuwa inachukiwa wakiiona ni nchi hatari na ikapelekea hata kuzuiwa kununua vifaa vya kuisaidia kupigana vita na China. Hata Marekani akainyima Japan manunuzi ya vifaa vyake kupigana vita. Ikapelekea Japan kushindwa vita ile na kurudisha kwa China maeneo yao.
Ukiangalia japan imefika hapo ikitaka kuwa kama wazungu lakini imefanikiwa kufika na bado wazungu wamegoma kuipa ushirikiano, hii ikawapa chuki na kisasi wajapan kwa wazungu, kama mmoja ya mwanadiplomasia wa Japan aliposema;
"The West taught Japan poker, but after winning all the chips, declared the game immoral.".​

Kurudisha maeneo kwa china kukaifanya Japan irudi kutafuta maeneo ya kuweza pata mahitaji yao kuendelea kuwa na nguvu na hapo maeneo pekee yakawa yamebaki Siberia na South Pacific. Jeshi la Mfalme wa Japan wakaona bora wakachukue malighafi kwa kuipiga Siberia lakini kufika kure wakapigwa kwenye vita iliyoitwa Battle of Khalkhin Gol ya mwaka 1939. Jamaa wakawa wamepewa somo hakuna kitu rahisi tena.
Ukiangalia maeneo ya South Pacific nayo yameshashikiriwa, ikabidi Japan wawe wapole kuangalia upepo. Chuki yao kwa wamarekani, na wazungu kwa kuwanyima msaada wa vifaa na mali ilipohitaji kupigana na China ikapelekea Japan iingie upande wa Ujerumani na Italy kwenye vita ya pili ya dunia (WW2) ambazo nazo zilikuwa na chuki sawa. Jamaa wakaona sasa ndio muda rasmi wa kumpiga mtu pekee aliyekuwa amewapiga na kuwaamsha-Marekani ambapo wakaitarget Bandari yake ya Pearl Harbor kama kianzio, huku pia wakizipiga Singapore, Hong Kong, Philipino na Malaysia kwa upande wa nyumbani Asia.
Ingawa Japan wenyewe walipigana kwenye WW2 na wamarekani na waingereza ili waweze tambulika kama nchi yenye nguvu na wakitaka pia kutafuta pa kupata Mafuta na Plastiki ambavyo kwa wakati huo vilikuwa malighafi ya muhimu zaidi lakini kuingia Marekani kuipiga Bandari ya Pearl Harbor ikawa ni kosa lililowagharimu na kuleta/kuandika/kuacha historia mpya dunia!.


Hiyo ndio Japan nchi iliyo apa kutokuja tengeneza Bomu la nyuklia wala kushabikia vita tena duniani kupitia mkataba uliojulikana kama The Treaty of San Francisco-1951
 
Historia mujarabu kabisa ,hiyo vita ingekuwaje ya ngumi tu(mabomu ya kawaida) bila kutumia mawe (nyuklia) US alikuwa amepoteza tayari, Japan alimshika pabaya US
kosa jingine la wajapan hawakuwa vizuri katika kutunza njia za mawasiliano ikapelekea wazungu waweze wasikiliza kila wanachowasiliana kama pale Marekani walipojua route ya Admiral Isoroku Yamamoto wakaja na Operation Vengeance kumuua ikawashusha morale wanajeshi wajapan. Lasivyo USA bigtime angepigwa
 
B 29 (Enola gay) iliandika historia ambayo mpaka leo inakumbukwa kwa kubeba Phat man na kulipeleka Hiroshima
 
Lakini kwa chokochoko za NK naona Japan atarudi kutengeneza madude..... maana NK madude yake yote anayaelekeza kwenye ardhi ya Japan kwa majaribio.
 
Lakini kwa chokochoko za NK naona Japan atarudi kutengeneza madude..... maana NK madude yake yote anayaelekeza kwenye ardhi ya Japan kwa majaribio.
mkuu shinzo abe amesema hataruhusu chini ya uomgozi wake na hadi katiba yao imekataza , sijui wanayaogopea nini?... Lakini in the other side viwanda vyao vimeka kiutayari yan nuclear reactors na viwanda vyote muda wowote wakisema waanze watakuwa nayo maana hadi rocket wanazo zile wanazotumia fika nje ya dunia!.
 
Bila Nyuklia Usa Alikuwa Mwepesi Sana Kwa Mjapan Pigwa KAMIKAZE STYLE Jamaa Wakaona Hee! Kenonkeee? Nini Hiki
lazima wamkumbuke mjapan ujanja wao wote wakaona wasipompiga bomu atawafikia pentagon!!
 
Back
Top Bottom