PreGE2025 Waitara: Yule bwana mdogo ni mbinafsi. Amshutumu Fatma Karume kwa "Utapeli wa Kisiasa" Kesi ya Nyamongo

PreGE2025 Waitara: Yule bwana mdogo ni mbinafsi. Amshutumu Fatma Karume kwa "Utapeli wa Kisiasa" Kesi ya Nyamongo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara, ambaye aliwahi kuwa mwanachama wa Chadema kabla ya kujiunga na CCM, ameibua tuhuma nzito dhidi ya wakili maarufu Fatma Karume, akimtuhumu kwa kushiriki kile alichokiita "utapeli wa kisiasa" unaohusiana na mzozo wa wachimbaji wa Nyamongo.

Akizungumza bungeni leo, Aprili 11, Waitara amedai kuwa Fatma Karume ameingia ubia na baadhi ya watu wa Nyamongo kufungua kesi nchini Canada kwa madai ya kutetea haki za wakazi wa eneo hilo.

"Wale watu ambao wamefanya ziara kule kusini, Makamu Mwenyekiti yule kijana bwana mdogo ni muongo na mbinafsi. Na kama akija kwenye jimbo lako, kiboko yake nipo. Yule nimemgonga 2008, nimemgonga 2015, nimemgonga 2020 na mwaka huu kichapo kipo pale pale,"

"Huyu ameenda kwenye hifadhi ya Serengeti, anajua kuna sheria anawaambia chukueni ng'ombe mkachunge hifadhini, zilikamatwa ng'ombe na watu waliumia yeye akala kona hakuwasaidia... Huyu ni mbinafsi".

Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita waitara amemtuhumu Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Heche kuwa ni muongo na mbinafsi na kwamba anashirikiana na mwanaharakati Fatma Karume kujipatia pesa kwa njia zisizo halali

Huyo waitara ni aina ya wabunge wa hovyo kupata kutokea Tanzania hii ni mtu mjinga mjinga sana huko ccm kwenyewe hawamtaki na hata jina lake jimboni halitarejea tena kwani hana wapiga kura alipata ubunge kwa upepo wa magufuli
 
Amemgonga mara 3?
 
Back
Top Bottom