Waitara, walimu wamekukosea nini?

Waitara, walimu wamekukosea nini?

Oxpower

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2012
Posts
2,181
Reaction score
3,115
KWAKO NAIBU WAZIRI WAITARA

Kuna wakati tunaumia sana na kuishi kwa hofu kubwa, kwa sababu kuna mambo tunayaogopa sana kuyakabili, na hayo ndiyo huonyesha udhaifu wetu, na huleta kunyanyasika na kila unapoyakumbuka yanakukosesha amani kabisa, UNAPOKOSA AMANI TAYARI UNAKUWA KWENYE HATARI YA KUSHINDWA.

Tukirejea tamko lako ulilofanya tar24 april ulipotamka kwamba kuhama kumesitishwa mpaka kibali maalumu huku ukisisitiza kwamba hilo litahusu walimu kwakuwa WALIMU NI WAONGO.

Siandiki hapa kuonyesha kwamba mimi sijashindwa ,hapana si lengo langu,lengo langu ni kukukumbusha tu kwamba walimu ni watu smart saaana.labda nikuulize

UMEITA WALIMU WAONGO WAMEKAA KIMYA.
Umejisikiaje?unajionaje,?umadhan walimu ni wapole sana?unadhan walimu hawana hasira?unadhan walimu hawawezi kukujibu?.

Hapana si kweli ,unachotakiwa kufahamu ni kwamba walimu sio chama cha Siasa,wao wanaishi kwa utaratibu na kanuni za utumishi.binafsi sijawahi kukufatilia sana kwenye siasa ila nachokifahamu kuhusu wewe ni kwamb ulikua CHADEMA na huko kazi yako huko ilikuwa ni kutukana CCM ,

Na bahati uliyoipata ni kwamba wakereketwa wa ccm wakawa wanakujibu na hapo ndipo ukapata umaarufu....

Huko kwenye siasa huwa mnajibizana kwakua mnataka kura na umaarufu .

je walimu wamekufanya nini?
Kuna watu wanahama kwa ajili ya kwenda kuuguza wazazi wao ambao wapo taabani vitandani,

kuna watu wanataka kunusuru ndoa zao, kuna watu wanataka wasogee kwenye mikoa yenye fursa za Kielimu

Huyu Mwalimu wa Tanzania kawafanyia nn?... je mnataka waalimu wavue unyonge na kuanza kupambana kudai haki?

Kuna mwenzio wakati yupo iringa hata jina simjui anatishia et walimu wakitaka kuhama waache kazi,? Ni nani kawamilikisha nchi nyie,hii nchi ni yetu hivyo ni lazima tuishi kwa kufata utaratibu tuliojiwekea.

WANYONGE WAKICHOKA HUGEUKA WAASI
 
Huyo licha ya kuwa chapombe, alishauza nafsi yake gizani. Hajitambui.
 
wateule wa awamu hii wanajifanya malaika!!!! ila Mungu yupamoja nasi!!!!
 
kuna song la wagosi lilibamba sana! walimu tuna hali ngumu! walimu
 
Njaa tu jitu linakua na tabia za kike juzi tu alikua anabwabwaja kuhusu serikali leo hii kupata cheo anawageuka tena walewale aliokua anajifanya anawatetea ila hili ni funzo kwa watanzania wote tusijihusishe na wanasiasa ni wachumia matumbo tu Waitara Mungu anakuona na utaishia kufa tu na hutakumbukwa kwa lolote we endekeza njaa tu utaona mwisho wake
 
Du!!!!!!

Njaa inamsumbua sana.hatujasahau matusi yake kwa ccm
 
Back
Top Bottom