Waitara, walimu wamekukosea nini?

Waitara, walimu wamekukosea nini?

Huwa najiuliza sana,hawa wanasiasa njaa huwa wanamuda wakujiuliza wao ni kina nani na role yao katika jamii ,
Watu kama waitara sidhani km hua anajiuliza hilo swali angekua yy ndio jafo sijui ingekuwaje mkurya yule sio mstaarab kabisa jamaa
 
Watu kama waitara sidhani km hua anajiuliza hilo swali angekua yy ndio jafo sijui ingekuwaje mkurya yule sio mstaarab kabisa jamaa
Hata mimi naamini huwa hawapati huo muda kabisa .hapo ni naibu tu
 
Hapo kwenye kipande cha kuuvua unyonge ndo cha muhimu mkikazia hapo na mlivyo wengi wataomba poo.
 
Huyu jamaa wakati alipokuwa rais wa chuo pale udsm miaka ile ya katikati mwa 2000, alikuwa smart sana kwenye kutetea maslahi ya wanachuo mfano boom lilipochelewa kutoka, aliongoza mwenyewe migomo na maandamano hadi haki ilipopatikana.

Naona tangu ameingia kwenye siasa, nguvu kubwa anaitumia kulipigania tumbo lake. Ni vyema wangerudisha ule mfumo wa kubadilishana vituo vya kazi na si kuwazuia kabisa watumishi kuhama. Madhara ya hii kitu ni kwa serikali maana hao watumishi kimwili watakuwa kwenye vituo vyao vya kazi ila kiakili watakuwa wanaziwazia familia zao tu na hivyo kudhorotesha utendaji wa kazi.
 
Umeandika kwa hisia sana, waitara yumo humu na huu uzi ameuona na anafatilia michango ya wanajukwaa!!
Kila siku nasema walimu wote kwa umoja anzeni leo na watoto walioko mashuleni, chekechea na darasa la kwanza muwafundishe na kuwalea katika misingi ambayo watatambua thamani na mchango wa walimu hata watakapo kuwa wakubwa na kuwa viongozi hawatakua na kiburi, jeuri na ujasiri wa kucheza na haki za walimu! Kwa kufanya hivi miaka 30 ijayo kada ya ualimu itakuwa ikizungumzwa kwa namna nyingine kabisa tofauti na leo.
Gari likishindwa kupita kwenye kijimuinuko fulani hurudishwa nyuma hatua kadhaa na huja na nguvu mpya.. RUDINI NYUMA HATUA KADHAA MJE NA NGUVU MPYA!
 
Back
Top Bottom