WAITARA: Ndani ya kanisa la Ufufuo na Uzima kwa Askofu Gwajima, ajiita Simba

Mbunge Waitara ambaye pia ni mbunge wa jimbo la UKONGA ambapo alikuwa ameongozana na aliyewahi kuwa mbunge wa MUSOMA MJINI Mh. Vicent Nyerere ambao wote kwa pamoja walikuwa wageni katika kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Dkt. Gwajima

Ambapo amesema kwamba alifaamiana na Askofu Gwajima alipokuwa Mahakama ya Kisutu ambapo wote kwa pamoja walikuwa wameshitakiwa, ambapo alishitakiwa akiwemo yeye, mbunge wa Ubungo, Said Kubenea na madiwani wengine 9 wa manispaa ya Ilala kwa kutaka kuvuruga uchaguzi wa meya ambapo kesi hiyo ilidumu kwa mwaka 1 na baadae kushinda.

Huku akijiita Leo maana yake Simba. Asema kwamba kuwa mbunge wa UKONGA ni kwamba hajazuka tu, asimulia pia maisha yake ikiwepo shule na chuo alichosoma akiwa mkoani Dar es salaam.
77aab977ec92394cf0ec56f089f92ee4.jpg

Auzungumzia pia MWENGE ambao unatumia gharama nyingi katika kuuendesha kuanzia posho, mafuta ya gari, misafara mirefu, kunywa, kula na watu kukesha.

Aiponda bajeti iliyopita ambayo serikali iliinadi kwamba ni bonge la bajeti haijawahi tokea, na kuzungumzia maswala ya Bungeni kutunga na kusimamia sheria mbalimbali kwa wananchi wake.

Hapo ni kanisani wala sio jukwaa la kisiasa,...hakupaswa kuyasema hayo yote madhabahuni, ilimpasa kuomba na kupata upatanisho wa nafsi yake na muumbaji wake.

Hili likiachwa liendelee litapoteza credibility ya ya Gwajima na kanisalake lak8ni pia dini ya Kikristo itatafsiriwa kama sehemu ya kupiga siasa. Hofu yangu ni je wabunge au wanasiasa wengine wakisimama katika mimbari ya misikiti na kufanya walichofanya wanasiasa hawa kwa Gwajima reaction yake itakuwa vipi?
 
Alichokifanya makonda leo kwenye mashindano ya kusoma quran ni ini kama sio siasa. Au siasa ni pale tu wanapoongea wapinzani
Makonda hatangazi siasa bali anaeleza Serikali ya Mkoa na Serikali kuu kinachofanywa kuhusu wana Dares salam.

Na hilo ni jukumu la serikali la watanzania halikwepeki sio siasa.
 
Wako sahihi kabisa, kwani pia kwa sasa hawana ajenda mpya- yawezekana Gwajima ndo mtabili wao 2020
 
Back
Top Bottom