WAITARA: Ndani ya kanisa la Ufufuo na Uzima kwa Askofu Gwajima, ajiita Simba

Erick Richard R-Madrid

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
399
282
Mbunge Waitara ambaye pia ni mbunge wa jimbo la UKONGA ambapo alikuwa ameongozana na aliyewahi kuwa mbunge wa MUSOMA MJINI Mh. Vicent Nyerere ambao wote kwa pamoja walikuwa wageni katika kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Dkt. Gwajima

Ambapo amesema kwamba alifaamiana na Askofu Gwajima alipokuwa Mahakama ya Kisutu ambapo wote kwa pamoja walikuwa wameshitakiwa, ambapo alishitakiwa akiwemo yeye, mbunge wa Ubungo, Said Kubenea na madiwani wengine 9 wa manispaa ya Ilala kwa kutaka kuvuruga uchaguzi wa meya ambapo kesi hiyo ilidumu kwa mwaka 1 na baadae kushinda.

Huku akijiita Leo maana yake Simba. Asema kwamba kuwa mbunge wa UKONGA ni kwamba hajazuka tu, asimulia pia maisha yake ikiwepo shule na chuo alichosoma akiwa mkoani Dar es salaam.
77aab977ec92394cf0ec56f089f92ee4.jpg

Auzungumzia pia MWENGE ambao unatumia gharama nyingi katika kuuendesha kuanzia posho, mafuta ya gari, misafara mirefu, kunywa, kula na watu kukesha.

Aiponda bajeti iliyopita ambayo serikali iliinadi kwamba ni bonge la bajeti haijawahi tokea, na kuzungumzia maswala ya Bungeni kutunga na kusimamia sheria mbalimbali kwa wananchi wake.
 
Nilishawahi kusema gwajima akinyanyua miguu yote miwili akakanyaga hakuna wa kumzuia ila sasa kashanyanyua amebakiza kukanyaga ila wasoma nyota walilijua hili mapema wakaamua kumthibiti ili nimeamini huwezi shindana na nyota ya mtu hata kama ni muovu akisha pigiwa mstari hesabu basi.
 
Back
Top Bottom