Waitara: Mawakala wa CHADEMA walinipigia kura

Waitara: Mawakala wa CHADEMA walinipigia kura

Joined
Sep 17, 2018
Posts
7
Reaction score
14
Mbunge mteule wa Ukonga Mwita Waitara Baada ya kutangazwa kama mshindi katika uchaguzi mdogo wa marudio katika jimbo hilo amesema mawakala wa CHADEMA katika vituo vya kupigia kura walimpigia yeye.

Akiongea leo baada ya kutangazwa, Mwita amesema alikuwa na matarajio ya kushinda kwa zaidi ya asilimia 95, hivyo hajashangaa kupata ushindi huo wa asilimia 89.

''Nina ushahidi wa ujumbe mfupi kwenye simu yangu, mawakala wa CHADEMA katika vituo jana wamenipigia kura na walikuwa wananitumia matokeo mapema tu hiyo inaonesha nilikuwa na uungwaji mkono mkubwa sana'', amesema.

Aidha Mwita amekishauri chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kujitazama kilipojikwaa na sio kilipo angukia huku akiweka wazi kuwa kama wanataka chama kibakie waachane na mwenyekiti wao Freeman Mbowe na wakiendelea kumkumbatia chama kitawafia.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi leo, msimamizi mkuu wa uchaguzi jimbo hilo, Jumanne Mashauri amemtaja Mwita Waitara wa CCM kama mshindi wa kiti cha ubunge baada ya kupata kura 77,795 sawa na asilimia 89.1 huku mpinzani wake, Asia Daudi Msangi ( CHADEMA) akipata kura 8,676 sawa na asilimia 9.95.

Muungwana
 
Yaani hujuma zoote serikali inazomfanyia Mbowe kwenye vitega uchumi vyake hajateteleka na wanachama wake hawajaacha kumuunga mkono, seuze wewe kupewa ubunge na polisi ndio kuwasababishie waache kumuunga mkono?!
 
Huyu akili zake zitamrudia uchaguzi wa 2020, atajutia hizi kauli chafu anazozitoa, CCM watamtupa kama hawamjui. Amalizie hiki kipindi kilichobaki na asahau kuhusu ubunge.
2020 watarudia uhuni huu huu ndiyo maana wana guts
 
2015 anakumbuka shida walizopata watu, katika kumpigania asiporwe ushindi wake pale Ukonga na hao hao mafioso wa sisiemu.. Leo 2018 amevuka ameenda kwa hao hao Mafioso wa sisiemu, na kwa pamoja ameshiriki kufanya yale yale ambayo sisiemu walijaribu kuyafanya 2015.. Ila kwa sasa sisiemu imeenda mbali, sasa hawaibi tena, wanapora haki mchana kweupee.. Atakaejaribu kusimama na kuzuia uporaji kifo kinamuita..
 
Yaani hujuma zoote serikali inazomfanyia Mbowe kwenye vitega uchumi vyake hajateteleka na wanachama wake hawajaacha kumuunga mkono, seuze wewe kupewa ubunge na polisi ndio kuwasababishie waache kumuunga mkono?!
Mkuu ina ushahidi
 
2015 anakumbuka shida walizopata watu, katika kumpigania asiporwe ushindi wake pale Ukonga na hao hao mafioso wa sisiemu.. Leo 2018 amevuka ameenda kwa hao hao Mafioso wa sisiemu, na kwa pamoja ameshiriki kufanya yale yale ambayo sisiemu walijaribu kuyafanya 2015.. Ila kwa sasa sisiemu imeenda mbali, sasa hawaibi tena, wanapora haki mchana kweupee.. Atakaejaribu kusimama na kuzuia uporaji kifo kinamuita..
Huyo anasumbuliwa na nafsi yake kwa alichokifanya baada ya kununuliwa.
 
Huyu akili zake zitamrudia uchaguzi wa 2020, atajutia hizi kauli chafu anazozitoa, CCM watamtupa kama hawamjui. Amalizie hiki kipindi kilichobaki na asahau kuhusu ubunge.
kwani amekuahidi kwamba 2020 atagombea?
 
Huyu akili zake zitamrudia uchaguzi wa 2020, atajutia hizi kauli chafu anazozitoa, CCM watamtupa kama hawamjui. Amalizie hiki kipindi kilichobaki na asahau kuhusu ubunge.
Hata wewe ukute ulimpigia kura jana. Tumeshawajua nyie humu kelele ila uwanjani mnaunga mkono juhudi.
 
haa haa. huu. ni uwongo mtupu. huyu karudishwa bungeni kwa hila za tume na polis....
 
Back
Top Bottom