Waislamu Elimu Ahera siyo kila kitu, wapeni watoto Elimu Dunia pia

My Honest Book

JF-Expert Member
Jul 7, 2015
1,356
2,100
Naomba nieleweke kwa uzuri kabisa, isionekane nimeamka na kuamua kuchoose violence kwa ndugu zangu waslamu, hili swala limetokana na tabia moja ambayo naamini inafanywa na waislamu naiona haiko sawa hata kidogo zaidi ya kuharibu future za watoto wa maskini.

Ninachokisema hapa nimekishuhudia mwenyewe kwa kuwahoji hawa watoto.

Ni hivi, kuna hii trend ya kujengwa misikiti kila sehemu, na hii inatokana na watu wanaojua namna ya kuzipata pesa za Waarabu kwa kutumia proposal ya kujenga misikiti yenye hostel.

Sasa ishu inakuja kwa hao watoto wanaosomeshwa kwenye hiyo misikiti, asee unakuta wanachukuliwa mikoani huko ndani ndani kwenye familia maskini ambazo zimeshindwa kuwapeleka watoto wao wakapate elimu dunia ya bure ya Magufuli, lakini unakuta hawa mabwana wenye pesa za Waarabu badala ya kuwapeleka shule wakasome vizuri instead wanawachukua hawa watoto ambao hawajui kusoma wala kuandika ila wanapewa elimu ahera peke yake.

Hawa watoto wananyimwa fursa nying sana kwenye maisha yao, kwasababu watabaki kuwa mashehe tu kama fursa peke yake watakayoweza kuifanya ukubwani.

Hili nimelikuta Mbeya mjini sehemu inaitwa Majengo, nilimkuta dogo mmoja ustadhi anayeswali msikiti huo huo ila yeye anasoma Udaktari Rufaa Mbeya, nikamuuliza kuhusu hilo swala akabaki anajiuma tu.

Ushauri: Vipi kama mkikubaliana kama misikiti ishatosha, hivyo hizo pesa za Waarabu mzitumie kuwasomesha hao watoto, muwapeleke shule nzuri za kislamu wapate elimu zote kwa pamoja kuliko kuforce kujenga misikiti sehemu ambazo uislamu hakuna. Kama Mbeya misikiti mingi ila waumini wa kutafuta, kisa pesa za bure kutoka uarabuni.

Nawasilisha,
Kwasasa nipo Arusha.

SON OF ANDREW
 
Ni kweli!!

Uko Arusha kuwa makini huko ndo wapo kibao wanajazana ,Nimeishi Tanga karibu na msikiti wa shamsil maarifa mapinduzi wanaita kma sijakosea .

Ila madrsa hata watu wa Tanga wengi hwasomi ila warangi na Watu wa Arusha wako kiboa pale na hyo elimu dunia hWana time nayo wanasoma mpaka miaka 7 unakuta mtu yuko pale..Best ukaanza kurekebisha hii Tabia huko kwenu Arusha ndo wanajazana sana TAMTA ,ZAHRAU na SHAMSIL MAARIFA.
 
Naomba nieleweke kwa uzuri kabisa, isionekane nimeamka na kuamua kuchoose violence kwa ndugu zangu waslamu, hili swala limetokana na tabia moja ambayo naamini inafanywa na waislamu naiona haiko sawa hata kidogo zaidi ya kuharibu future za watoto wa maskini...
Sawa ustaadhi ili baadaye wasije lia kwa kusema wale ‘makafir’ wanapendelewa kwenye ajira na maendeleo!
 
Waacheni wawape elimu hiyo ila baadae hatutaki lawama kwamba sjui wakristo wanapendelewa kwenye mafasi nyeti maana kama mliwekeza kwenye elimu ya dini mkaacha elimu ya dunia ambayo ndio itawapa vijana wenu fursa lawama hatutaki.

Unajua baada ya miaka 10 tu matunda tutayaona wao waache kubalance mambo wamsikilize muarabu na sheria zake hakuta kua na hata mmoja atakaye weza kuongoza nchi mtabaki lawama tu
 
Hizi ni propaganda mkuu, jamii zote christian na muslim huwa watoto wakiwa wadogo hupitia madrasa au sundaschool kupata elimu ahera na kumjua mwenyezi Mungu.

Wakati wakristo wanakwenda Sunday school na waislam wanakwenda madrasa pia, wapo waislamu waliopita madrasa na kupata elimu ahera vizuri tu na wakati huohuo pia wakiwa na elimu dunia kwa kiwango kikubwa tu kama ilivyo kwa wakristo pia.

Kwanini Waislamu wengi hawana hiyo elimu inaitwa Elimu dunia? hili ndio swali la kujiuliza kuliko kulaumu elimu ya madrasa.

Kila unachokiona Tanzania na duniani Tambua kiko hivyo kwa makusudi sio bahati mbaya hata hili la waislamu kutokwenda shule lipo kwa makusudi sio bahati mbaya na kuielewa hiyo kusudi unapaswa kuwa na fikra huru.
 
Waacheni wawape elimu hiyo ila baadae hatutaki lawama kwamba sjui wakristo wanapendelewa kwenye mafasi nyeti maana kama mliwekeza kwenye elimu ya dini mkaacha elimu ya dunia ambayo ndio itawapa vijana wenu fursa lawama hatutaki.

Unajua baada ya miaka 10 tu matunda tutayaona wao waache kubalance mambo wamsikilize muarabu na sheria zake hakuta kua na hata mmoja atakaye weza kuongoza nchi mtabaki lawama tu
Na mwarabu wangejua sio mtu mwenye upendo kihivyo eti ahangaike kwa ajili ya ahera ya wabongo! Hapo anawaplease‘ miungu’ wake tu aendelee kupata hela. Kuweni na akili zenu!
 
Naomba nieleweke kwa uzuri kabisa, isionekane nimeamka na kuamua kuchoose violence kwa ndugu zangu waslamu, hili swala limetokana na tabia moja ambayo naamini inafanywa na waislamu naiona haiko sawa hata kidogo zaidi ya kuharibu future za watoto wa maskini.

Ninachokisema hapa nimekishuhudia mwenyewe kwa kuwahoji hawa watoto.

Ni hivi, kuna hii trend ya kujengwa misikiti kila sehemu, na hii inatokana na watu wanaojua namna ya kuzipata pesa za Waarabu kwa kutumia proposal ya kujenga misikiti yenye hostel.

Sasa ishu inakuja kwa hao watoto wanaosomeshwa kwenye hiyo misikiti, asee unakuta wanachukuliwa mikoani huko ndani ndani kwenye familia maskini ambazo zimeshindwa kuwapeleka watoto wao wakapate elimu dunia ya bure ya Magufuli, lakini unakuta hawa mabwana wenye pesa za Waarabu badala ya kuwapeleka shule wakasome vizuri instead wanawachukua hawa watoto ambao hawajui kusoma wala kuandika ila wanapewa elimu ahera peke yake.

Hawa watoto wananyimwa fursa nying sana kwenye maisha yao, kwasababu watabaki kuwa mashehe tu kama fursa peke yake watakayoweza kuifanya ukubwani.

Hili nimelikuta Mbeya mjini sehemu inaitwa Majengo, nilimkuta dogo mmoja ustadhi anayeswali msikiti huo huo ila yeye anasoma Udaktari Rufaa Mbeya, nikamuuliza kuhusu hilo swala akabaki anajiuma tu.

Ushauri: Vipi kama mkikubaliana kama misikiti ishatosha, hivyo hizo pesa za Waarabu mzitumie kuwasomesha hao watoto, muwapeleke shule nzuri za kislamu wapate elimu zote kwa pamoja kuliko kuforce kujenga misikiti sehemu ambazo uislamu hakuna. Kama Mbeya misikiti mingi ila waumini wa kutafuta, kisa pesa za bure kutoka uarabuni.

Nawasilisha,
Kwasasa nipo Arusha.

SON OF ANDREW
Boko haramu=western education is haramu.

Hawawezi kukuelewa ndivyo walivyofundishwa na mabwana zao waarabu.

#MaendeleoHayanaChama
 
ulishawahi kumuona mtu mwenye elimu ya dini ya kiislam anaomba omba?
Hyo ni elimu Kama elimu nyingine.
Usiidharau sababu kupitia hyo elimu maisha yao yanaenda na wanaishi.

acha kudanganya .ikifika siku ijumaa nenda kariakoo wanavojazana kuomba omba wakipita madukani na kusubiri matajiri .wengine wazima kabisa mpaka unajouliza wimbi lote nini.

unataka elimu ya dini ikatumike kurusha ndege au kutengeneza madaraja !.
 
Mleta uzi malizana kwanza na matatizo ya dini yako hauna huruma ya kiasi icho kwa waislam, mbona waislam wasomi ni wengi sana kwenye hii nchi tena baada ya izo kasumba kutokea waislam wengi wakaingia kwa kasi kwenye elim dunia fanya research
Na ushasema watoto wanachukuliwa vijijini wanaenda kusomeshwa elim ahera lipi bora apo waachwe wasipate elim yyte ile au wabaki vijijini waendelee kuchunga mbuzi? Ni bora wapate ht iyo elim ya dini wapate ustaarabu kidogo wawe watu wa ibada wizi upungue mtaani umalaya upungue ushoga na utapeli upungue
Mwisho wa siku mifumo ya elimu dunia serikali yenyew kama imefeli ivi ndio elim bure lakini ukienda vijijini uko utaona ubovu wa iyo elim

Mada kama izi zakipumbavu tu
 
Unaona Sasa unavyochanganya mada.
Wale omba omba wamekwambia wamesoma madrasa ipi?
Hao ni omba omba hawana tofauti na wale wagogo.kila Quran kichwani hawana.huo ndo ukweli.
Uenda hawakusoma madrasa Wala shule Ila ni waislam.
acha kudanganya .ikifika siku ijumaa nenda kariakoo wanavojazana kuomba omba wakipita madukani na kusubiri matajiri .wengine wazima kabisa mpaka unajouliza wimbi lote nini.

unataka elimu ya dini ikatumike kurusha ndege au kutengeneza madaraja !.
 
Waacheni wawape elimu hiyo ila baadae hatutaki lawama kwamba sjui wakristo wanapendelewa kwenye mafasi nyeti maana kama mliwekeza kwenye elimu ya dini mkaacha elimu ya dunia ambayo ndio itawapa vijana wenu fursa lawama hatutaki.

Unajua baada ya miaka 10 tu matunda tutayaona wao waache kubalance mambo wamsikilize muarabu na sheria zake hakuta kua na hata mmoja atakaye weza kuongoza nchi mtabaki lawama tu

Mngaliiwacha Zanzibar ikajiendesha yenyewe kama zamani , mtaona nini waislamu wanafanya
 
WAISLAMU WA KONDOA HAWAENDI KABISA SHULE. Wanasema kwao Formal Education ni haramu.
Wanasoma Madrasa tu.

ILA MOOD MZONGUAJI SANA.

KAIBA MA CHARACTER ISLAEL.
HUKU YEYE ALIKUWA AKIISHI MAKA NA MADINA.

MOODY HOVYO.

Haya ndiyo mafundisho ya Yesu ??

Sina kawaida ya kuwafundisha watu kwa maneno yangu bali nawafundisha kulingana na maandiko yao matakatifu.

Sasa tuone hali na imani ya wanafunzi wa Bwana Yesu.

1. Yesu alisema, hata sasa ninyi nanyi mngali hamna akili? (Mathayo15:16).

2. Alimwambia Petro kwamba; “Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka? (Mathayo 14:31).

3. Petro alikanusha kuwa mfuasi wa Yesu mara tatu bali alimlaani. (Mathayo 26:69-75).

4. Yuda Iskariote alimuuza Yesu kwa shilingi 30 tu. (Mathayo 26:15).

5. Wakati Yesu alikuwa hatarini, wanafunzi waliendelea kulala). Mathayo 26:40-45; Marko 14:36:041).

6. Yuda alijinyonga. (Mathayo 27:5).

7. Imani ya wanafunzi: “Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu” (Mathayo 17:20).

8. Ndipo wanafunzi wote wakamwacha wakakimbia. (Mathayo 26:50).

9. Wengi wataniambia siku ile; Bwana, Bwana hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri. Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu. (Mathayo 7:22-23).

Hapa juu umesoma hali na imani ya wanafunzi wa Bwana Yesu sawa na Biblia.

Lakini sisi Waislamu hatuamini kwamba Nabii yeyote anaweza kushindwa kiasi hiki kwamba asiweze kupata matunda ya juhudi yake na athari nzuri isitokee kwa mahubiri na mafundisho yake.

Hata katika Qur'an Tukufu wanafunzi wa Bwana Yesu wametajwa kuwa mfano mzuri juu ya ulimi wa Bwana Yesu menyewe.

Qur'an: “Enyi mlioamini! Muwe wasaidizi wangu kwa Mwenyezi Mungu kama alivyosema Isa bin Mariam kuwaambia wanafunzi (wake): Ni nani wasaidizi wangu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu? Wanafunzi wakasema: Sisi ni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu.” (Qur'an 61:15
 
Back
Top Bottom