Patriot
JF-Expert Member
- Feb 11, 2008
- 5,753
- 4,866
Jana, waziri mkuu, Mizengo Kayanza Pinda ametoa ahadi kwamba mahakama ya kadhi, eti itatungiwa sheria pekee bunge la Januari. Tamuko hili lililenga kushawishi kura za waislamu waone kwamba katiba hii inawajali.
Naomba niseme ahadi hii ni feki na ilistahili itolewe kwa watu wasio na akili. Alichokifanya Pinda ni kuonyesha kwamba Waislamu ni wajinga. Hilo ni bunge la katiba. Bunge hili halina msemaji wa serikali na wote ni wabunge kwa uzito mmoja. Mwenyekiti wa Bunge naye ni FEKI tena feki kweli kweli maana hakupaswa kutoa ruhusa kama hiyo, eti Pinda anatoa kauli kama kiongozi wa serikali ndani ya bunge la katiba. Hii ni mara ya pili baada ya ile ya Rose Migiro kutoa kauli juu ya uamuzi wa mahakama kuu.
Kwa uelewa wangu, binafsi sina ushabiki wowote na mahakama ya kadhi na nimesema mara nyingi kwamba hizi siyo enzinza mahakama za kidini kwa nchi kama TZ, lakini yaonekana wanaoishabikia wametoa meno kwa kudhani eti wamepewa ahadi. Hiyo ni ahadi feki. Bunge la Januari halitaweza kuwa na uhusiano wowote na bunge la katiba, wakati ambao hata katiba yenyewe itakuwa haipo.
Huuu ndo upuuzi unaoendelea bungeni.