Waislam waunge mkono hoja ya katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waislam waunge mkono hoja ya katiba mpya

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Mkorosai, Dec 23, 2010.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. M

  Mkorosai Member

  #1
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waislam wanapaswa kuunga mkono hoja ya Katiba mpya kwa nguvu zao zote ili hoja zao za kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi ziweze kujadiliwa kwa uwazi na ikiwezekana zitambuliwe rasmi. Kitendo kinachofanywa hivi sasa kutaka kuzianzisha mahakama hizo kinyemela hazitawasaidia sana.

  Kwa Watanzania wote, tunahitaji Katiba mpya ambayo itaweka kila kitu bayana, katiba itakayo linda haki zetu wananchi, kupunguza Madaraka ya Rais (wajao) na kuweka mstakabali wa taifa letu hasa masuala ya Muungano.

  Nawashauri Waislam wajitokeze zaidi wabebe bango ili katiba hii tuliyoachiwa na Wakoloni wa Kiingereza na kubandikwa viraka kibao, iondolewe na kuweka Katiba yetu itakayoweka usawa wa kuabudu ( why sunday a holiday and not friday), usawa wa kushiriki kwenye siasa na kuiweka nchi yetu kwenye mstari tutakaopenda wote kwa pamoja.
   
 2. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huu ni udini au????
   
 3. M

  Mkorosai Member

  #3
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kuhamasishana tu ili Hoja ya Katiba iungwe mkono na kila sekta. Hata Wazanzibar wanao hisi kuwa muungano wa serikali mbili hauwafai, wanapaswa sasa kuinga mkono kwa nguvu hoja ya mabadiliko ya Katiba ili tujadili kwa uwazi ni muungano wa namna gani tunauhitaji! Hata Watanzania Bara kwa pamoja nao waunge mkono hoja hii maana Zanzibar inaonekana kufaidika zaidi na Muungano kuliko wao. Kila kundi lina sababu ya kuunga mkono hoja ya mabadiliko ya katiba.
   
 4. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #4
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Nina itilia mashaka approach yako ya ku-foster uanzishwaji wa katiba mpya

  Yaani washinikize katiba mpya kwa ajili ya Kadhi tu?? Je hili ndilo hitaji pekee kuu walilonalo??

  If so.......naomba niweke kamguno kidogo (mmmhhhh!!!!!!!!)
   
 5. M

  Mkorosai Member

  #5
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  waislam kama waislam wanazo hoja nyingi wanazohitaji katika katiba!! wana issues zinazo wahusu zinazopaswa kujadiliwa kwa uwazi na ikiwezekana ziwekwe kwenye katiba! si suala la Kadhi tu, wala siku ya ibada! Hata katiba kuandikiwa Lancaster nyumbani kwa wakoloni ambako hawaenzi uislam bado ni issue ya kuwataka wadai katiba mpya iliyoandikiwa hapa hapa na ambayo itawajali na kuchukuwa maoni yao!
   
 6. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #6
  Dec 23, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kwenye red;katiba tuliyoachiwa na mkoloni ina mahakama ya kadhi, hii ni katiba ya nyerere. katiba ya nyerere ndo ilifuta mahakama ya kadhi ambayo mkoloni alituachia. akwa hiyo tafadhalini tusiseme kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi, BALI TUSEME KUREJESHWA KWA MAHAKAMA YA KADHI kwani nyerere tu na kakikundi chake walifuta. Just think, kama wakoloni wenyewe waliona umuhimu wa mahakama ya kadhi inaingiaje akilini waafrika na wa Tanzania wenzetu wasione umuhimu wake?
  NB, mahakama ya kadhi ipo sehemu nyingi ambazo hata waislam si wengi kivile sembuse hapa TZ ambako waislam ni above 50%? Does not make any sense.
   
 7. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #7
  Dec 23, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  katiba ni ya waTZ hakuna haja ya kuwaomba wakristu wala waislamu.

  Done.
   
 8. K

  KALAMAZOO JF-Expert Member

  #8
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katiba mpya ni muhimu kwa taifa bila kujali itikadi ila nadhani kwa waislam ni muhimu sana kwa sababu kuna mamabo mengi kwenye katiba ya sasa hawapewi haki sawa.Fursa ya kujadili katiba mpya ikipatikana ndo itajulikana kwamba kumbe hata wale wanaodaiwa kusoma madrasa wanajua kutetea pointi.Lazima waumini siku zao za kuabudu ziheshimike hakuna kupiga kura siku ya jumapili na kuwanyima fursa wakristu haki yao ya ibada,vilevile pia siku ya ijumaa iwe ni mapumziko ili kuwapa waislam muda wa ibada nk.
   
 9. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #9
  Dec 23, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Binafsi sioni busara kwa viongozi wa dini kuhamasisha juu ya katiba mpya. Wawe Waislamu au wawe Wakristo.
  Kwa sababu hata hiyo katiba mpya sidhani kama itakidhi matakwa ya dini zote hizo.
   
 10. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #10
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Hatuhitaji ikidhi 100% , tunahitaji a harmonized constitution.
   
 11. Mwadui

  Mwadui Senior Member

  #11
  Dec 23, 2010
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 102
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  huu sio udin bali ni ukweli kwani hii katiba ya sasa inambana kila mtu, hivyo kila taasisi itumie mwanya huu kudai katiba mpya.
   
 12. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #12
  Dec 23, 2010
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hapa tunawahitaji waislamun ili kufikia malengo yetu ya kisiasa! Vingenevyo ni wavivu, wasio soma n.k! Huu ndo unafiki wa watu wa JF. Wanavyowatukana waislamu humu kama wenyewe wangekuwepo they would stay millions of miles away from CDM and Christian community.
  Nimekuwa niki-advocate kuwa na platform ambayo haibagui dini kwa sababu mahitaji yetu kama nchi hayabagui dini lakini unaambulia matusi kejeli na utoto wa akini Quinine, Rev Masinilo and the rest of fanatical wild bunch!
  Nadhani tuendelee wenyewe tu tuliosoma!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 13. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #13
  Dec 23, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Waislam waandaa rasimu ya katiba mpya Send to a friend Wednesday, 22 December 2010 20:10 0diggsdigg

  Salim Said
  KILIO cha makundi mbalimbali ya kijamii na kisiasa katika kudai katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kimechukua sura mpya baada ya Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislaam (T), kuanza mchakato wa kuandaa rasimu ya katiba hiyo ambayo itawasilishwa serikalini ndani ya siku 30.
  Hatua hiyo imekuja baada ya taasisi hiyo, kuamini kuwa suala la katiba mpya halina tena mjadala kutokana na umuhimu wake kwa taifa.

  Hatua hiyo inakuja wakati taasisi za kijamii, kisiasa, kidini na hata watu binafsi, zikiibuka na kudai katiba mpya.
  Siku kadhaa zilizopita Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alisema atamshauri Rais Jakaya Kikwete, kuangalia namna ya kuanzisha mjadala wa kitaifa, kama mchakato wa kuandika katiba mpya.

  Lakinin kauli hiyo ya Pinda ilitofautiana na ya Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani na Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, ambao kwa nyakati tofauti, walisema kwa sasa, hawaoni haja ya kuandikwa kwa katiba mpya.

  Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislaam Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, alisema kwa kuona umuhimu wa suala hilo katika mustakbali wa taifa, taasisi imeanza mchakato wa kuandaa rasimu ambayo wataiwasilisha serikalini.
  "Kwa muktadha huu, tumeanza kuandaa mapendekezo muhimu ya Waislaam na Tanzania ya sasa na siyo ya jana katika katiba mpya, pia tutatahadharisha baadhi ya mambo katika katiba hiyo," alisema Sheikh Ponda.

  "Lengo ni kuhakikisha kwamba tunapata katiba inayokwenda na wakati, itakayojenga na kulinda haki, misingi ya usawa,amani na kuleta ustawi mzuri wa taifa." alisisitiza.
  Alisema rasimu hiyo itawasilishwa mara baada ya kukamilika na kwamba itajumuisha mawazo ya Waislaam wa mikoa yote nchini.

  Kwa mujibu wa Sheikh Ponda, mawazo hayo yatakusanywa kwa njia ya semina na makongamano maalumu kuhusu elimu juu ya umuhimu wa katiba mpya.

  "Pia tunaomba kila Mtanzania mwenye mapendekezo mazuri ya kuivusha nchi yetu na kudumisha amani kwa ajili ya katiba mpya, kuyafikisha katika ofisi za taasisi yetu au kwa kutumia anwani zake," alisema Sheikh Ponda.

  Alisema Waislaam wanaamini kuwa suala la katiba mpya ni la muhimu katika kuleta demokrasia na uhuru wa kweli.
  "Suala hili si la mtu au taasisi moja kujifungia chumbani na kuandaa bali ni suala linalohitaji njia shirikishi kwa makundi yote ya kijamii," alisema.
   
 14. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #14
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Hapo ni Mwanzo mzuri, Ushikiano muhimu sasa.

  Staki kuskia hii katiba wengine waseme

  Ooh ya bakwata

  Ooh ni Onswar Suna.

  Ooh ni msikiti fulani!!

  Hili ni Suala la kitaifa tusiendekeze makudi yasiyo na maana.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...