Waislam Wapigwa Stop na Kova

Waislam Wapigwa Stop na Kova

Bramo

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2009
Posts
13,230
Reaction score
10,201
Walikuwa wanatarajia kuandamana kuhamasisha wananchi wasichague CCM, Wanadai CCM iliwahadaa katika ILANI yake ya mwaka 2005 ya kuanzisha mahakama ya kadhi.

Afande kova anasema kuwa Mufti wa Tanzania ameshalitolea ufafanuzi suala hilo so No Maandamano..

Ha ha habari ndo hiyo, haha...habari ndo hiyo
 
Walikuwa wanatarajia kuandamana kuhamasisha wananchi wasichague CCM,Wanadai CCM iliwahadaa katika ILANI yake ya mwaka 2005 ya kuanzisha mahakama ya kadhi,Afande kova anasema kuwa Muft wa Tanzania ameshalitolea ufafanuzi suala hilo so No Maandamano..

Ha ha habari ndo hiyo, haha...habari ndo hiyo

Habari yako imekaa kiushabiki
 
Kuna mtu/ watu nyuma ya hili; mbona linageuzwa geuzwa namna hii kwa faida ya nani?
 
Kwa nini jalada la suala hili lisifungwe? Watu tumeshakuwa na maamuzi mbadala.
 
Ukisikia siasa ni mchezo mchafu usibishe,,,,
cheki mkulu wa nchi alivyo wapiga waislamu chenga za kironaldinho
 
... Muft wa Tanzania ameshalitolea ufafanuzi suala hilo so No Maandamano..

Ha ha habari ndo hiyo, haha...habari ndo hiyo

Mufti na polisi wote ni wa serikali na serikali yenyewe ni ya sisiemu!
 
Mimi naona hakuna haja ya kuandamana; kama wamejiandisha -- wasubiri October wasiipigie kura ccm. Hakuna haja ya kuwashika sikio kama kweri wananuia wanachosema
 
So far katika nchi hii hakuna maandamano ambayo yamekuwa na productivity!...Wastage of time at the peak tune!
 
Kila la kheri.Nawatakia amani ya Yesu iwe nao

bora charity imesema ivyo. Lakini chari, kwa upande mwengine, kwanini umetoa ile avatar yako ya mwanzo? nilikuwa naipenda sana ile avatar nikiiangalia,..hahaha.
 
bora charity umesema ivyo. Tatizo awa jamaa wanaenda kidinidini mno, hata aibu hawana, hivi kwanini waandamane kwaajili ya dini yao tu na si kwaajili ya kuikomboa nchi ya Tanzania toka mikononi mwa ccm? hii ni aibu halafu wanakera kupindukia, hawana hata aibu kwenye hii nchi tunayotakiwa kuwa na umoja mtu anakuja leo ati anaandamana kwasababu ya matakwa ya dini yake...wakimaliza hao wakristo tukaandamana kwa matakwa yetu, wakija hao wanakuja waganga wa kienyeji kuandamana, wakimaliza hao wanakuja wahindu, badaye wabudha, hili taifa litagawanyika vifunguvifungu kidini hadi likome...huu ni upuuzi na inakera kusikiliza.

Lakini chari, kwa upande mwengine, kwanini umetoa ile avatar yako ya mwanzo? nilikuwa naipenda sana ile avatar nikiiangalia,..hahaha.
 
Kazi njema Kamanda Kova, mtu kama hataki kuichagua CCM basi asiichague mwenyewe na sio kuwahadaa na wengine! Walishaandika Nyaraka kuelekea uchaguzi Mkuu, 2010 si zinatosha jamani? Na wale Waislamu ambao wamevaa mashati ya kijani na wameonesha nia wafanyeje, wahamie CCJ ambayo nayo haieleweki mpaka sasa? Oh, please!
 
Ukisikia siasa ni mchezo mchafu usibishe,,,,
cheki mkulu wa nchi alivyo wapiga waislamu chenga za kironaldinho

Walichoahidiwa wamekipata (ie waanzishe Mahakama wenyewe na kuiendesha wenyewe), labda kama wana jingine lililojificha ndani ya mioyo yao!
 
Ninavyoona mimi kuandamana kwa amani kahuna tatizo ni haki ya wananchi.
Serikali inaogopa nini? au inahofu wananchi watahamasika na kutoichagua CCM?
Swala sio udini, ni demokrasia.
 
So far katika nchi hii hakuna maandamano ambayo yamekuwa na productivity!...Wastage of time at the peak tune!

Nyakati za kubomoa mabucha ya nguruwe zilikuwa za mzee Ruksa, wajiulize yameisha?
 
Swala sio udini, ni demokrasia.

You are totally wrong! Hakuna uhuru usiokuwa na mipaka ndugu, hata kama utaubandika jina la demokrasia, uhuru wako unapoishia ndipo na wa mwenzako unapoanzia! Hawa watu wameambiwa waanzishe Mahakama yao wenyewe, bado wamekaa vijiweni kunywa kahawa wakisubiri Serikali iwaanzishie IBADA yao ya KIISLAMU! Upstairs kwa hawa wandugu kunafanya kazi kweli?
 
Nasema maandamano yangefanyika yangekuwa yanaidhalilisha sana dini ya kiislam,viongozi wake,waumini wake,kitabu chake[Quran] na Mtume wake Muhamad SAW kwasababu zifuatazo.

[1] Waislamu wanataka kuandamana kwasababu serekali ya CCM imeshindwa kuanzisha mahakama ya Kadhi.Ukweli ni kwamba Serekali ya CCM imewaruhusu waislam waanzishe na kuiendesha mahakama ya kadhi wenyewe kwasababu ni sehemu ya ibada yao [waislamu].Ni ajabu kubwa kuona wanazuoni tena waliobobea kuendelea kudai mahakama ya kadhi ilihali serekali imesharidhia kuanzishwa kwake.

[2] Waislamu wa Tanzania wanajua wazi CCM imekuwa ikiwadanganya wananchi kwa muda mrefu katika mambo mabali mbali,inashangaza sana kusikia viongozi wa waislam hawakuona haja ya kuandamana wakati mabilioni ya EPA,Meremeta,ununuzi wa radar,ndege ya rais,mikataba ya madini na ufujaji wa fedha kwenye maidara ya serekali ukifanyika.Akili yangu inakataa kuamini kwamba viongozi wa waislamu leo hii wanagundua CCM ni waongo kwasababu tu wameshindwa kuvunja katiba ya JMT kwa kuingiza mahakama ya kadhi.Viongozi wa aiana hii kamwe hawataweza kuwakomboa waislam kwasababu wanashindwa kuwaeleza ukweli waumini wao kwamba mahakama ya kadhi inaweza kuanzishwa na waislamu wenyewe bila kutegemea fadhila za serekali.
 
hahahaha, mzee chadema wakipewa nchi. Nadhani sijui dini nyengine wakae wapi?

Ukimpiga chura teke unamwongezea mwendo, endelea kuifagilia CHADEMA, wenye chama hicho huwa wanasema "Mpaka kieleweke!"
 
Back
Top Bottom