Essentially hapa kuna violation ya freedom of expression. Hili haliwezi kukataliwa.Ukweli kwamba Mufti kashatolea maelezo jambo fulani haumaanishi kwamba waislamu wote ni lazima wakubaliane na mufti, na waislamu wana haki ya kuandamana ili kuonyesha msimamo wao as long as wanafuata sheria.
Lakini, pamoja na kuelewa kwamba polisi wame violate freedom of expression, kuna watu wengine watasema "well, that is true, lakini kuna the bigger picture ya security hapa, na hatujui haya maandamano yanaweza kuzaa nini, it is too risky to allow". Basically unatumia tyranny ili kuhakikisha unamaintain security, at least that is the most eloquent excuse that can be given.
Lakini ukisema hivyo, utakuwa umesha prejudge nia ya waislamu kwamba iko sinister, na utakuwa umeshakubali kwamba huwezi ku deal na waislamu walio sinister. Both of these two admissions are not good.
Benjamin Franklin alisema "Those who sacrifice their liberty for security deserve neither". Kwa kuwakatalia maandamano waislam kwa sababu za usalama na siasa (under the thinly disguised reason given) kamanda Kova na jeshi la polisi hawatupi usalama wala uhuru.
Mimi nasema waislam waruhusiwe kuandamana, na waambiwe wakitaka hata kwenda mahakama zote Tanzania waende. Wakileta fujo kwenye maandamano wadhibitiwe kwa mujibu wa sheria.
Huwezi kuwa na nchi inayojitia kuwa ya kidemokrasia, halafu hapo hapo watu wanataka kuandamana kuonyesha msimamo wao (hata kama msimamo si mzuri, suala la kuandamana kuonyesha msimamo haliwezi kukataliwa kwa sababu msimamo si mzuri, au swali la msingi lishatolewa jibu na mufti, vipi kama hawakubaliani ma mufti kama inavyoonekana hapa? Tunawalazimisha wakubaliane naye)
Jeshi la polisi kwa mara nyingine linadhihirisha kwamba Tanzania si nchi ya kidemokrasia, basically ni police state.