Waislam wamtaka Magufuli azingatie utawala wa Sheria

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,073
114,571
Kiongozi Mwandamizi wa dhehebu la Kiislamu la Shia Ithnashery nchini Tanzania Imamu Swadiq Sheikh Hemed Jalala ameitaka Serikali ya awamu ya tano kuzingatia utawala bora na kuweka usawa baina ya wananchi bila ya kuangalia tofauti zao ili kwa pamoja waweze kujiletea maendeleo.

Sheikh Jalala ameitoa kauli hiyo wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mrithi wa Mtume Muhamad Imam Ali ambae alikufa miaka elfu moja na 30 iliyopita lakini anakumbukwa kwa utawala wake wa kuzingatia usawa kwa binaadamu.

Aidha Sheik Jalala amesema kuwa Utawala bora hauwezi kupatikana kama hakutakuwa na utulivu na amani katika nchi hivyo serikali ya awamu ya tano isimamie kikamilifu suala la amani na utulivu ili wananchi waweze kufanya kazi kwa bidii.
 
Naona mwanakijiji amegeuka kuwa main ajenda!! Mwacheni jamani, ni miaka mingi mno imepita Toka ameanza kujiita MZEE!!
 
Walivyo wabaguzi watakuja kusema hao si waislam, bali ni wasaliti wa uislam.
 
Kiongozi Mwandamizi wa
dhehebu la Kiislamu la Shia Ithnashery nchini Tanzania Imamu Swadiq Sheikh Hemed Jalala ameitaka Serikali ya
awamu ya tano kuzingatia
utawala bora na kuweka usawa
baina ya wananchi bila ya
kuangalia tofauti zao ili kwa pamoja waweze kujiletea
maendeleo.
Sheikh Jalala ameitoa kauli hiyo
wakati wa maadhimisho ya
kumbukumbu ya kuzaliwa kwa
Mrithi wa Mtume Muhamad
Imam Ali ambae alikufa miaka
elfu moja na 30 iliyopita lakini
anakumbukwa kwa utawala
wake wa kuzingatia usawa kwa
binaadamu.
Aidha Sheik Jalala amesema
kuwa Utawala bora hauwezi
kupatikana kama hakutakuwa
na utulivu na amani katika nchi
hivyo serikali ya awamu ya tano
isimamie kikamilifu suala la
amani na utulivu ili wananchi
waweze kufanya kazi kwa bidii.
Umeanza lini kufuatilia matamko ya waislamu?
 
Back
Top Bottom