WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 956
Ngoja nikusanye wapagani wenzangu tuandae ya kwetu........lazime maeneo yote ya matambiko kama ule mbuyu wa pale Kenyatta Drive yaheshimiwe na yalindwe kwa gharama za serikali
1.Mhh..haya wee! Ila mkiingiza mambo yenu ya mizimu au sijui miungu wenu mjue mnapoteza muda wenu bure.Tanzania ni secular State haina dini hivyo mjishughulishe zaidi na mambo ya ustawi wenu kama wanajamii ya kitanzania kwa ujumla wake na siyo waabudu miti.
2.Ibada na imani ni kitu cha kibinafsi sana - kitu chako wewe na imani yako, wewe na Muumba wako au nguvu ya juu unayoiamii na siyo lazima kutuwekea kwenye Katiba ambayo ni mkataba wa kijamii baina ya raia na wale waliopewa ridhaa kutawala.
3. Naamini kila mtanzania mwenye kutakia nchi mapenzi mema hatataka kamwe kuona mambo binafsi kama imani na ibada vikiwemo kwenye Sheria mama. Hebu tujiulize hiyo Katiba itakuwa na sura gani kama kila imani itaingizwa kwenye katiba - si ni vurugu na kuchanganyikiwa huko?