Waislam waandaa rasimu ya Katiba mpya

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,669
155,084
KILIO cha makundi mbalimbali ya kijamii na kisiasa katika kudai katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kimechukua sura mpya baada ya Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislaam (T), kuanza mchakato wa kuandaa rasimu ya katiba hiyo ambayo itawasilishwa serikalini ndani ya siku 30.
Hatua hiyo imekuja baada ya taasisi hiyo, kuamini kuwa suala la katiba mpya halina tena mjadala kutokana na umuhimu wake kwa taifa.

Hatua hiyo inakuja wakati taasisi za kijamii, kisiasa, kidini na hata watu binafsi, zikiibuka na kudai katiba mpya.
Siku kadhaa zilizopita Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alisema atamshauri Rais Jakaya Kikwete, kuangalia namna ya kuanzisha mjadala wa kitaifa, kama mchakato wa kuandika katiba mpya.

Lakinin kauli hiyo ya Pinda ilitofautiana na ya Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani na Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, ambao kwa nyakati tofauti, walisema kwa sasa, hawaoni haja ya kuandikwa kwa katiba mpya.

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislaam Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, alisema kwa kuona umuhimu wa suala hilo katika mustakbali wa taifa, taasisi imeanza mchakato wa kuandaa rasimu ambayo wataiwasilisha serikalini.
“Kwa muktadha huu, tumeanza kuandaa mapendekezo muhimu ya Waislaam na Tanzania ya sasa na siyo ya jana katika katiba mpya, pia tutatahadharisha baadhi ya mambo katika katiba hiyo,” alisema Sheikh Ponda.

“Lengo ni kuhakikisha kwamba tunapata katiba inayokwenda na wakati, itakayojenga na kulinda haki, misingi ya usawa,amani na kuleta ustawi mzuri wa taifa.” alisisitiza.
Alisema rasimu hiyo itawasilishwa mara baada ya kukamilika na kwamba itajumuisha mawazo ya Waislaam wa mikoa yote nchini.

Kwa mujibu wa Sheikh Ponda, mawazo hayo yatakusanywa kwa njia ya semina na makongamano maalumu kuhusu elimu juu ya umuhimu wa katiba mpya.

“Pia tunaomba kila Mtanzania mwenye mapendekezo mazuri ya kuivusha nchi yetu na kudumisha amani kwa ajili ya katiba mpya, kuyafikisha katika ofisi za taasisi yetu au kwa kutumia anwani zake,” alisema Sheikh Ponda.

Alisema Waislaam wanaamini kuwa suala la katiba mpya ni la muhimu katika kuleta demokrasia na uhuru wa kweli.
"Suala hili si la mtu au taasisi moja kujifungia chumbani na kuandaa bali ni suala linalohitaji njia shirikishi kwa makundi yote ya kijamii," alisema.

SOURCE:- MWANANCHI
 
Vipi tena jamani,hawa jamaa wanaandaa rasimu ya katiba ya kiislamu au katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania?Katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania itaandaliwa na watanzania wote bila kujali dini zao!!nafikiri wanakifanya sasa ni kupoteza muda wao tu,kwa si wakristu au waislamu wanaoweza kuandaa rasimu ya katiba ya nchi hii.Na waislamu wasitalajie kuwa mahakama ya kadhi itakuwa kwenye katiba mpya,kwani hii si nchi ya kiislamu,bali ni nchi isiyofungamana na dini yoyote(Secular Government).
 
Makubwa......lakini nao ni sehemu ya wananchi na wanahaki ya kupza sauti zao kwenye uanzishwaji wa katiba mpya ila mmmmmmhhhhh!
 
Waelewe kwamba serikali haina Dini hivyo kuingiza suala lolote la dini yoyote kwenye katiba kutaathiri maana ya neno hilo. Ni mtazamo tu.
 
Makubwa......lakini nao ni sehemu ya wananchi na wanahaki ya kupza sauti zao kwenye uanzishwaji wa katiba mpya ila mmmmmmhhhhh!

Hakuna anayelikataa hilo,wanapaswa waandaa rasimu ya katiba kama wananchi na is kama waislamu,hapo ndiyo tofauti inapokuja!!
 
Ngoja nikusanye wapagani wenzangu tuandae ya kwetu........lazime maeneo yote ya matambiko kama ule mbuyu wa pale Kenyatta Drive yaheshimiwe na yalindwe kwa gharama za serikali
 
Waislam wana matumain ya SHARIA na KADHI kuingizwa ktk Katiba. Ni bora kubaki na iliyopo kuliko kuleta mpya yenye UDINI.
 
Kama Katiba mpya itaandaliwa na BAKWATA basi afadhali tubaki na Katiba ya sasa, much better!
 
Vipi tena jamani,hawa jamaa wanaandaa rasimu ya katiba ya kiislamu au katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania?Katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania itaandaliwa na watanzania wote bila kujali dini zao!!nafikiri wanakifanya sasa ni kupoteza muda wao tu,kwa si wakristu au waislamu wanaoweza kuandaa rasimu ya katiba ya nchi hii.Na waislamu wasitalajie kuwa mahakama ya kadhi itakuwa kwenye katiba mpya,kwani hii si nchi ya kiislamu,bali ni nchi isiyofungamana na dini yoyote(Secular Government).

soma paragraph ya mwisho kabisa utaelewa acha rukaruka kama mbayuwayu. ulisha fikiria vitu vingiine kabisa. . toka huko tujenge nchi mkuu
 
tusiwahukumu nao wana haki ya kutoa mapendekezo lakini si lazima yachukuliwe na kuingizwa kwenye katiba kunauwezekano yakachujwa na mazuri machache yakatumia wajumbe tusianze kubagua dini za wenzetu kwani hata wengine waliwahi kuandika waraka
 
KILIO cha makundi mbalimbali ya kijamii na kisiasa katika kudai katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kimechukua sura mpya baada ya Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislaam (T), kuanza mchakato wa kuandaa rasimu ya katiba hiyo ambayo itawasilishwa serikalini ndani ya siku 30.
Hatua hiyo imekuja baada ya taasisi hiyo, kuamini kuwa suala la katiba mpya halina tena mjadala kutokana na umuhimu wake kwa taifa.

Hatua hiyo inakuja wakati taasisi za kijamii, kisiasa, kidini na hata watu binafsi, zikiibuka na kudai katiba mpya.
Siku kadhaa zilizopita Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alisema atamshauri Rais Jakaya Kikwete, kuangalia namna ya kuanzisha mjadala wa kitaifa, kama mchakato wa kuandika katiba mpya.

Lakinin kauli hiyo ya Pinda ilitofautiana na ya Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani na Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, ambao kwa nyakati tofauti, walisema kwa sasa, hawaoni haja ya kuandikwa kwa katiba mpya.

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislaam Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, alisema kwa kuona umuhimu wa suala hilo katika mustakbali wa taifa, taasisi imeanza mchakato wa kuandaa rasimu ambayo wataiwasilisha serikalini.
"Kwa muktadha huu, tumeanza kuandaa mapendekezo muhimu ya Waislaam na Tanzania ya sasa na siyo ya jana katika katiba mpya, pia tutatahadharisha baadhi ya mambo katika katiba hiyo," alisema Sheikh Ponda.

"Lengo ni kuhakikisha kwamba tunapata katiba inayokwenda na wakati, itakayojenga na kulinda haki, misingi ya usawa,amani na kuleta ustawi mzuri wa taifa." alisisitiza.
Alisema rasimu hiyo itawasilishwa mara baada ya kukamilika na kwamba itajumuisha mawazo ya Waislaam wa mikoa yote nchini.

Kwa mujibu wa Sheikh Ponda, mawazo hayo yatakusanywa kwa njia ya semina na makongamano maalumu kuhusu elimu juu ya umuhimu wa katiba mpya.

"Pia tunaomba kila Mtanzania mwenye mapendekezo mazuri ya kuivusha nchi yetu na kudumisha amani kwa ajili ya katiba mpya, kuyafikisha katika ofisi za taasisi yetu au kwa kutumia anwani zake," alisema Sheikh Ponda.

Alisema Waislaam wanaamini kuwa suala la katiba mpya ni la muhimu katika kuleta demokrasia na uhuru wa kweli.
"Suala hili si la mtu au taasisi moja kujifungia chumbani na kuandaa bali ni suala linalohitaji njia shirikishi kwa makundi yote ya kijamii," alisema.

SOURCE:- MWANANCHI

Katiba ijayo iwe inataja:-
Idadi ya wanawake wa kuoa,
Kodi za Nguruwe zilipe mahakama ya kadhi,
Miaka ya kuolewa vibinti iwe miaka sita na kuendelea,
Kukata mikono ya wezi halali,
Kuoa na kuacha kama kawa.
 
I can smell shekhes are dreaming for the United Islamic Republic of Tanzania.
 
Yale yale ya yule mtume asiye juwa kusoma. Hivi hawa wafuasi wa allah wanataka nini? Au mpaka viboko vya mwembe chai vianze tena, ndio kitaeleweka kitu?
 
Back
Top Bottom