Je hiyo si ni demokrasia au?
Au Waislamu(kwa umoja wao, au kwa wingi wao) hawana haki ya kutoa maoni yao katika nchi hii, hata kama hamyapendi?
Ni kifungu gani cha Kanuni za Sheria au Katiba walichovunja kwa kutoa maoni yao?
Mimi nawashangaa baadhi ya WanaJF kujifanya wameenda shule, kumbe wameishia kupata vyeti tu lakini kuelimika hawajaelimika, utamzuiaje mtanzania kutoa maoni yake katika nchi hii ilhali havunji sheria za nchi?, huu ni ugreat thinker wa namna gani!!
Waislamu siyo makondoo, ni watu wenye msimamo usioyumba, wakitaka kitu wanaweza kukitafuta mpaka wakakipata. msidhani kwa dharau zenu, mtaweza kuwarudisha nyuma kudai au kusimamia kile wanachokiamini bila kuvunja sheria za nchi.
Falsafa mojawapo ya uislamu ni kutokumuonea mtu, na kutokubali kuonewa kamwe.
Msidhani kwa vijembe vyenu, dharau zenu, matusi yenu, mtawanyamazisha Waislamu wasidai haki zao, au kutolea matamko yale ambayo wanayathamini kwa dhati hata kama wewe unayadharau.
Waislamu hawatanyamaza katika nchi hii mpaka serikali itakapojibu hoja na madai yao kwa ushahidi ulio maridhawa kabisa kwamba hakuna ubaguzi wowote ule FORMAL au INFORMAL juu ya waislamu.
Ni Haki kwa Mwananchi yoyote kutaka majibu kutoka kwa viongozi wao, na ni heshima kwa viongozi kutoa majibu yenye kujitosheleza. hii haki ni watu, either awe mmoja mmoja, au katika wingi wao.
Na kwa wale Wanasiasa wanaojifanya kufumba macho juu ya kuwepo kwa udini Tanzania, ni lazima mtafute dawa ya hili tatizo, hili tatizo lipo, na hisia kwa wananchi kuhusu huu udini upo, mfano mzuri ni matamko haya ya waislamu, mkijifanya kukaa kwenye comfort zone na kufumba macho msione hili tatizo, Kamwe hamtakuja kuukwaa uongozi wa juu wa Taifa hili, kwa sababu mko nje ya reality, na kundi moja la kijamii katika nchi hii litawaona kama mnaojaribu kulinda status quo ili kunufaisha kundi linalowaunga mkono.
HAKUNA MWENYE HAKI YA KUSILENCE WAISLAMU, NI HAKI YAO KUTOA MAONI YAO, MATAMKO YAO, HOJA ZAO, HATA KAMA HAMZIPENDI.