Waingereza watacheka baadaye watalia na Boris

Rubawa

JF-Expert Member
Dec 25, 2015
1,891
2,000
BARAZANI

Na Ahmed Rajab

HAPA ndipo demokrasia ya Uingereza ilipofika: kwamba safari hii waziri mkuu wa taifa zima la wakaazi wasiopungua milioni 66 anachaguliwa na watu wasiozidi 160,000. Hapa, kwa hakika, ndipo Theresa May, waziri mkuu anayestaafu, pamoja na wenzake walipoifikisha demokrasia ya nchi yao.

Hao watu 160,000 wataomchagua waziri mkuu mpya wana taswira isiyolingana na taswira ya Uingereza ya leo: wengi wao ni vizee na ni wazungu.

Taswira ya Uingereza ya leo ni tofauti kabisa na hiyo. Uingereza ya leo ina Waingereza wa mchanganyiko wa rangi na tamaduni; na wengi wao ni vijana.

Hao wataomchagua waziri mkuu mpya ni wanachama wa chama kinachotawala cha Conservative. Kazi yao, kwa hakika, ni kumchagua mrithi wa Theresa May wa kukiongoza chama chao.

Wao na wabunge wao wamekabiliwa na kibarua kigumu kwani ingawa wamo kwenye mchakato wa kumchagua kiongozi wanayemuona kuwa ni bora kwa chama chao lakini wanajua kwamba kiongozi huyo pia ndiye atayekuwa waziri mkuu.

Katika duru ya mwanzo Alhamisi iliyopita, wagombea walitakiwa waungwe mkono na wabunge wasiopungua 17 ili waweze kusonga mbele na kuingia katika duru ya pili ya mchuano. Kati ya wagombea kumi waliojitokeza kuwania nafasi hiyo watatu walishindwa kuwapata wabunge 17 wawaunge mkono. Walibidi watolewe kwenye mmenyano huo.

Miongoni mwao walikuwa mabibi wawili. Kwa hivyo, kwa kuondolewa mabibi hao tuna hakika ya jambo moja. Nalo ni kwamba waziri mkuu mpya hatokuwa mwanamke.

Kwa muda mrefu kabla ya duru ya mwanzo ya kura za wabunge wa chama chao, waziri wa zamani wa mambo ya nje Boris Johnson amekuwa akijificha. Boris ni miongoni mwa wagombea wa nafasi ya May lakini amekuwa akiogopa kuhojiwa na kusailiwa ipasavyo na waandishi habari.

Hata Jumapili iliyopita pale steshini moja ya televisheni ya Uingereza ilipokuwa na mdahalo wa wagombea Johnson aliyayuka. Hakuonekana kwenye studio ya mdahalo huo. Alifanya hivyo kwa kushauriwa na wapambe wake waliozipanga mbinu za kuhakikisha kwamba ataibuka mshindi.

Wenye kumpigia kampeni Johnson wanayaogopa maswali. Hofu yao kubwa ni kwamba akiulizwa maswali mengi anaweza akajichanganya na kujiumiza mwenyewe. Hiyo ndiyo sababu iliyowafanya waamue kuwa bora Johnson awakimbie waandishi habari. Waliona afadhali ajifiche, atawe.

Hadi sasa, ninavyoandika haya, wamebakia wagombea sita waliopigiwa kura jana baada ya Matt Hancock, waziri wa afya, kujitoa katika shindano hilo. Hancock ni kijana, mdogo kwa umri kushinda wagombea wote wenye kutaka kumrithi May. Waliokuwa wakimuunga mkono waliamini kwamba ujana wake ungemsaidia kuwavutia wenye kutaka vijana washike hatamu za uongozi.

Lakini baada ya kuzipiga hesabu zake Hancock aling’amua kwamba hatopata idadi inayohitajika ya wabunge wa kumuunga mkono katika duru ya pili ya upigaji kura. Katika duru hiyo kila mgombea alihitaji aungwe mkono na wabunge wenzake wasiopungua 33.

Ndo Hancock akafanya uungwana wa kujitoa katika mchuano huo na, akaamua badala yake, amuunge mkono Boris Johnson. Aliona kheri ajiangushe mwenyewe kuliko kuadhirika kwa kuangushwa baada ya kura kupigwa katika duru ya pili.

Bahati mbaya duru hiyo ilikuwa jana wakati Raia Mwema likiwa mitamboni linachapishwa kwa hivyo hatukuweza kujua miongoni mwa wagombea sita waliosalia nani aliyepata kura nyingi kushinda wenzake, nani aliyemfuatia na nani na nani walioangushwa.

Akitaka asitake, waziri mkuu mpya atakabiliwa na changamoto mbili kubwa. Ya kwanza ni ya kuitoa Uingereza kutoka Muungano wa Ulaya (EU) na ya pili jinsi ya kupambana na chama kipya cha Brexit kinachoongozwa na Mbunge wa Bunge la Ulaya Nigel Farage ambaye ndiye mshika bendera mkuu wa wenye kutaka Uingereza ijitoe kutoka EU.

Kwa macho ya wengi aliyekuwa akiongoza hadi hapo jana miongoni mwa hao wagombea sita alikuwa Boris Johnson. Mwanasiasa huyo ana uzoefu wa muda mrefu wa kuendesha mambo na kuwaongoza watu. Aliwahi kuwa mhariri wa gazeti, meya wa London na waziri wa mambo ya nje.

Alionekana kuwa na mapungufu katika utekelezaji wa majukumu yake katika nyadhifa zote hizo tatu alizozishika. Alipokuwa mhariri wa gazeti la kila wiki la Spectator aliwaliza baadhi ya waandishi wake kwa utendajikazi wake.

Alipokuwa meya wa London alilitia hasara kubwa jiji la London kwa miradi isiyokamilika. Ilibainika pia kwamba akiwa meya aliwahi kufanya mambo bila ya kufuata kanuni.

Na alipokuwa waziri wa mambo ya nje mara kwa mara aliteleza kwa baadhi ya matamshi yake. Alipoteuliwa waziri watu wengi wenye kumfahamu walishangaa. Hawakuamini kwamba waziri mkuu May angemteua Johnson awe waziri wake wa mambo ya nje kwa sababu akijulikana kwa ila zake za kusema uongo, kubadili misimamo na kujisemea tu mambo bila ya kuzingatia athari za kauli zake.

Wapinzani wa Johnson wanatamani ajikwae. Na wanaomba kwamba akijikwaa, ajikwae ulimi na si kidole. Wanaamini kwamba yakimfika hayo huenda yakammaliza kisiasa.

Tokeo kama hilo ndilo linalowatia hofu mashabiki zake wakubwa na kuwafanya wamshauri ajitahidi afanye juu chini asihojiwe na waandishi habari.

Wachambuzi wengi wamekuwa wakitabiri kwamba Johnson ndiye atayefanikiwa kumrithi Theresa May. Lakini mara nyingi katika uchaguzi kama huu yule asiyetarajiwa kabisa ndiye huibuka mshindi.

Hata hivyo, kwa sasa Johnson ndiye mwenye idadi kubwa ya wabunge wenye kumuunga mkono. Miongoni mwao ni wabunge wenye asili ya Kiafrika wakiwa pamoja na waziri wa Brexit James Cleverly (mama yake ni mhamiaji kutoka Sierra Leone), waziri mdogo wa Brexit Kwasi Kwarteng (wazazi wametoka Ghana) na waziri wa zamani wa maendeleo ya kimataifa Priti Patel (wazazi Wahindi waliohamia Uingereza kutoka Uganda).

Chama cha Conservative kimebadilika sana katika miaka ya hivi karibuni. Zamani ilikuwa nadra kuwaona Waingereza weusi wakijiunga na chama hicho seuze kuwa na usemi pamoja na nyadhifa kubwa ndani ya chama chenyewe na katika serikali zake.

Siku hizi imekuwa ni jambo la kawaida kuwaona wasio wazungu, tena vijana, wakiwa katika safu za mbele za uongozi wa chama hicho.

Licha ya kujitahidi kujibadili kwa kujipaka rangi ya uvumilivu bado chama hicho kimejaa wabaguzi wenye kuamini kwamba Uingereza imevamiwa na wageni. Wanachama wake wengi wamekiacha mkono chama hicho na wamejiunga au wamekuwa wakivipigia kura vyama vya UKIP na Brexit, ambavyo wengi wanavihisi kuwa ni vya kibaguzi na vya mrengo wa kulia zaidi.

Boris Johnson anamhusudu Winston Churchill, aliyekuwa waziri mkuu mara mbili (1940-1945 na 1951-55). Churchill alikuwa mbaguzi na mara kwa mara matamshi yake ya kibaguzi yakiwashtua na kuwakera vijana wa chama chake cha Conservative waliokuwa na fikra za kimaendeleo.

Si ajabu kwamba Johnson anamhusudu Churchill kwani ana dharau kama alizokuwa nazo Churchill kuwahusu Waafrika na Waislamu.

Lililo la ajabu ni kwa Johnson kuwa na madharau juu ya Waislamu ilhali mke wa nduguye mmoja ni Mwislamu aliyetoka Afghanistan.

Pia, ingawa kuukeni kwake Boris Johnson ametokana na vizazi vya Mfalme George wa Pili wa Uingereza, hata hivyo, kama tulivyoeleza wiki chache zilizopita, babu wa baba yake, alikuwa Mwislamu wa Kituruki. Jina lake lilikuwa Ali Kemal. Babu yake Boris akiitwa Osman.

Kemal alikuwa mwandishi habari, mshairi na kwa miezi mitatu aliwahi kuwa waziri wa mambo ya ndani katika serikali ya waziri mkuu Ferid Pasha wakati wa utawala wa Uthmaniya (Ottoman). Mke wa mwanzo wa Kemal, yaani bibi wa baba yake Boris Johnson, alikuwa Mwingereza wa tabaka la mabwanyenye.

Watoto na wajukuu wa Kemal walibadili jina lao. Badala ya kujiita Kemal wakajiita Johnson. Inavyoonesha ni kwamba Boris Johnson amemrithi mengi Ali Kemal. Amemrithi kwa kuandika utamu, kwa kuwa mwanasiasa, kwa kuwa mbunge (ingawa wa nchi tofauti) na kwa uhodari wa kuhutubu.

Picha moja niliyoiona ya Ali Kemal inamuonesha akivaa tarbushi, akiwa na sharubu kubwa, alizozisokota nchani. Siku moja, Novemba 4, 1922 aliingia kwenye duka la kinyozi katika hoteli moja jijini Istanbul ili akate nywele na kuzitengeza sharubu zake. Mara akavamiwa na akatekwa nyara.

Waliomteka waliazimia kumpeleka Ankara alikoshtakiwa kwa kesi ya uhaini. Walipofika mji wa Izmit wakiwa njiani kuelekea Ankara walishambuliwa na genge la kamanda mmoja wa kijeshi aliyekuwa akimuunga mkono Kemal Ataturk, baba wa Uturuki ya leo.

Ali Kemal alipigwa mawe, marungu na visu mpaka akafa. Kisha maiti akatundikwa mtini.

Chama cha Conservative kimepiga hatua kubwa kwa kuwapa wanachama wake usemi wa mwisho wa nani awe kiongozi wao. Lakini kwa taifa, hatua hiyo ni pigo kwa demokrasia ikiwa watu wachache ndio wanaoachiwa kumchagua waziri mkuu atayewaongoza walio wengi.

Akichaguliwa Johnson Waingereza watacheka kwa sababu atawachekesha. Boris Johnson ana kipaji kikubwa cha kuchekesha watu. Lakini nina hakika hatimaye uongozi wake utageuka na kuwa mkasa wa “majuto mjukuu”.

Baruapepe:aamahmedrajab@icloud.com; Twitter: @ahmedrajab
 
BOB OS

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
3,321
2,000
waingereza sio kama lumumba kila kitu wanasema ndioooooooooooo,,,
wao wanaangalia masilahi ya nchi,siyo ya mtu...
kukuondoa kuwa waziri mkuu ni kitu cha sekunde tu,,hayo majuto watapata wapi.........
Na pia naona unajaribu kuingiza udini hapo,waingereza siyo wajinga ..............
 
Rubawa

JF-Expert Member
Dec 25, 2015
1,891
2,000
Yaan wewe Ahmed rajabu mwisilam unayewali msikiti wa kwa mtogole unataka kujifanya unayajua sana maswala ya kwa malikia kuwashinda hata raia wa malikia wenyewe

Acha kuingilia katiba za watu fatilia kwanza katiba ya nchi yako hapo rumumba na usikute wewe ni ccm. Ccm ndo huwa mnamawazo mgando sana namna hii

Unashangaa watu160000 kuchagua waziri mkuu wakati tanzania rais anachaguliwa na mtu mmoja tu salum jecha
Nimekubari Juma Lokole naona utaki kupitwa karibu sna Barazani...
 
Domsel

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
683
1,000

Uingereza imevamiwa kweli, ustaarabu na uwezo wa utaalamu wa asili wa waingereza inaenda kumalizwa na waarabu na wafrika waliojaa uigaji wa dini hata sio zao .
Waarabu wanaenda kuwamaliza kabisa kwa kuwalazimisha kuiga dini yao. Watawaua kwa kuwachinja na vitisho. Ni janha la dunia.
Waache wazee watawale siyo hao vijana feki.
 
Mkokaa

JF-Expert Member
Jan 3, 2019
4,814

Unaakuli kuliko waingereza??? 🤣🤣🤣🤣
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom