Wahudumu wa vituo vya mafuta wengi wao hawajali wateja

NAKWEDE

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
27,966
35,152
Habari wandugu,

Ninakerwa sana na wahudumu wa vituo vya mafuta,yaani ukienda kununua mafuta ya taa ukifika wala hawakujali, utasikia wanaambizana "nenda kamhudumie, mara nenda wewe"

Wahudumu wa vituo vya mafuta wanathamini na kupenda wateja wenye magari regardless mteja huyo ni male au female. Wakimuona utaona wanamuonyesha aweke vipi gari yake, wakati wakiwa ameshikilia kabisa ule mpira ili akifungua tu tank amhudumie fasta yaani wanaonyesha kabisa kumjali mteja.

Ombi langu kwenu, heshimuni wateja wote awe ana jaza mafuta kwenye gari na hata hao wenye vidumu vya kununua mafuta ya taa wote wanahitaji hiyo
CUSTOMER CARE
 
Elimu ndogo + mshahara 140,000 + stress = customer dissapointment !!

Wengi wao ni standard seven failure, pia station
managers wao hawawafanyiagi continues training on how to handle customers.
 
Umnukishe harufu bure ya mafuta ya taa bila kupata cha juu,ukiwa na kidumu cha Lita tano atakuchakachuaje?,wenye magari hata wakitaka Lita ishirini lazima na pump attendant ataondoka na Lita moja.
 
hahahahahahahahahahahahahahahaha
 
ipo shelly moja kilwa road b4 round abt pale kota za polisi aisee unaingia shelly mdada kakaa chumba cha mlinzi anaongea na simu unapaki gari umngojee...tatzo wengi wao sura kama yangu kiume
sijui malingo ya nn
 
Habari wandugu,

Ninakerwa sana na wahudumu wa vituo vya mafuta,yaani ukienda kununua mafuta ya taa ukifika wala hawakujali, utasikia wanaambizana "nenda kamhudumie, mara nenda wewe"

Wahudumu wa vituo vya mafuta wanathamini na kupenda wateja wenye magari regardless mteja huyo ni male au female. Wakimuona utaona wanamuonyesha aweke vipi gari yake, wakati wakiwa ameshikilia kabisa ule mpira ili akifungua tu tank amhudumie fasta yaani wanaonyesha kabisa kumjali mteja.

Ombi langu kwenu, heshimuni wateja wote awe ana jaza mafuta kwenye gari na hata hao wenye vidumu vya kununua mafuta ya taa wote wanahitaji hiyo
CUSTOMER CARE
Wanakimbilia magari kwa sababu wana namna ya kuiba wakati wanabonyeza pump handle wakitia petrol/diezel, lkn kwenye mafuta ya taa wataibaje wakati kidumu kinaonyesha wazi?
 
Sasa hivi wamekomeshwa kidogo na hizo EFD
 
Back
Top Bottom