Wahudumu wa TIGO wana roho mbaya!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wahudumu wa TIGO wana roho mbaya!!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by TANMO, Nov 10, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #1
  Nov 10, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,907
  Likes Received: 203
  Trophy Points: 160
  Nilitaka kujisajili kwenye Huduma ya TIGO PESA cha kushangaza nikaambiwa eti nilishajisajili hivyo nikalazimika kwenda kwenye Ofisi za Tigo pale Mlimani city kutaka kufahamu ukweli wa hili suala pamoja na kuomba kupatiwa namba ya siri.

  Yapo mazuri niliyokutana nayo pale na kwa haya Tigo wanastahili pongezi:

  ....Utaratibu mzuri wa kutumia namba ili kuepusha migogoro ya foleni
  .... Mhudumu wa pale mlangoni anafanya kazi yake kwa ufasaha na hababaishi
  .... Mlinzi pia ana ushirikiano wa kutosha kwa wateja

  Sasa tatizo linakuja pale unapokwenda kwa wale akina dada watoa huduma......


  ....Hawako friendly hata kidogo, ukienda pale wanakuona kama unawasumbua
  ....wakati mwingine wanaacha kumsikiliza mteja wanazungumza kwenye simu
  ....kuna mmoja alipigiwa simu huyo akanyanyuka kwenda kupokea na aliporudi bila hata kumwomba samahani mteja anamuuliza "una shida gani?"
  ....wana tabia ya kupiga stori wenyewe kwa wenyewe huku wamemweka mteja pending
  ....mara wanatumiana sijui vitu gani online wanaambiana "iicheki hiyo" huku mteja ukisubiri
  ....Wana dharau sana wateja na wanatoa majibu ya hovyo hovyo
  ....wana tabia ya kutoa majibu ambayo hayaridhishi na siyo ya kitaalamu, ukiwauliza maswali zaidi wanakuonesha dhahiri kukerwa na maswali yako, mara washike simu mradi tu kukufanya ukate tamaa uondoke.
  ....Cha kushangaza wakati mwingine wanatumia hata kiingereza, ukiwauliza swali kwa lugha hiyo hiyo, wanabadilisha wanatumia kiswahili

  Jana ilikuwa mara yangu ya Tatu kwenda pale ili nisaidiwe kupata suluhu ya Tatizo hilo hilo, cha kushangaza waliniambia kuwa nimesajiliwa kwenye hiyo huduma ingawa hawakuniambia nilisajiliwa lini na katika kituo gani, kwa maelezo kuwa ni long process mpaka wanipe majibu yote hayo (nikaridhika). Kila ninapoomba kupatiwa namba ya siri ninaambiwa kuwa nitatumiwa ndani ya masaa 24 kwa sms, bado naisubiri hapa!

  TIGO licha ya mazuri yenu kwetu wateja, pamoja na matatizo mbalimbali mliyo nayo pia mnaangushwa na watu wa jinsi hii, manake mteja ninakwenda kwenye Ofisi zenu kutatuliwa tatizo lakini badala ya ufumbuzi wa tatizo langu ninaondoka pale nimekereka kwa sababu ya majibu ya dharau ya wahudumu wenu.

  Mapendo.
  TANMO.
   
 2. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #2
  Nov 10, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Wafanyakazi wa TIGO lack the thing called COMMUNICATION METHODS naposema hivyo namaanisha ATTITUDE TO CUSTOMERS (What the say, The way they say it, Their Body Language).
   
 3. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #3
  Nov 10, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,907
  Likes Received: 203
  Trophy Points: 160
  Inabidi wajifunze namna ya ku deal na wateja (ikiwa ni pamoja na kuwa na uelewa kuhusu Tigo in General) vinginevyo wanatufukuza..
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Nov 10, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  na hilo si tatizo la watu wa Tigo tu... customer care, in general, is a national problem in our beloved Tanzania
   
 5. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #5
  Nov 10, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,121
  Likes Received: 3,309
  Trophy Points: 280
  Wanajiona wamefika hao!
   
 6. u

  utantambua JF-Expert Member

  #6
  Nov 10, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  TIGO have customer disservice in lieu of customer service. They are the most inefficient service provider in the industry.
   
 7. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #7
  Nov 10, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mkuu you're right yaani ukienda kuhudumiwa it is as if hiyo huduma labda unapewa bure there is so much of Customer Promiscuity, sijui hata kama huwa wanafanyiwa Performance Appraisal
   
 8. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #8
  Nov 10, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,431
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  bongo customer care ni ziro ziro
   
 9. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #9
  Nov 10, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,907
  Likes Received: 203
  Trophy Points: 160
  Kwa hilo ni kweli Watanzania tupo nyuma sana, labda ni kwa sababu za kupeana ajira kwa vimemo hivyo watu wanashindwa kuwajibishana...
   
 10. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #10
  Nov 10, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,431
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  customer care za bongo bwana zinafurahisha kweli siku moja nilienda kutoa hela kwenye atm flani ikagoma mi nikaondoka zangu nikakaa tena siku nyingine nikaenda tena hamna hela kwenye atm inasema jaribu atm nyingine mimi nikaondoka zangu tena nikakaa kama wk 2 kwenda beki nilivokuwa naccomand kumbe ilikuwa inarecord nimetoa hela
  daah hao jamaa wakaniambia eti niandike barua ya maombi ya kurudishiwa hela nielezee na tatizo daah nilicheka kweli jamani
  ila sikuandika nikawaambia tutaonana mahakamani kesho yake wakanipigia hela zipo kwenye a/c
  vilaza kweli
   
 11. Achahasira

  Achahasira JF-Expert Member

  #11
  Nov 10, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu mimi nilikaribia kumtukana dada,nimepiga sim huduma ya wateja nimekaa saa zima.nikaaza kutaja matatizo yangu,nikawa simsikii vizuri yaani nasikia sauti kwa mbali sana.nikawa nauliza unanisikia niendelee.mara tusi likamtoka kwa ukali ma kwa sauti ya juu.
  muda wote anaongea mbali na mic kwenye matusi kaiweka mdomoni.
   
 12. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #12
  Nov 10, 2011
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Nenda pale Kamata wanaweza kukusaidia angalau wapo wanaojua wanafanya nini kazini.
   
 13. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #13
  Nov 10, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Customer care za bongo ni customer kero!! Its an opportunity lakini kuwashawishi wahudhurie uwafundishe namna ya kuhandle wateja mmmm!! Lakini ni serious problem nchini kila kona, pengine watu wanajali zaidi muonekano wa mteja na si kujali namna ya kumfanya mtu atoe pesa yake bila kushurutishwa kwa maneno mbofu mbofu!!
   
 14. KUN

  KUN JF-Expert Member

  #14
  Nov 10, 2011
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  tiGO ni matapeli kuanzia kampun yenyew mpak wafanya kazi wake
   
 15. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #15
  Nov 10, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Nenda sehemu nyingi bongo, utatamani ufungue biashara yako uwafundishe namna customer care inavyotakiwa!! Si ofisi binafsi, serikalini wala shirika! its worse! Better when you for Gambling in a cassino watu wanajali mtu na pesa yako.
   
 16. P

  Pretty P Senior Member

  #16
  Nov 10, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 120
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hata mimi yalinikuta hayo na iyo bank naifahamu fika ni tabia yao hao. ukikomaa wanaogopa na kukurudishia
   
 17. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #17
  Nov 10, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,626
  Likes Received: 1,381
  Trophy Points: 280
  Sio Tigo tu mkuu ni sehemu nyingi sana, halafu videmu vingi vya customer care huwa vinadhani kila mtu anataka kuvitongoza.. very childish
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...