wahudumu wa afya wamekuwa wamachinga

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
yapo mambo mengi yanayosababisha huduma katika vituo vya afya vya serikali kuzorota.lakini moja ambalo ni muhimu ni maslahi duni yasiyoakisi gharama za maisha.
Sasa hivi wahudumu wa afya hawachukui rushwa tena badala yake hujibebesha mapochi makubwa yaliyojaa pamba,gloves,dawa,mabomba ya sindano,pedi za kinamama,vinguo na pampers za watoto.haya yote ni mahitaji muhimu ya wanaofika hospitali ambayo mara nyingi hayapatikani kwenye hospitali zetu kwa sababu ya ukiritimba na ukosefu wa uwajibikaji.
Hawa ndo wahudumu wa afya waliojitolea kuwahudumia watanzania hata inapobidi kufanya kazi za kijasiliamali katika maeneo yao ya kazi.
 
Ila wanaowauzia husema na vile vilivyoletwa na serikali wahudumu wanauza.... Ukweli hawaujui kwani waliahidiwa huduma bure. Leo kuna mmoja kaambiwa akanunue gloves na canular kwa ajili ya mkewe kutoka nje anasema waliahidiwa na serikali huduma ni bure, nurse kumsikia kwa upole akamjibu vimeisha na Pesa hakuna huko MSD. Kazi ipo...... Wahudumu wa afya wasisitize kuboreshewa vitendea kazi.
 
Serikali yetu ndo imetengeneza mazingira ya jichukulie chako mapema
 
Ila wanaowauzia husema na vile vilivyoletwa na serikali wahudumu wanauza.... Ukweli hawaujui kwani waliahidiwa huduma bure. Leo kuna mmoja kaambiwa akanunue gloves na canular kwa ajili ya mkewe kutoka nje anasema waliahidiwa na serikali huduma ni bure, nurse kumsikia kwa upole akamjibu vimeisha na Pesa hakuna huko MSD. Kazi ipo...... Wahudumu wa afya wasisitize kuboreshewa vitendea kazi.
neno la huduma bure limetupumbaza sana,ngoja mabwana wakubwa wa kizungu wasitishe misaada ndio tujue kama huduma ni bure au imelipiwa.
 
yapo mambo mengi yanayosababisha huduma katika vituo vya afya vya serikali kuzorota.lakini moja ambalo ni muhimu ni maslahi duni yasiyoakisi gharama za maisha.
Sasa hivi wahudumu wa afya hawachukui rushwa tena badala yake hujibebesha mapochi makubwa yaliyojaa pamba,gloves,dawa,mabomba ya sindano,pedi za kinamama,vinguo na pampers za watoto.haya yote ni mahitaji muhimu ya wanaofika hospitali ambayo mara nyingi hayapatikani kwenye hospitali zetu kwa sababu ya ukiritimba na ukosefu wa uwajibikaji.
Hawa ndo wahudumu wa afya waliojitolea kuwahudumia watanzania hata inapobidi kufanya kazi za kijasiliamali katika maeneo yao ya kazi.

matatizo yz MSD unayajua lakini...??
Usilaumu burebure.. Sasa kama dawa na vifaa tiba hakuna MSD,au pesa haijaja toka serikalini kwenda MSD kwa ajili ya hospitali yenu..kwa nini usimwambie mgonjwa hata kama ni mja mzito aende maduka ya madawa akanunue? Sanasana kama kuna wagonjwa waliotumia vifaa walivyonunua kisha vikabaki mikononi mwa watoa huduma,ndivyo unaweza kusaidiwa ili usiende mbali kuvitafuta..
 
mkuu soma post yangu vizuri.nielewe.
 
Jamani hospitalini anayetibiwa bure ni mtu mwenye umri wa miaka 60 na zaidi,na muathirika wa virusi vya Ukimwi,basi!!
Wagonjwa wa TB na Ukoma,wanapata msamaha wa magonjwa hayo tu,lakini kama Malaria,Typhoid wanalipia. Na wengine kama hao ni wagonjwa wa akili..Psychiatric problems..
 
Kwa kweli kwa Tanzania ya sasa hakuna kazi yoyote ya wito. Ule msemo wa ualimu na uuguzi ni wito hauapply tena........kwa uzalendo gani?
 
mkuu soma post yangu vizuri.nielewe.

Pale mwanzo nilikuelewa vizuri J... Baada ya kusoma tena kama ulivyotaka,nimekuelewa vibaya..utaniuliza kwa nini..
Vifaa tiba mhudumu wa afya atavipata wapi? Akinunua maduka ya madawa ni ghali,halafu yeye auzeje?
It is impractical J...
 
Jamani hospitalini anayetibiwa bure ni mtu mwenye umri wa miaka 60 na zaidi,na muathirika wa virusi vya Ukimwi,basi!!
Wagonjwa wa TB na Ukoma,wanapata msamaha wa magonjwa hayo tu,lakini kama Malaria,Typhoid wanalipia. Na wengine kama hao ni wagonjwa wa akili..Psychiatric problems..
mkuu hayo makundi uliyotaja kutibiwa bure dawa zao zinachimbwa kama mitishamba au la?hakuna bure ,hata kwa babu ambilikile ni sh 500
 
nami nasikia kwenye magazeti kwa babu 500... Mi naongelea kitu ninachokijua kwa kuona kila siku,kwenye hospitali za serikali,si kusikia... Basi hapo ndo tulidiffer labda..
 
Pale mwanzo nilikuelewa vizuri J... Baada ya kusoma tena kama ulivyotaka,nimekuelewa vibaya..utaniuliza kwa nini..
Vifaa tiba mhudumu wa afya atavipata wapi? Akinunua maduka ya madawa ni ghali,halafu yeye auzeje?
It is impractical J...

it is practicle coz i hv seen it.watu wanaenda maduka ya jumla halafu wanaenda kuuza.labda nikuulize kuhusu pedi na vijiguo vya watoto kama na venyewe vinatoka msd.
 
Kwa kweli kwa Tanzania ya sasa hakuna kazi yoyote ya wito. Ule msemo wa ualimu na uuguzi ni wito hauapply tena........kwa uzalendo gani?

Nambie wewe, nasikia wanaitwa watu wa wito, mara wawe wazalendo!
mwee!
TANESCO, TANAPA, BOT, TRA, TANROADS, nk, nk, hawatakiwi wazalendo!
 
Hivi Kikwete na genge lake na familia yake wangekuwa mzalendo, nani angemnyooshea mwenzake kidole?
 
it is practicle coz i hv seen it.watu wanaenda maduka ya jumla halafu wanaenda kuuza.labda nikuulize kuhusu pedi na vijiguo vya watoto kama na venyewe vinatoka msd.

haya, sasa hizo pedi na vijiguo vya watoto vinahitajika wakati gani kwenye masuala ya matibabu?
 
mkuu wamama wangapi wanatumia pedi?wajawazito wakipata watoto wanauziwa nguo za watoto,nursing mothers vile vile wanauziwa nguo za watoto,labda hujawahi kuona na haya yote yanafanywa na wahudumu wa afya ili kujikwamua kimaisha.
 
akina mama wa aina hiyo nadhani ni wale ambao uhudhuriaji wao kliniki ni wa mashaka.. Maana wanaelezwa vifaa vya kujiandaa navyo siku zinapokaribia.
Ila wanaposhikwa na uchungu wa kujifungua wanaenda mikono mitupu.. Na hayo ndiyo yanayowakuta..
 
mkuu ina maana kliniki mama anaambiwa mambo ya pedi na nguo za mtoto?jitahidi kuelewa ninachokuelewesha.
 
umewahi kuoa katika maisha yako? Au umewahi kuhudhuria kliniki za wajawazito? Fanya uchunguzi kisha rudi tutakutana tu hapa..
 
Back
Top Bottom