Wahitimu wa vyuo waokolewe


Watu hawajiongezi kabisa, Mimi ni graduate lakini nafanya kazi aiendani na mm kabisa Lakini maisha yakenyooka sana, Vijana tunapenda sana uofisa, Akat watu tunatindua ukuta Zama Darini chimba sana mitaro [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] Maisha ni elimu tosha
 
Kama serikali imeshajua haiwezi kuajiri wanaohitimu kwann tuna gamble na pesa zinazowekezwa kwenye elimu kwa kuwapa wanafunzi mikopo ya masomo kwanini tusiweke katika bajeti ya mikopo ya biashara ili basi watu wajiajiri sasa kama tunavyotaka.
 
Suluhisho la hili tatizo ni ajira za kudumu ziondolewe, mtu aajiriwe kwa miaka 5 tu, baada ya hapo wakajiajiri....nadhani ikiwa hivyo itatatua hii changamoto ya ukosefu wa ajira, pia uchumi utakwenda kwa kasi kwa sababu sekta binafsi zitakuwa nyingi zikiongozwa na wasomi.
 
Kuwa graduate sio kizio cha utajiri
 
kuna kipindi nilikua nataka watu (2) wakushusha mizigo ya duka katoro uko.

mimi si mwenyeji wa kule hivo niliandika tangazo tu hapo mbele ya duka.
walikuja watu 16 .
kwa bahati mbaya/nzuri ni watu 3 ndo walikua na elimu ya form 4 ila 12 wote walikua wamefika chuo degree na diploma.
wa 4 walikuja na cv kabisa niliumia sana .

mmoja alikua na cv nzito mno mno ilibidi nijaribu kuisambaza kwa rafiki zangu asee
 
Sijawahi kusikia daktari bingwa wa upasuaji anakosa kazi; namaanisha tusome vitu au fani ambayo si kila mtu anaweza kufanya
Hujui unachoongea..ungia chimbo fanya utafit kidogo..vijana kuanzia 2013 wa MD weng wako mtaan..wengne wameshakata tamaa hata kujiendeleza kuwa mabingwa wamekata tamaa...kuna kad nying tu ambazo si kila mtu anaweza tena za science na engeneering na bado watu wako mtaan...miaka hii mi5 imekua mibaya snaa kwa wasomi wetu
 
Baadhi ya wahitimu huwa na mawazo yafananayo na yafuatayo:

1. Ajira maana yake ni serikalini au sekta ya umma. Ukisikia wanasema, hakuna ajira, maana yake sikupata ajira serikalini.

2. Wengi wanatafuta ajira, hawatafuti kazi.

3. Kozi za ufundi sanifu huonekana ni dhalili kwao, mfano za VETA.

4. Wengine huko vyuoni hawako siriasi na masomo. Ukiwaona, huwezi kuamini wamechukua mkopo ili waje shule. Shule ni kama pikiniki fulani ya kujimwambafai kitaa kwamba na miye niko chuo!

5. Baadhi huenda vyuoni kutafuta vyeti tu na siyo ujuzi wala maarifa.

6. Ukiwaambia wachukue vyeti bila kusoma, baadhi watakuwa radhi kufanya hivyo.

7. Mtaji wa kujiajiri uko wapi? Ni kisingizio tu.


Majuzi niliwauliza vijana fulani kuhusu kujiajiri, nikajibiwa "Mtaji!?" Nikauliza unataka shilingi ngapi ili uweze kujiajiri, jibu kizungumkuti.
 
Uko sahihi, ukiuliza ndio ana cheti...je anaweza kufanya kitu gani kinachoonekana...hapo ni blablaa, nadhani tusome fani zinazotuachia ujuzi fulani wa kutengeneza kitu na kukiweka sokoni, tukiwa tunalalamika umri unaenda na utatuzi hakuna, njia sahihi ni kupambana wewe mwenyewe kwa kutafuta ujuzi sahihi, ata ukiajiriwa na ukaachishwa kazi,uwe na uwezo wa kutengeneza au kutoa huduma fulani (kujiajiri).
 
Umekosea san kucompare mtu aliesoma fani na mwingne alieenda kusomea vyeti kwahyo toa hako na ujinga kichwani pili kunywa maji utulie

Hlaf ujiulize utafanya nn October kwenye box la mpiga kura

Over
 
Kama serikali imeshajua haiwezi kuajiri wanaohitimu kwann tuna gamble na pesa zinazowekezwa kwenye elimu kwa kuwapa wanafunzi mikopo ya masomo kwanini tusiweke katika bajeti ya mikopo ya biashara ili basi watu wajiajiri sasa kama tunavyotaka.
Ndio shida ya serikali zisizojitambua.

Wanakinga maji kwenye kapu la ukindu.

Mradi tu jua limechomoza na kuzama basi tunachanja tu mbuga kama gari-moshi lenye hitilafu ya kiteknikali.
 
Hio ndio suluhu, ajira ziwe za mkataba ili watu wawe phased out! Ina maana baada ya miaka 5 intake ya waajiriwa inabadilika. Itasaidia walau watu watakuwa na uwezo wa kimtaji.

Kikubwa tu walipwe mishahara mizuri ili hata wakiondoka wawe na mitaji yao tayari.
 
Hapo umezungumza bonge la point....... Yaani kwa mfano hao wanaosema tujiajiri balaa lake hawalijui. Kujiajiri ni safari ya kurudisha akili yako the day kabla haujaenda shule ili ujiulize unaweza fanya nini na vipawa na vipaji vyako......

Sio jambo dogo kudadadeki.....

Tunachojua kuexport sisi ni pembe za ndovu na madini plus mawe ya almasi na tanzanite.

Vitu vingine ni chenga tupu.......
 
Kumbuka hao watu wamekuwa trained kuwa maofisa na ndio maana wanabehave hivyo.....

Unapokuwa trained kama mtu wa aina fulani unategemewa kufanya majukumu ya huyo mtu.....

Huwezi ukasomea degree ya u daktari halafu uje kuwa mkulima au mhasibu. Hiyo ni kupoteza muda na pesa.

Kama tunajua watu wakisoma hawaajiriki then kwann tusiamue tu kusitisha hizo trainings za wasomi wa vyuoni tutumie hiyo pesa kufanyia mitaji ya biashara maana pesa ya miaka mitatu ya tuition fee plus accommodation ni pesa mingi sana.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…