Kama kweli tunataka kuwa wavumbuzi wa system mbalimbali, ni lazima tuwe fit katika THEORY. Kama tunataka tufanye transformation ya mambo tunayosoma darasani into real working systems, ni lazima tuwe fit katika PRACTICAL. Kwa hiyo, hakuna mtu mwenye akili timamu anayeweza kujitokeza hadharani kama hapa JF na kujivunia kuwa yupo fit katika kimojawapo; syllabus za vyuo hivyo viwili (DIT na UDSM) zinaelekeza ujuzi katika maeneo yote ya theory na practical.
MATOKEO
Kama mtu atakuwa na theory halafu akakosa practical ya kutosha, atakuwa anasumbuliwa na msukumo wa kujua jinsi mambo aliyoyasoma vitabuni yanavyokuwa implemented. Anaweza kudhalilika kazini kwa muda mfupi, lakini huyu ana nafuu zaidi kwani ana nafasi ya kujifunza bila kurudi darasani, na akijua practical anakuwa mzuri zaidi na kuweza kuvumbua teknolojia mpya ili kuboresha systems.
Kama mtu atakuwa na practical halafu akakosa theory, atakuwa ana kikomo cha ufanyaji wake wa kazi; atakuwa mzuri kwa existing systems lakini hataweza kufanya uvumbuzi wa teknolojia mpya ili kuboresha systems. Silaha yake zaidi itakuwa ni kazi iliyopo mbele yake, na ili aweze kuwa mtu wa Teknolojia, atalazimika kurudi darasani kuongeza maarifa, na mara nyingi atalazimika kwenda katika training/short courses mbalimbali, vinginevyo atapitwa na wakati (obsolete).
Kwa hiyo, kuwa fit katika vyote ni bora zaidi, ila kama rasilimali haziruhusu kujua vyote, basi mimi binafsi ningechagua kwenye THEORY zaidi, kwani kwa mtu aliyekwisha hitimu na kuondoka chuoni, practical ni rahisi kujifunza (kazini) kuliko kujifunza theory (kurudi darasani)!
NB: Bahati nzuri nimepita kote huko; Iyunga, MIST, DIT na UDSM