Wahindi wote waliosoma wanajua kingereza, huku lugha yao ya taifa kihindi, why not Tz

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
8,822
33,526
habari wadau.

nimekuja india kikazi. nimeona wahindi wanajua sana kuongea kiingereza.. hata wa mtaani.. anaongea english nzuri japo wana mother tongue yao..

lugha yao ya taifa sio english ni kihindi... ila wanajua sana english..

nawaza tu why not Tanzania...

hata ambao tumeenda shule wengi wetu hatuwezi kuongea english iliyonyooka hata kwa dakika 10 mfululizo..

mfano hai presentation vyuoni, ama ma ofisini
 
huwa wanaongea kiingereza kichafu.
sisi wabongo huwa hatujiamini. Hatutakio kuongea kiingereza chenye lafudhi ya kiswahili.
Tumejiwekea malengo ya kuongea kama waingereza kitu ambacho hakitatokea.

Las Simba ingilia kati mkuu uokoe jahazi.
 
Hiko penda sana Ruga ya malikia huko Bombay shoma sana sunche Patel hii kapeto jua sana chingereza hiko kuja mimi na bachan mituni fundisha nyinyi yote hapana lia
 
huwa wanaongea kiingereza kichafu.
sisi wabongo huwa hatujiamini. Hatutakio kuongea kiingereza chenye lafudhi ya kiswahili.
Tumejiwekea malengo ya kuongea kama waingereza kitu ambacho hakitatokea.

Las Simba ingilia kati mkuu uokoe jahazi.
Kiingereza chao sio kibaya, ila lafudhi ndio majanga
 
Hapa kwetu, wanasiasa ndio wanatuvuruga! Unstable teaching language policy, hypocrisy, they sent their offsprings to study abroad!
 
Kule India kihindi ni kama lugha ya kikabila tu, hivyo kila mtu anakijua, na kiingereza ndio kama lugha ya taifa tu, hivyo kila mtu anakijua. Huku hatutaki utumwa.
 
Kwani sisi hatuna lugha ya taifa?

tunayo kiswahili. hata wahindi wanayo kihindi , hata waganda wanayo kiganda, swali langu why wanajua sana english huku wenyewe kwa wenyewe wanaongea lugha yao muda wote...

sisi tunajua kiswahili pekee. english wengi hatujui japo tunafundishiwa shuleni
 
tunayo kiswahili. hata wahindi wanayo kihindi , hata waganga wanayo kiganda, swali langu why wanajua sana english huku wenyewe kwa wenyewe wanaongea lugha yao muda wote...

sisi tunajua kiswahili pekee. english wengi hatujui japo tunafundishiwa shuleni
Okey sasa hivi ndio nimeipata vema point yako
 
habari wadau.

nimekuja india kikazi. nimeona wahindi wanajua sana kuongea kiingereza.. hata wa mtaani.. anaongea english nzuri japo wana mother tongue yao..

lugha yao ya taifa sio english ni kihindi... ila wanajua sana english..

nawaza tu why not Tanzania...

hata ambao tumeenda shule wengi wetu hatuwezi kuongea english iliyonyooka hata kwa dakika 10 mfululizo..

mfano hai presentation vyuoni, ama ma ofisini
India ina watu bilioni 1.3, Tanzania milioni 60, sasa wahindi milioni 100 wakijua kingereza utaona ni wengi ila ki asilimia sio wengi wanaojua kingereza
 
Ukirudi Tanzania hakikisha unawazoesha watu wa karibu yako kuongea kingereza. hii itakuwa njia ya kwanza ya kutatua hilo tatizo kisha ndio tuanze kuilamu serikali.
 
fika india uone.. wanajua sana.. india ukijua kiingereza kama ni mgeni hukosi huduma popote.. mimi nipo india naona kwa macho sio story
 
Tatizo ni attitude ya Serikali (hasa ya awamu hii) inaaminisha watu kuwa Kiingereza hakina umuhimu, Rais anahutubia anawaambia wananchi kuliko muwafundisge watoto wenu Kiingereza wafundisheni vilugha vya makabila

fika india uone.. wanajua sana.. india ukijua kiingereza kama ni mgeni hukosi huduma popote.. mimi nipo india naona kwa macho sio story
Kwa population ya India unaweza kuona ni wengi wanaojua lakini hapana, na inategemea na maeneo, halafu kingereza chao nacho ni mtihani kukielewa
 
Halafu shida nyingine ya Tanzania ni kwamba ukiongea kingereza kama muingereza basi ndo unaonekana unajua kingereza, wakati wahindi, waarabu waNigeria wanakiengereza kilicho na lafudhi ya lugha mama
 
Back
Top Bottom