Wahindi wana Mashamba Makubwa sana nchi hii.

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,789
8,917
Watu wengi tunawachukulia poaa sana Wahindi,kisa wanaishi mjiji.Ila ukweli ni kwamba wahindi wamewekeza sana kwenye Aridhi,Wana mashamba makubwa na ya kutisha.

Binafisi nimetembelea Wahindi kama 9 Arusha mashambani kwao,wana mashamba na wamewekeza sana,Wengine utasikia wanasema wana mashamba Tanga,wengine Singida huko.

Kwa Arusha na Moshi wana mashamba makubwa sana.Tunawachukulia poa sana ila jamaa ni wakulima,usiwaone wanashinda kwenye Maduka ukawachukulia kawaida.Pia wanajua sana kilimo jamaa.

Ni wakulima wazuri sema hili hatulijui sisi,na wanafuga na kulima pia.
 
Na Wana supply bidhaa za kilimo kwenye masoko ya Kimataifa. Ukimuambia kijana wa kiume wa Tanzania aende shambani atakuambia Hana mtaji. Yaani anataka awe na kuanzia milioni tano ndiyo aanze Kipimo 😅

Wanachotaka ni kazi ya bodaboda, kukaanga chips mayai na kuuza nailcuts
 
Sio mtaji tu mkuu hata ile moyo tu wa kuwekeza ktk kufanya lolote uwekezaji moyo huwa vijana umepotea kabisa, mtu anakubali kuwa mtumwa wa nafsi yake badala ya kujituma kwaajili ya maendeleo yake ya baadae. Tamaa ya maisha mazuri wameiweka mbele wakasahau kuna kufanya juhudi binafsi hayo maendeleo yaje,.
 
Wahindi wanalima kisasa alafu pia wanajua kufanya marketing ya products zao; kweli alietunga shairi la mali utaipata shambani hakukosea
 
Back
Top Bottom