Wahindi walivyo na umoja,wataendelea kufanya biashara zao hapa Tanzania au wataondoka?

Hakuna kitu hawa jamaa kwakiasi kikubwa wanatuhumiwa kwenda kufisha pesa nje ya nchi pia huwa hawaweki pesa bank ss unasemaje wakiondoka watanzania watapata shida hapa cha muhimu waishi kwa kufuata sheria sio magumashi
 
Pesa zenyewe wanaficha uswisi huku hata vibanda vyenyewe vya kuishi hawajengi wamekomaa tu na NHC, majeshini iwe JWTZ, hatuwaoni wala magereza, polisi au hata mwalimu au nurse shule za kata huko

- Raia gani hawa wabaguziiii, wakiona maslahi kama ubunge ndo wanataka na kujiita watanzania, stupid gabachoriiii
 
Wahindi wapo na wataendelea kuwepo, Manji yupo na ataendelea kuwepo.

Ukiisoma historia ya pwani ya Afrika Mashariki, Wahindi walikuwepo kabla ya Wabantu kuja pwani hii.
Duh alafu wageni wanaitwa waafrika wenyeji wanaitwa wahindi_Indians
 
haha mmeshindwa kujikwamua toka enzi za elnino mje mjikwamue kwenye matetemeko.mh! ama kweli usiombe kukumbuka shuka kumekucha.Dunia yenyewe ya kwanza ina matatizo sembuse hii ya mwisho tusidanganyane jaman.watu waache kujifanya miungu watu na ndo mana Mungu kawadis wamebakia tu kumtaja kinafki ipo siku tu
achana na fikra potofu
 
Kama wakiamua kuanza waseme haraka mie nikawai fremu zao za duka, nitapumzika kuzunguka na biashara yangu
 
Tumekuwa tukipiga kelele humu juu ya Wahamiaji haramu na wote wanofanya kazi bila vibali,kuanzia jamii ya Kihindi mpaka wale Wachina.Mkuu Salary Slip kwa heshima kubwa kabisa wewe ni mmoja wa watu waliopigia kelel suala hili.Sasa kama jamaa kaanza na Manji (Muhindi unemsema) basi tumuache.Sasa sisi tunapenda nini?Utashangaa Watu wanamtetea Manji,wakati huo huo inajulikana jinsi anavyofanya mambo kimagumashi.Kuanzia wafanyakazi mpaka madili yake.

Ukweli kote kote huyu jamaa hachomoki
Huku kwa Mkemia na huku Uhamiaji

Unajua kuna "Utawala wa Sheria" na "Utii ktk Utawala wa Sheria"...Unaweza kuwa ktk nchi yenye utawala wa sheria,lkn wewe mwenyewe sio mtii wa Utawala wa kisheria.

Kumuita tu kiongozi "mpu..mbavu" ambaye pengine alilokuwa analisema kasimama kama kiongozi na si mtu binafsi ni kuitukana mamlaka iliyomuweka!Hata mimi na wewe tutatukana tu humu kwenye keyboard,lkn huwezi kutoka hadharani na kumuita Rais au muwakilishi wake majina kama mphumbavu,mjinga and the like.Utawala wa sheria ni pamoja na kutii utawala ulio kisheria.

Hivi kulikuwa na haja ya basi la wachezaji wa Yanga kupita Central polisi wakati Manji yupo anahojiwa?Haja ya kwaya kwenda kuimba?Hivi eneo la Polisi na mahakama si ndio kuna zile alama za horn kuwekewa \ (mstari) ikiwa na maana ya kuacha kupiga kelele??Haya yote yanakuwa yanashiria nini kwa vyombo vya dola na serikali iliyopo madarakani?

Kweli hatumpendi JPM (sio wote wasiompenda) lkn pia msimchokoze,yeye naye ni binadamu,ana nyongo,kwanini ukamdharau kwa kwenda na wapambe wa kulifuta gari mbele ya kituo kikuu cha Polisi??

Wahindi wengi huwa wajanja sana!Wanajijua jinsi walivyo wazee wa shortcut,ndio maana huwezi kuwakuta upinzani zaidi huwa upande wa dola na kusaidia ili biashara zao zilindwe.

Kama unajijua una magumashi,tulia,acha mbwembwe...Mwenzake MO katulia tuliiii!!Inajulikana mashamba ya Mkonge kuanzia Moro mpaka Tanga kayapata "kimagumashi" na kuyakopea mkopo!!Katulia tuliii asimguse kipofu.Alipomaliza kuweka mambo yake sawa,kwa kutumia kofia ya ubunge na dilpomatic passport yake,MO "akastaafu" siasa akiwa ndio kwanza 40.Sasa tunamsoma kwenye Forbes tu

Sasa Manji ulianza na Coco Beach,ukaonywa,maghala ya NSSF na madili kibao!!Tulia,upo nyumba ya vioo.Watu wanjua njia zako za mkato...Tulia

Huko nasikia Wahindi wa viwanda vya Pugu Road wanapaki mabegi,maana hawana vibali.Tembelea pale kiwanda cha NIDA mkabala na Uhai Production,kuna wapakistan wanatoka usiku tu.Pembeni yake kuvuka daraja kuna jengo wanakaa Wachina karibu na kituo cha mafuta tabata relini,wanatoka usiku tu.Ukija ilipo kampuni ya magari ya usafirishaji ya RAMADA wamejaa Wasomali ambao jua wanaliona wakati wa mawio na machweo tu,wanashinda ndani tu kazi ndani kwa ndani.Sasa hivi wameanzisha hotel wanapika ndani kwa ndani mnaona msosi tu
Bora umeongea mkuu yani wapinzani wengi wetu hata harujielewi nashindwa mpinzani anapata wapi ujasiri wa kumsifia na kumtetea Manji tunakua hatuna tofauti na watu wasiojielewa hivi Kuna ufisadi wa waziwazi mkubwa kama wa Manji na rushwa ya nje nje ya mabilioni.

Wengi hawajielewi kabisa hawana tofauti na upande wa pili.
 
mwisho watakao umia niwatanzania,wahindi wana umoja,watanzania tujiandae na anguko kubwa la kiuchumi,kwa sababu asilimia kubwa ya uchumi wa nchi yetu imeshikwa na wahindi,visasi vitatumaliza haya yote ni kwasababu manji alimsaidia membe kwenye kampeni,pole manji
Kumsadie kutoa rushwa kwa wajumbe ili wamuunge mkono awe rais alafu alipwe fadhila kwa migodi na kupitisha bidhaa zake bure bandarini.

Wenye akili ni wa chache sana Watanzania tunatia aibu tunalia umasikini kumbe umasikini tunao wenyewe kichwani.

Mungu akusaidie.
 
watu wote maharamia hawajakatazwa kuondoka. Wapo wahindi wengi tu wanafanya shughuli zao halali na kufuata taratibu za nchi. Hawa hawawezi ondoka eti mtumia madawa ya kulevya fulani au mhujumu uchumi fulani anapelekeshwa
 
Hawa watu wana umoja sana na pia huwa ni wepesi kuhama nchi, kuhamishia fedha zao nje ya nchi au kufunga biashara zao pale wanapoona kuna mazingira ambayo sio mazuri au rafiki kwa biashara zao na hata usalama wao mfano nyakati za uchaguzi au panapokuwa na ghasia za kisiasa,n.k.

Sasa kwa desturi ya hawa wenzetu na halii hii inayoendelea hapa nchini,hawa jamaa wataendelea kubaki nchini au watafunga biashara zao na kuondoka?
Wewe ungependa wafanye nini?
 
Nahisi wataondoka! Ila tujifunze kitu ...
Watanzania hatuna uzalendo, hatupendani, hatuthaminiani ... ndiyo maana tunawaheshimu wageni zaidi ya wenyeji. Waondoke tujipange upya kurudisha uzalendo.


Uzalendo huwezi kuurudisha kama unawekewa kiongozi usiyemtaka kwa mtutu wa bunduki
 
Umeelewa swali?
Tatizo kubwa hapo moja hakuna atakayelielewa swali maana hakuna swali la kujibu sababu umeliweka kiitikadi zaidi. Huyu jamaa angeachwa mngesema wamemwacha sababu ni ccm kila kukicha hata kama kizuri kimefanyika mnataka kuleta longo longo. Mimi katika wiki kama mbili zilizopita nilikuwa mstari wa mbele kumsema Magufuli na nitaendelea kumsema Magufuli kwa baadhi ya mambo lakini kwa hili siwezi kuutoa utu wangu kumtetea mtu anayethubutu kumkashifu na kumdharau kiongozi wa serikali sababu ya utajiri wake. Huyu anavuna alichokipanda na kama kuna wenzake wanaojishughulisha na hiyo biashara basi waungane naye tu wahame nchi ni bora. Sijaona kibaya alichokifanya Makonda kumtaja huyu jamaa si Tanzania tu hata kwingine duniani watu huwatangaza watuhumiwa ili mradi tu hakusema kuwa ni muuza unga alichokisema Makonda kuwa ni mtuhumiwa.
 
Waende tu ili na sisi tupate nyumba za NHC kwa kodi ya laki moja mitaa ya posta.
 
Wahindi wapo na wataendelea kuwepo, Manji yupo na ataendelea kuwepo.

Ukiisoma historia ya pwani ya Afrika Mashariki, Wahindi walikuwepo kabla ya Wabantu kuja pwani hii.
Wahindi na Waarabu nani aliwahi kufika pwani ya Azania?
 
Back
Top Bottom