Wahenga tu: Katika awamu 5 za serikali ya JMT zilizopita ipi unaikubali zaidi kwa Utendaji uliotukuka?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,933
141,900
Tujikumbushe.

1. Awamu ya kwanza Rais Mwalimu Nyerere RIP

2. Awamu ya pili Rais mzee Mwinyi

3.Awamu ya tatu Rais mzee Mkapa RIP

4. Awamu ya nne Rais mzee Kikwete

5. Awamu ya tano Rais Magufuli RIP

Maendeleo hayana vyama!
 
Awamu ya 3 ndiyo ilikuwa na mabadiliko + kwa wananchi. Japo nilikuwa bado mwanafunzi lakini nakumbuka kuona maisha ya watu yakiboreka sana
Nimekuelewa kwa sababu hukuwepo awamu ya kwanza.

Kila hitaji lilikuwepo tena Made in Tanzania.
 
Awamu ya pili ndio msingi wa maendeleo ya leo

1) vision 2025 andiko lake lilianza 1994
2) Soko huria liliasisiwa 1992
3) Structural Adjustment Program (SAP) ni kazi ya Mzee Mwinyi kuachana na mfumo mfu wa ujamaa
4) fursa ya kurudishwa vyama vingi vya siasa na mabadiliko mengi ya kiuchumi yalikuwa wakati wa Mwinyi
5) Mchakato wa kupunguza wafanyakazi ili uwiano wa wafanyakazi na kazi wafanyazo ulingane na waliopo waweze kuboreshewa maslahi uliasisiwa 1993-95
6) Uhuru wa kujieleza na kukosoa ukatamalaki
7) Mapambano dhidi ya rushwa hadi kufikia kufukuza baraza lote la mawaziri kwa kuthiri kwa rushwa hapo Jan 1990
8)kuanzisha mchakato wa kuachana na Idara ya kodi na kuanzisha Mamlaka ya kodi ulianza wakati wa Mwinyi na kuzinduliwa 1996 muda mchache baada ya Mkapa kuwa Rais
9) kulizika Azimio la kishamba la Arusha
10) Uchumi kuchangamka na Raia kuanza kujenga na kufunguka sana kwa shughuli binafsi
 
Back
Top Bottom