Wahaya zaidi ya uwajuavyo!

Judgement

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2011
Posts
10,326
Reaction score
4,789
Jirani ninaishi na Mzee wa kihaya , (jina hifadhini).
Ni Mzee aliye attend shule vizuri.

Aidha baada kustaafu , tayari alikua ameshawekeza vitega uchumi vya majumba kadhaa.
Nyumba mbili amezipangisha watu binafsi , na mbili ni Guest House.

Mzee huyu amejipatia umaarufu ktk constituency yetu kufuatia uwezo wake , na pia vituko vyake.

Alishatalikiana na mkewe miaka iliyopita.
Watoto wake ni wakubwa wakiwa wamesambaa mikoa tafauti na shughuli zao.

Burdani ya Mzee huyu , mbali ya kua na nyumba kadhaa , bt hajabakiza ya makazi yake.
Anaishi kwenye chumba kimoja miongoni mwa guest zake.

Wakati flani binti yake aishie Ar alifika kumtembelea. Ikabidi afikie guest , ktk hali isiyo ya kawaida Mzee aliamrisha bintie tozo la pango such as normal customer.
Binti hakua na hiari zaidi ya kulipa , kwa 3days alizokaa na kuondoka zake.

Miezi kadhaa ikapita , akaja mwanae wa kiume toka Dar.
Nae alipofika akakwaana na dhahma kama aliyoikwaa dadie, akalipia room siku 2 akasepa.

Kijana huyu alipofika Dar, ikiwa imepita miezi kadhaa akabuni ni jinsi gani nae amtie adabu Mdingi.
Akampigia simu na kumwambia "Baba mimi naoa next wiki , fanya juu chini ufike , tumia nauli yako , na utarudishiwa ukifika"

Mdingi bila ajizi akafanya kama alivyoagizwa.
Akafika Dar siku aliyotakiwa afike.
Na kijana akafika kumpokea.
Wakachukua Tax na walipofika Mwembechai kijana akamwambia dreva asimame dukani akimuacha Mdingi garini.

Kilichofata kijana ndy akawa amesepa mazima!
Na simu yenye No zake ambazo Mdingi hutumia kumpata yeye akazima.

Kilichojiri huku nyuma Tax driver alimkomalia Mdingi ashuke na alipe kwani hakua na ramani ampeleke wapi !
Dingi hakua na hiyari zaidi ya kulipa , kisha akatafuta guest akajilipia malazi , na palipo kucha akaenda kata ticket kurejea alikotoka!
Hivyo ni baadhi ya vituko vya wahaya.
 
lakini ,,,,,,,sidhani kama vituko kam ahivi vinafanywa na wahaya tu!!! naamini ni tabia ya mtu atokaye kwenye kabila lolote!!

au Judgement unataka kusema kuna wahay zaidi ya wangapi washafanya hiki kituko???
 
Last edited by a moderator:
lakini ,,,,,,,sidhani kama vituko kam ahivi vinafanywa na wahaya tu!!! naamini ni tabia ya mtu atokaye kwenye kabila lolote!!

au Judgement unataka kusema kuna wahay zaidi ya wangapi washafanya hiki kituko???

Sina maana wahaya wooote wako hivi !
Laa!
Bt majority wana vituko, mbwembwe, mikogo , kujidai , maringo etcetera!
 
Last edited by a moderator:
Hivi ni kituko cha aina gani , kukitoza gharama ya malazi , kitu ulichokikojoa mwenyewe!
 
lakini ,,,,,,,sidhani kama vituko kam ahivi vinafanywa na wahaya tu!!! naamini ni tabia ya mtu atokaye kwenye kabila lolote!!

au Judgement unataka kusema kuna wahay zaidi ya wangapi washafanya hiki kituko???

Afadhali dadangu Paloma umesema......wanatubambikia hata vitu general vya tabia ya mtu binafsi.
 
Last edited by a moderator:
afu nlitaka nikumensheni........sijui bananaboy Bishanga keshapita hapa?!??!

Nina wasiwasi sana na Bishanga!
Unaskia Paloma, navyomjua anavyowangaga majukwaani usiku, na hii Sredi ipo since y'day , atakua kapita! Isijekua kijana aliyemtelekeza Mdingi akawa ndy yeye!
 
Last edited by a moderator:
huyo mzee ana akili sana

Nitty !
Akili ya una nyumba 4 then ukaishi kwenye chumba kimoja, umejichanganya na wateja, akili ya hivyo binafsi yangu siitaki.
 
Last edited by a moderator:
Bishanga kaka umepita huku? Paloma yaani ss wahaya hatuna jema. Mzima lakini mummy?

Shemeji nimekuona unalalamika kitambo!
Acha kulalami mpenzi , hayo ni matukio tu!
Afu kwa taarifa mi wahaya ni watani zangu , na hapa nilikua sijawananga wanung'una! Ningeweka na utani shem sijui ungepovu ?
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…