GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
Moja ya ' Kanuni ' Mama kabisa ya Uandishi wa Habari ni kuwa Neutral and Fair hasa katika upelekaji wa taarifa kwa mlaji au walaji wako lakini hii tabia nimeivumilia kwa muda mrefu sasa na leo MWANAMUME nimeona ' yamenifika ' shingo na kuamua kuwatemea ' nyongo ' Wahariri wote wa Vyombo vya Habari hasa vya Magazeti kwa aina yao mpya ya ' ubakaji ' na ' unajisi ' kwa tasnia ambayo taratibu sasa inaelekea ukingoni kuanza kuheshimiwa na Walaji.
Haiwezekani kabisa eti leo ukiondoa tu Gazeti la ' Kinafiki ' la Bingwa hakuna Gazeti lingine lolote lile ambalo limeandika taarifa ya Timu ya Yanga FC ' kufungwa ' Goli 4 kwa Bashite / 0 jana huko nchini Algeria na Klabu ya MC Algiers huku mchezo ule umeisha mapema tu mnamo Saa 3 na dakika 55 usiku muda ambao nina uhakika kuwa Watu wengi wa News Room huwa wapo Kazini.
Uchungu zaidi kama siyo hasira zinanipanda pale ninapokumbuka kuwa ni mwaka huu huu wakati wa Michuano ya Kombe la Mapinduzi kule Visiwani Zanzibar Klabu ya Simba SC ilikuwa inacheza na Taifa Jang'ombe na nakumbuka mechi ile ilimalizika usiku wa Saa 5 na dakika 4 hivi na Simba SC ilifungwa lakini Kesho yake asubuhi tu Front Page ya Magazeti yote nchini habari uza yao ilikuwa ni ' Kufungwa ' kwa Simba lakini jana kufungwa kwa Yanga FC kule Algeria huku mpambano huo ukiisha mapema tu leo hawajaandika.
Jamani Waandishi wa Habari na hapa nawalenga sana Wahariri ( Gate Keepers ) Kitaaluma kuwa nyie wana Tasnia ndiyo kila siku mmekuwa wa Kwanza kuwasema wenzenu wa Tasnia zingine kwa kutokuwa na ' Ueledi ' je hivi na nyie hivi Vitendo vya kuonyesha upendeleo wa wazi wazi kwa Yanga FC na kupenda ' kuiangamiza ' na ' kuichafua ' tu Simba SC kila ' uchao ' ndiyo aina ya ' Maadili ' yenu mliyofundishwa huko Vyuoni mlikopita?
Na ili muone kuwa hata Mwenyezi Mungu hapendezwi na huo ' Unafiki ' wenu tena ' uliotukuka ' kabisa wa Kitasnia ndiyo maana kila na kadri mnavyojitahidi ' kuipamba ' na ' kuisifu ' Klabu ya Yanga FC ikishiriki tu Michuano ya CAF huwa ' inaangukia ' pua ( kufanya vibaya ) mapema sana na pengine hii ndiyo ' laana ' ya Mungu kwa aina ya Uonevu usiovumilika wa Kiuandishi wa Habari mnayoifanyia Simba SC mara kwa mara.
Ni matumaini yangu makubwa kuwa ' Ujumbe ' wangu huu ' murua ' kabisa utawafikia hata kama utakuwa ' mchungu ' Kwenu ILA kama kawaida yangu GENTAMYCINE huwa ' silei ' upuuzi na upumbavu na ndiyo leo nimeamua kuwatemea rasmi ' nyongo ' yangu hii japo nina uhakika kuwa pamoja na Yanga FC ' kufungwa ' na ' kufurumushwa ' kabisa Mashindanoni CAF Kesho katika Magazeti yenu mtakuja na Headlines zile zile za ' Yanga yafa Kishujaa ' au ' Yanga yafa Kiume ' au ile ya ' Bahati yao MC Algiers '.
Badilikeni upesi!