Kunawale wanaoendelea kutafuta sababu ya janga la mlipuko ambalo ni jambo la msingi kabisa. Lakini hali halisi ni kwamba kunawatu ambao wameathirika na mlipuko huo, ambao hawatakuwa na mahala pa kulala kwa siku chache zijazo, wengine watakuwa hawana chakula, wakati wengine watakuwa wamepoteza mali na ndugu zao ama watoto wato. Jambo la msingi ni kufikiria hawa watu watalala wapi, watakula nini na familia zao zisipoteana na serikali kuonyesha uwezo wake wa kuwalinda wananchi wake ikishirikiana na taasisi mbalimbali za kijamii!
Maoni yangu
Vyombo vya kijamii pamoja na serikali zile za mitaa ikishirikiana na watu binafsi watoe maeneo machache ambayo watu watalala humo! Watu wajitolee magodoro, vyakula, na maswala ya afya ili watu waishi humo kwa siku chache mpaka hali itakapokuwa shwari. Hii itasaidia familia kutokupotezana. Serikali kuanza kufanya taathimini ya maafa na kufanyia eneo uchunguzi wa kina, na watu wenyewe kuwa na imani kwamba watakuwa salama!
Makumbi ya kuwaweka wahanga yapo mengi tu ni yale tunayofanyia harusi! hilo ni wazo tu ndugu zangu! Maana akili yangu hanipi picha kabisa watu kuanza kuhangaika wapi watalala ama kula. Watoto wadogo kutangatanga bila mwelekeo. Hofu hii sio ndogo ndugu zangu, na kama jamii tunatakiwa tuwasaidie waliopata janga hili maana sio tu watu hawana chakula ama malazi ila kunawatu hata akili zao zitaathirika hasa pale watakapoachwa mitaani kujilinda wenyewe.
Ile bajeti yetu ya maafa ndio ifanye kazi sasa!