View attachment 400899Kuna maneno nimewahi kuyasikia mahali, mkulu mmoja akinena na kusemezana na watu wake kuwa anataka tabaka fulani liishi kama shetani! Leo hii kwenye post hii ningependa kupingana naye kwa nia njema kabisa! Kama kuna mtu au watu wanaishi maisha ya kifahari hapa duniani basi ni wale wanaomtii shetani..labda kama alimaanisha kuzimu/jehanam ila akakosea kidogo kutofautisha kati ya kuzimu/jehanam na shetani
Huko mahali sio kizuri ila kiuhalisia hakuna hata mmoja alishawahi kufika huko na kutuletea ripoti kamili zaidi ya kusoma kwenye Misahafu na maandiko matakatifu
View attachment 400914hii dhana ya kuzimu hii hii dhana ya jehanam ni kwa wale waamini na waaminio kwenye kiama, ni kwa wale waaminio kwenye hukumu ni kwa wale waaminio kwenye jehanam na kuzimu
Kiuhalisia ni kwamba kuzimu na jehanam viko hapa hapa duniani! Pepo pia iko hapa hapa duniani
Kiama tunachokiogopa sana hakijafika kuzimu tunakokugwaya hakuko mbali tunaishi nako
Maisha baada ya kifo ndio huamua mustakabali wa roho yako! Kama itabaki pale kaburini kimya kwa hali ya utulivu na kutobughudhiwa na hali yoyote ile (hii ndo pepo ya marehemu) au itatoka kaburini na kutangatanga ulimwenguni au itachukuliwa na wachawi na kufanywa msukule au kutumiwa kwa namna yoyote hasi (hii ndio jehanam yake)
View attachment 400935
Tunaombea marehemu walale mahali pema peponi huu ni uzushi na maneno ya faraja tuu! Labda kama ni kwa muktadha na maana ya nilichoandika japo juu
Kwahiyo wandugu marehemu wengi ni wahanga wa kuzimu bila kujua na bila uhalisia bali ni kutokana na maneno yetu...! Kuzimu na jehanam za kweli vipo huku huku duniani kwenye hospitali zetu kwenye Magereza zetu kwenye mitaa yetu kwenye nyumba zetu kwenye misitu na zile sehemu zisizojulikana na kuonekana na wengi huko kuna jehanam zenye mateso na maumivu ya kila aina! Ila kwakuwa tumezingwa na ufahamu duni tunaangalia lakini hatuoni tunasikia lakini hatuelewi, tunabaki na doctrines zile zile za mapokeo
View attachment 400948