Wahanga wa ajira za ualimu

Wahanga wa ajira za ualimu

GIPAMA

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2016
Posts
1,103
Reaction score
543
*UMOJA WA VIJANA WANAOSUBIRIA AJIRA (UVITA)*

Tumekuwa tukidharaulika sana mitaani kwa kukosa *ajira* lakini pia kwa kuswema vibaya kuwa sisi ni wazembe kwanini hatujishughulishi na mambo mengi ya kujipatia kipato hadi tuanze kulalamika lalamika kudai ajira.

Nataka niwakumbushe kuwa sisi tulimaliza mwaka *2015* kuanzia mwezi wa tano (may )hadi mwezi wa nane ( august . Kuanzia mwezi November hadi January ndio tulikuwa tunamaliza graduation kwa kila chuo.

Kwa hiyo tulianza harakati za kutafuta temple na kazi ndogo ndogo hasahasa kuanzia mwezi January. lakini kabla hatujakaa sawa tukapata kauli kutoka kwa naibu waziri tamisemi ndugu *Selemani Jafo* kuwa ajira zingetoka mapema sana mwaka huu. (wenye nia ya kufuga waliacha , wenye nia ya kulima waliacha, waliokumbana na mikataba walikataa ) kutokana na kauli ya Naibu waziri.

Kuanzia hapo tukambana na matamko mengi kitu ambacho sio tu kilitufanya kusite kuanzisha miradi lakini pia kilitupa hasara kwa mfano (akiwa bungeni waziri *Simbachawene* alisema ajira zitatoka mwezi mei) vijana walikopa nauli kwenda kufuata vyeti , sehemu mbalimbali ,wengine wachache waliobahatika kupata mkataba wa muda mfupi walisitisha mikataba *Mimi binafsi niliuza shamba langu* kwa lengo la kufuata vyeti vyangu ili kujiandaa. kwa masikitiko makubwa kabisa ajira hazikutoka ,wengi tulikata tamaa tuliingia kwenye madeni ,tulipata mkanganyiko wa mawazo na wengine walikosa vibarua.

lakini wakati tunasema ngoja sasa tuanze kufiriki kwa upande wa pili ,Mh rais anatuambia tusubiri baada ya mwezi mmoja au miwili (ni vigumu kuingia mkataba private wakati Rais kakuambia usubiri miezi miwili ). lakini cha ajabu miezi miwili hiyo imepita na hakuna lolote kiukweli tumesikitishwa sana na ahadi hewa ,tumedhalilishwa kisaikolojia , Mimi sasa nina vidonda vya tumbo , mana shamba langu niliunza.

sasa *UVITA* inataka kujua mambo yafuatayo :-

1. *Je ajira za walimu mwa huu zipo au hazipo.*

2. *Kama zipo, Ni lini ajira hizo zitatangazwa?*

3. *Kama hazipo UVITA tunataka tupewe taarifa mapema (wiki hii) ili kuondekana na high depression tuliyokuwa nayo*

Sio kwamba sisi walimu ni wajinga sana hapana ila tumelelewa katika misingi ya *kizalendo* *hatulilii ajira tunalilia kwenda kumsaidia mtoto wa maskini*. Jua kwamba kuna walimu walikaa zaidi ya miezi mitatu hawakupata mishahara ila kwa kuwa nia yao kubwa ni kumkomboa maskini waliendelea kufundisha.

Je tukiamua kuingia mikataba katika shule za private mtoto wa maskini kama mimi kule kaliua Tabora atafundishwa na nani ?

*Sasa serikali iseme tu ..kuwa mwaka huu hakuna ajira , na watoto wa maskini huku ngara watajua wenyewe*. waone kama sisi tutalalamika tena kuhusu ajira.
inasikitisha kuona uzalendo wetu ndio unatuumiza.

~MUNGU MBARIKI RAIS WETU, ILI IKIWEZEKANA ATOE TAMKO, SI KAMA TUPENDAVYO SISI, BALI NI KWA MAPENZI YAKO EE MUNGU MUUMBA WA MBINGU NA NCHI~
 
Aiseeh pole mkuu. Kuna mmoja yupo field kaomba ule wimbo wa ccm mbele kwa mbele...
 
"Msema kweli ni mpenzi wa Mungu" na msema uongo wa nani.... Sina imani nae tenaaa raisiii wawanyonge hasikilizi wanyonge....siasa kwenye mambo ya msingii ....
 
hivi wanaotaka ajira ni walimu tu!
maana kila siku utasikia ajira za ualimu zitatoka lini? kama nshu ni kuajiri walimu tu basi serikali iendelee kuuchuna tu.
Kila mtu anauliza kilicho upande wake, siwezi kuulizia za kilimo wakati mimi n mwalimu, alafu acha u.k.i.l.a.z.a..... Huo ujumbe haukuhusu wewe ila umeudandia, ungeonekana kipanga kama ungekaa kimya. Hujui tunavyoumia ww.
 
Acha kufikiria kitoto, hapa kuna great thinkers! Kama anafuta afute. Na si kila umoja ni lazima usajiliwe, UKAWA imesajiliwa wapi? mbona unaifahamu hadi wewe!?
Haya wewe unaefikiria kikubwa na kufananisha umoja wa kisiasa ambao ni temporally na umoja huo UVITA ambayo inatakiwa kuwa permanent registered sababu kila mwaka wanafunzi wanahitimu na wanapata adha kama yako kuwa ni sawa tu hakuna tofauti..jifunze kupitia chama cha walimu TZ,chama cha wafanyabiashara TZ utajua namaanisha nini
 
Acha ujuaji wewe....... Wote tunaosubili ajira (walimu) tuko upande mmoja, huo ni umoja, sidhani kama kuna asiependa kusikia tamko kuhusu ajira, alafu inaonekana ww ni mvivu wa kusoma, hujasoma habari yote.
 
Acha ujuaji wewe....... Wote tunaosubili ajira (walimu) tuko upande mmoja, huo ni umoja, sidhani kama kuna asiependa kusikia tamko kuhusu ajira, alafu inaonekana ww ni mvivu wa kusoma,
hujasoma habari yote.
Kama mko upande mmoja si mngekuja na Tamko moja kupitia vyombo vya habari na mkasikilizwa hatimae maombi yenu yakafanyiwa kazi kama vifanyavyo vyama vingine vya kutetea wafanyakazi,wanafunzi na nk
 
*UMOJA WA VIJANA WANAOSUBIRIA AJIRA (UVITA)*

Tumekuwa tukidharaulika sana mitaani kwa kukosa *ajira* lakini pia kwa kuswema vibaya kuwa sisi ni wazembe kwanini hatujishughulishi na mambo mengi ya kujipatia kipato hadi tuanze kulalamika lalamika kudai ajira.

Nataka niwakumbushe kuwa sisi tulimaliza mwaka *2015* kuanzia mwezi wa tano (may )hadi mwezi wa nane ( august . Kuanzia mwezi November hadi January ndio tulikuwa tunamaliza graduation kwa kila chuo.

Kwa hiyo tulianza harakati za kutafuta temple na kazi ndogo ndogo hasahasa kuanzia mwezi January. lakini kabla hatujakaa sawa tukapata kauli kutoka kwa naibu waziri tamisemi ndugu *Selemani Jafo* kuwa ajira zingetoka mapema sana mwaka huu. (wenye nia ya kufuga waliacha , wenye nia ya kulima waliacha, waliokumbana na mikataba walikataa ) kutokana na kauli ya Naibu waziri.

Kuanzia hapo tukambana na matamko mengi kitu ambacho sio tu kilitufanya kusite kuanzisha miradi lakini pia kilitupa hasara kwa mfano (akiwa bungeni waziri *Simbachawene* alisema ajira zitatoka mwezi mei) vijana walikopa nauli kwenda kufuata vyeti , sehemu mbalimbali ,wengine wachache waliobahatika kupata mkataba wa muda mfupi walisitisha mikataba *Mimi binafsi niliuza shamba langu* kwa lengo la kufuata vyeti vyangu ili kujiandaa. kwa masikitiko makubwa kabisa ajira hazikutoka ,wengi tulikata tamaa tuliingia kwenye madeni ,tulipata mkanganyiko wa mawazo na wengine walikosa vibarua.

lakini wakati tunasema ngoja sasa tuanze kufiriki kwa upande wa pili ,Mh rais anatuambia tusubiri baada ya mwezi mmoja au miwili (ni vigumu kuingia mkataba private wakati Rais kakuambia usubiri miezi miwili ). lakini cha ajabu miezi miwili hiyo imepita na hakuna lolote kiukweli tumesikitishwa sana na ahadi hewa ,tumedhalilishwa kisaikolojia , Mimi sasa nina vidonda vya tumbo , mana shamba langu niliunza.

sasa *UVITA* inataka kujua mambo yafuatayo :-

1. *Je ajira za walimu mwa huu zipo au hazipo.*

2. *Kama zipo, Ni lini ajira hizo zitatangazwa?*

3. *Kama hazipo UVITA tunataka tupewe taarifa mapema (wiki hii) ili kuondekana na high depression tuliyokuwa nayo*

Sio kwamba sisi walimu ni wajinga sana hapana ila tumelelewa katika misingi ya *kizalendo* *hatulilii ajira tunalilia kwenda kumsaidia mtoto wa maskini*. Jua kwamba kuna walimu walikaa zaidi ya miezi mitatu hawakupata mishahara ila kwa kuwa nia yao kubwa ni kumkomboa maskini waliendelea kufundisha.

Je tukiamua kuingia mikataba katika shule za private mtoto wa maskini kama mimi kule kaliua Tabora atafundishwa na nani ?

*Sasa serikali iseme tu ..kuwa mwaka huu hakuna ajira , na watoto wa maskini huku ngara watajua wenyewe*. waone kama sisi tutalalamika tena kuhusu ajira.
inasikitisha kuona uzalendo wetu ndio unatuumiza.

~MUNGU MBARIKI RAIS WETU, ILI IKIWEZEKANA ATOE TAMKO, SI KAMA TUPENDAVYO SISI, BALI NI KWA MAPENZI YAKO EE MUNGU MUUMBA WA MBINGU NA NCHI~
vumilia mtaajiriwa,bado tunahakiki wanafunzi waliomaliza chuo lakini ni HEWA,TUNAOGOPA TUSIJE TUKAAJIRI WAHITIMU HEWAAAAAAAAA
 
Back
Top Bottom