Wahamiaji Haramu 42 Wafia Kwenye Container Dodoma.Jee Mipaka Yetu iko Salama?

Watu 42 wahamiaji wakisomali wamepoteza maisha na kutupwa katika wilaya ya Kongwa na Kiteto na wengine 72 kunusurika kwa kukosa hewa na chakula katika usafiri waliokuwemo wakisafirishwa kwenda nchi nyingine wakiwa wamepitia mipaka ya Tanzania, Wamepetia boda ya Namanga Arusha je, Jeshi la ulinzi wa mipaka yetu liko wapi, usalama wa taifa uko wapi jamani katika hili? na mengine mengi likiwemo la watanzania 6 wanamiliki bilioni 303 huko Uswizi. Source Tbc 1
 
nyerere made TANZANIA the home of the homeless....!!! yeeees tukawa maskini kwa ajili ya kunali UTU.....! pesa na utu bora utu! UTU wa mtu una thamani kuliko uwekezaji na ubinafsishaji...!!!! IPO SIKU WANAOMBEZA HUYU BABU WATAGUNDUA. ..!!!-
 
Watu 42 raia wa Somalia wamefariki,baada ya kupakiwa kwenye kasha la kontena na kusafirishwa hadi Dodoma.Na baada ya kugundulika kwamba watu hao wamefariki baada ya kukosa hewa,ndipo wenye gari walipoamua kuzitupa maiti hizo porini!Bado nashindwa kuelewa,nini kimetokea hadi wahamiaji hao haramu kuingia bila kizuizi chochote pale Arusha?Je!huu sio udhaifu?au tukisema udhaifu ni tusi?.
 
Dodoma ndio katikati ya nchi yetu je hao watu walifikaje hapo je nchi ina ulinzi wa kutosha je hali ya ulinzi kwenye mipaka yetu ipo salama.Juzi juzi twiga wilitoroshwa leo waethiopian wanaokwa barabarani,
 
Duh!Wapo nchini kihalali au ni wahamiaji haramu?

Mkuu wageni wa Uamsho hao. Walikuwa wanaelekea Morogoro kuitembelea Radio Imaan kuona inavyofanya kazi halafu baadaye wangeonana na Sheikh Bassaleh and Ponda kabla ya kuelekea Zanzibar. Taarifa za awali za inteligensia zimeonesha hivyo.
 
TBC 1 wameonyesha maiti za wahamiaji waliokufa Dodoma ndani ya container na 72 kunusurika.Container hilo limepita mpakani Namanga na maeneo mengi bila kujulikana,jee nchi yetu iko salama kiasi gani kama vitu vinaweza kupita mpaka kati ya nchi bila kujulikana?
 
I am sending them my utmost condolences. May their soal rest in peace. Mi nashangaa vyombo vya dola vikiwakamata wanawatupa rumande na kuwarudisha nchini kwao kwenye vita na njaa kali. Embu watanzania just imagine hali wanayopitia wao ingekua hapa kwetu then unafanikiwa kukimbia kwenda nchi jirani nao wanakukamata na kukurudisha hapa. Ungejisikiaje? Tuwatafutie hifadhi na kuwasaidia kijamii.

Hapo kwenye red, think loud Mkuu. Hao mafia sio wa kuwatakia hiyo kitu mkuu. Think twice.
 
Naona walikuwa wakija kuhudhuria bunge la bajeti ila tu ni bahati mbaya. Poleni sana
 
Acha ujinga Marekani inahusika nini na mgogoro wa Somalia? unajua kiini chake au unaongea tu? watu wako dini moja na ni jamii moja yenye kuongea lugha moja lakini hawaelewani kwa sababu ya dhuluma za wao kwa wao. Somalia toka ipate uhuru mwaka 1960 ukoo wa Merhani ambao wako karibu na Majahitani na Daroodi ndio wamekuwa wakitawala na wenye mamlaka makubwa dhidi ya Jamii ya Hawiye ambao ndio wengi ikabidi kushika mtutu wa bunduki kudai mkate wa taifa ugawiwe kwa usawa huku wakiongozwa na Jenerali Fara Ididi na kuipindua serikali ya Jenerali Siad Bare wa ukoo wa Merhani.Sasa unaposema Marekani inasabisha mateso ya wasomali kivipi wakati nchi yenyewe ni fukara haina mafuta wala madini na isitoshe sio strategic area kuwa muhimu kwa Marekani kama Marekani iliitaka Somalia kwa sababu za kiuchumi tutoe hoja kiutalaamu zaidi sio kidini.
Huyo jamaa inawezakuwa ni mbumbumbu kabisa ama amejichanganya kutokana na kinachofata Merhani na Marekani
 
Ni habari ya kusikitisha sana. Mungu awapumzishe salama waliofariki.
Ninashangaa tunavyotoa kejeli kwa roho za binadamu wenzetu. Hakuna mtu anayetaka kuihama nchi yake, wanaofanya hivyo ni kwa sababu wamekata tamaa ya maisha, na msidhani wamesafirishwa bure, bila shaka kuna walio na wanaotajirika kwa biashara hiyo.

Huwezi kujua uchungu na mashaka ya ukimbizi mpaka yakufike au yamfike mtu wako wa karibu. Ninawaombeeni Mungu nyinyi mnaotoa kejeli yasiwafikeni hayo.
 
1. Wasomali walifikaje Dodoma kwa wingi huo?
2. Je walifika wakiwa hai au wafu?
3. NI nani huyo kawatelekeza Dodoma?
4. Ilikuaje mpaka kifo cha Msomali wa 50 kutokea?
5. Sasa kitu gani kinaendelea hadi sasa?



Nina hofu sana mipaka ya Nchi yetu haina ulinzi wote hata ya mbwa wa kubweka!

UDHAIFU WA SERIKALI TAWALA!
 

Mkuu wageni wa Uamsho hao. Walikuwa wanaelekea Morogoro kuitembelea Radio Imaan kuona inavyofanya kazi halafu baadaye wangeonana na Sheikh Bassaleh and Ponda kabla ya kuelekea Zanzibar. Taarifa za awali za inteligensia zimeonesha hivyo.

Mkuu wakati mwingine basi jitaidi kuficha upambavu wako nyie ndio mnatuchafulia JF...unakejeli mpaka maiti halafu ndio unajitapa humu JF eti msomi.
 
usalama wanafuatilia magazeti yamekiandikeje chama chetu,
udhaifu udhaifu udhaifu tu.
tuombe tusiwachokeze al shabab maana kwa udhaifu huu wtalipua hata jengo la bunge katikati ya nchi.
kama watu wanpita vipi silaha,vipi madawa ya kulevya,vipi dawa bandia,vipi wizi wa wanyama pori.
mawazo yangu viongozi ifike sehemu kukubali kuachia madaraka kwa manufaa ya Nchi.
Kushindwa kuwajibika ni kuhatarisha usalama wa nchi.
nadiriki kusema elimu walionayo usalama ni hii ya kuangalia nilichoandika.lakini kazi walionayo ni zaidi ya kifo katika kutafuta habari.kumetoka wapi kuaminiana katika suala la usalama wa nchi.
Haya kwa madAKITA KAMENUKA NA MAMBO YA NDANI KAMENUKA KAZI UNAYO:
CHONDE KODI ZETU USIZIUNDIE TUME:GARI ILIKUWA NA DOCUMENT GANI;ILIGONGWA MHURI WAPI; MMILIKI NI NANI;BARABARA ILIKOPITA WAVUE VYEO WOTE HARAFU WATUSAIDIE WAKITOKE LUPANGO
 
TBC 1 wameonyesha maiti za wahamiaji waliokufa Dodoma ndani ya container na 72 kunusurika.Container hilo limepita mpakani Namanga na maeneo mengi bila kujulikana,jee nchi yetu iko salama kiasi gani kama vitu vinaweza kupita mpaka kati ya nchi bila kujulikana?


Ilikuwa inapigwa dua kisha polisi hawalioni gari
 
Inaelekea hii ni biashara yenye kipato kikubwa miongoni mwa watu wanaohusika.
 
Hii ni habari ya kusikitisha sana, Waafrika 42 wanakufa katika nchi yenu? wanashindwa kupita kwa usalama na amani mpaka wanaogopa wanajificha kwenye makontena?

Jamani hii hali ni mbaya na inasikitisha sana, hawa wanakimbia shida, dhiki na njaa waliokuwa nayo kwao, leo hii ardhi ya Mwenyeezi Mungu tunaona kama ni mali yetu?

Kwanza ni kosa kabisa kuwaita "wahamiaji haramu", hao ni wakimbizi wa kiuchumi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom