Wahamiaji Haramu 42 Wafia Kwenye Container Dodoma.Jee Mipaka Yetu iko Salama?

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,971
1,650
Asubuhi ya leo maiti 43 zimetelekezwa ktk kijiji cha Chitego mkoani Dodoma, na wengine 27 hali zao mbaya. Dereva alokuwa akiwasafiri amewatelekeza baada ya kuona wanazidi kufa kabla ya kuwafikisha walikokuwa wakienda.

Wahanga hao wanadai dereva aliwaambia washuke ili atengeneze gari, mara baada ya wasomali wote kushuka dereva akawaacha maiti 44 na wengine 70 wakiwa hai. Wasomali hao wamedai kuwa kuna wenzao wengine walikuwa wakiwatupa njiani walipohisi wamekufa.

Hili linathibitishwa na ukweli kuwa wasomali wengine 2 waliokotwa kijiji cha jirani cha Zajilwa wakiwa hawajiwezi. Walipohojiwa na polisi wamfai walitoka Somalia mwezi Machi.
 
dah hamna watoto wa kike niwape hifadhi maana dah hawa wanahangaika hivuo kutafuta amani ati ..nasi tumejaliwa
 
Natamani kuliaaaaa, nguvu sna, hawa waislamy wenzangu wanapata tabu bila sababu!!! Chanzo ni marekani huyuuuuu ......
 
Hii hbr inasikitisha jamani!

Hawa ndg zetu Wasomalia wako hali mbaya sana!

Hii ni njaa tu ama ni hii vita isiyoisha kule kwao ndio inawakimbiza!
 
kwa nn somalia haitawaliki?na hzi harakati za kiislam mwisho wake nn na nn lengo lake?wanatia huruma sana wasomali hata ukiangalia kwenye tv....
 
Too sad!Mungu awapumzishe salama waliotangulia na awape afya njema walio mahututi!Lakini huwa najiuliza kila siku,usalama mipaka ya Tanzania ukoje mbona kila siku wanakamatwa hawa wahamiaji haramu wakiwa tayari wapo ndani ya Tanzania badala ya mipakani?
 
1. Wasomali walifikaje Dodoma kwa wingi huo?
2. Je walifika wakiwa hai au wafu?
3. NI nani huyo kawatelekeza Dodoma?
4. Ilikuaje mpaka kifo cha Msomali wa 50 kutokea?
5. Sasa kitu gani kinaendelea hadi sasa?
 
I am sending them my utmost condolences. May their soal rest in peace. Mi nashangaa vyombo vya dola vikiwakamata wanawatupa rumande na kuwarudisha nchini kwao kwenye vita na njaa kali. Embu watanzania just imagine hali wanayopitia wao ingekua hapa kwetu then unafanikiwa kukimbia kwenda nchi jirani nao wanakukamata na kukurudisha hapa. Ungejisikiaje? Tuwatafutie hifadhi na kuwasaidia kijamii.
 
Natamani kuliaaaaa, nguvu sna, hawa waislamy wenzangu wanapata tabu bila sababu!!! Chanzo ni marekani huyuuuuu ......

Acha ujinga Marekani inahusika nini na mgogoro wa Somalia? unajua kiini chake au unaongea tu? watu wako dini moja na ni jamii moja yenye kuongea lugha moja lakini hawaelewani kwa sababu ya dhuluma za wao kwa wao. Somalia toka ipate uhuru mwaka 1960 ukoo wa Merhani ambao wako karibu na Majahitani na Daroodi ndio wamekuwa wakitawala na wenye mamlaka makubwa dhidi ya Jamii ya Hawiye ambao ndio wengi ikabidi kushika mtutu wa bunduki kudai mkate wa taifa ugawiwe kwa usawa huku wakiongozwa na Jenerali Fara Ididi na kuipindua serikali ya Jenerali Siad Bare wa ukoo wa Merhani.

Sasa unaposema Marekani inasabisha mateso ya wasomali kivipi wakati nchi yenyewe ni fukara haina mafuta wala madini na isitoshe sio strategic area kuwa muhimu kwa Marekani kama Marekani iliitaka Somalia kwa sababu za kiuchumi tutoe hoja kiutalaamu zaidi sio kidini.
 
Na hali ikiendelea Tanzania kama ilivyo Siku moja usishangae unakimbia nchi yako kama wasomali? Hii nchi inakaribisha kila mtu eti ni mwekezaji na akija ana dispose wanakijiji out of their natural resources endowment soils bila hata fidia halafu unategemea nini? So sad, rest in peace victims!1
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom