Wahamiaji haramu 40 wakamatwa jijini Dodoma

Wahamiaji haramu 40 wakamatwa jijini Dodoma

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,622
Reaction score
8,427
Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma linawashikilia wahamiaji haramu 40 raia wa nchini Ethiopia waliokamatwa katika barabara kuu ya Dodoma Arusha katika kijiji cha Kuhi kata ya Bereko wilayani Kondoa mkoani Dodoma wakiwa wamepakiwa kwenye gari aina ya Scania huku wakifungiwa kwenye Kontena la mizigo wakiwachanganya na shehena ya bidhaa wanazosafirisha kutoka Namanga Arusha hadi Mbeya.

Akizungumza mara baada ya kukamatwa wahamiaji hao, kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Gilles Muroto amesema mbali na wahamiaji hao pia wamekamata wasafirishaji ambao ni watanzania waliokuwa wakisafirisha wahamiaji hao ambapo amesema jeshi hilo limejipanga katika kudhibiti vitendo vya uhalifu makao makuu ya nchi.

Kwa upande wake naibu kamishna wa uhamiaji mkoa wa Dodoma Peter Kundy amewataka wananchi kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa za uwepo wa wahalifu nchini na kuacha kuwaficha wahalifu hao ambapo amesema biashara ya uhamiaji ni biashara haramu.

Aidha katika hatua nyingine kamanda Muroto amesema jeshi la polisi mkoa wa Dodoma limeendesha misako mbalimbali na kukamata jumla ya watuhumiwa 20 wa makosa mbalimbali ya kiuhalifu ikiwemo watuhumiwa waliokamatwa kwa kosa la kuiba fedha kwa njia ya mtandao na kosa la matumizi ya fedha bandia.

Chanzo: ITV
 
Hao ndio kwao ni Mabingwa wa:

1. STANDARD GAUGE ( ELECTRIC TRAIN )

2. SHIRIKA LA NDEGE ( ETHIOPIA AIRLINES )

3. UMEME WA UHAKIKA

- Hao kwao kuna vitu SERIOUS, siyo kama kwetu MIRADI ZEE LA VI-WONDER LINAANZIA KWA AJILI YA UPIGAJI.

Sasa TWAFAAAAAAAAAA
 
HAWA JAMAAA WANA NYUMBA MBAGALA ZAKHEM HIZI.NYUMBA ZIKO.CHINI YA WAPALESTINA ...WAH HAO WAKIPITILIZA WANACHOFANYA WAKIFIKA SEHEMU WANALALA MPAKA USIKU WANAELEKEA MBAGALA..HAPO HUTENGENEZEWA VIBALI VYA SAFARI KWENSA KUFANYA KAZI NJE ...NA WAPALESTINA HULIPWA HELA NYINGI SANA NAAMINI OFISI ZA POLISI ZINAWAJUA AWAJAMA N CHAIN NDEFU SANA
 
Back
Top Bottom