Wahadhiri Wanne Wafukuzwa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania!

Mzee sio utani,

Haya mambo "huria" na "Ubinafsi" tulipaswa kwanza tujifunze kwa wale waliotutaka tufanye. Wenzetu walioendelea wana mfumo mzuri wa kudhibiti ujinga kama huu.

Hivi unategemea nini kama Mhadhiri wa chuo kikuu huria anaishi maisha huria, mhadhiri kasoma kiujanja, ujanja tu kwa kuiba mitihani na kudesa!.

Huyo hawezi kuacha tabia yake. Vigezo vinavyotumika katika vyuo vyetu kupata wahadhiri ni "just awe" na Upper second na tofauti na walimu wa kawaida wanavyuo vya ualimu, wanajifunza pia maadili ya kazi na jinsi ya kufundisha.

Hizi digrii za "chupi" na "rushwa" siku hizi zimeua kabsaaa taaluma.

Nimewahi kufanya kazi na jamaa ana "first class" ya chuo kimoja binafsi (...) lakini mkichwa ni "o" kabisa, anaangalizia mpaka kuandika barua ya kiofisi. Hawezi kujieleza kwa kingereza wala kiswahili, kujibu hoja kwenye jalada hatakutafuta kokote ulipo hata kama umesafiri atasubiri mpaka hurudi.

hapo ndipo tulipofikishwa na mfumo usioleweka wa elimu yetu!!! enrollment uchwara mtupu, lecturers uchwara tu, degree uchwara matokeo yake ndo haya. Vyuo vinapotezA hadhi.

tunapenda njia fupi sie duh!! hata pasipostahili.
 
Ni aibu sanaaa! mwaka jana zilipatikana scholarship nyingi za kwenda kusoma Ubelgiji lakini baada ya kyfatilia ikaonekana asilimia kubwa ya walipata walipeleka vyeti vya kufoji!! wakatupiliwa mbali na sasa wanafanya hali ya kupata hata kwa wanaostahili kuwa ngumu zaidi, Tunaelekea kubaya saaaana.

Ndo huu mfumo wetu wa kuleana. usikute walikuwa watoto wa vigogo sasa kuwaadhibu anakuwa mzigo mkubwa!! Kama wamefoji mbona hawafikishwi kwenye vyombo vya sheria?
 
Haya mambo ni ya kuzima kwa nguvu zote. Naamini siyo Open University tu yanafanyika. Hata vyuo vingine. Niliwahi kuona mwanafunzi fulani anahangaishwa pale UD kwenye Faculty ya Political Science/Sociology, nikaishiwa nguvu kabisa. Walionyesha arrogance ya hali ya juu kwa mwanafunzi ambaye nilimuonea huruma sana maana alikuwa hana msaada wa aina yoyote.
Ndivyo walimu wengi walivyo
 
Huu mtindo wa kufanyiwa assignments hata kwa wenzetu Ulaya upo ijapokuwa kwa kiwango kidogo.

Siku moja niliona programme kwenye BBC wakizungumzia kuhusu hilo. Wanfunzi walikuwa wanadownload assignments at a fee kutoka websites fulani halafu wanazipeleka kwa masahihisho. Walikuja kugundua assignments nyengine zilikuwa ni za aina moja ndio wakashtuka na hilo dili.

Sasa tujitahidi tu lakini ni shida sana kuzuia vitu hivi kwa miaka hii ambayo cheating imehalalishwa.
 
MAsikini Juma Kanuwa kweli he was a very cool person but anyway ndio maisha kaka usife moyo kama kweli umeshiriki katika hili jirekebishe na uanze upya.
 
hahaaa wewe ngoshwe!!!

Pesa msema kweli!!!! Unanunua madesa vichwa mpaka na grades!!!

Uko wapi ubora wa elimu sasa?????????? Na hii na imani si open uni tu hata vyuo vingine itakuwepo.

Wat a dirty game!!!!!!!!!

biblia iko wazi

pesa ni jawabu la moyo

sasa kama moyo wao wahadhiri ulikuwa unatamani jawabu mlitaka wakaibe epa????
Vyuo vyote tanzania ni uchafu mtupu

udsm inaongoza kwa ngono

out inaongoza kwa kuhonga

tumain inaongoza kwa wanafunzi feki

mzumbe=nchimbea a.k.a dk hilo sisemi

yupi ana afadhali asie na kosa achukue jiwe awapige;so kama umepita kote uko usinyooshe mdomo;songa mbele
 
haya mambo ni ya kuzima kwa nguvu zote. Naamini siyo open university tu yanafanyika. Hata vyuo vingine. Niliwahi kuona mwanafunzi fulani anahangaishwa pale ud kwenye faculty ya political science/sociology, nikaishiwa nguvu kabisa. Walionyesha arrogance ya hali ya juu kwa mwanafunzi ambaye nilimuonea huruma sana maana alikuwa hana msaada wa aina yoyote.
Ndivyo walimu wengi walivyo

heshima mkuu kila chuo kina matatizo yake kama si kuonga ngono basi pesa;vyote;mi nasema nikifika huo itabidi nianzishe changu najisahihishia mwenyewe dk mwenyewe prof mwenyewe
 
Mkuu mshangao wako ni kama vile ndo kwanza unajua hapa kuwa hizo fojari za dizaini hiyo zipo!!!!!!!!

Ur right, lakini haya mambo yanakatisha tamaa, tutafika tu anyway!
 
Hili linazidi kufanya watu waogope kusema kuwa wamesoma degree zao hapa Tanzania!

shule zenyewe za kata

ukifika chuo kikuu ndo ivo tena!

dah
 
Back
Top Bottom