Wahadhiri Wanne Wafukuzwa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wahadhiri Wanne Wafukuzwa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Buchanan, Jan 12, 2010.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Jan 12, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Imeandikwa na Gloria Tesha.

  CHUO Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), kimewafukuza kazi wahadhiri wanne, mfanyakazi mmoja, na kimefuta matokeo ya wanafunzi 20 baada ya kubainika kuwa walifanya udanganyifu katika matokeo ya mitihani.

  Wanafunzi wengine 71 wapo hatarini kufutiwa matokeo endapo mpaka kesho hawatajitokeza kwenye kamati maalum iliyoundwa kuchunguza kadhia hiyo ya udanganyifu wa matokeo iliyoibuka miezi takribani minne iliyopita na gazeti hili kuwa la kwanza kuitangaza kwa umma.

  Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Tolly Mbwette aliwaeleza waandishi wa habari jana Dar es Salaam, kuwa uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha Baraza la Seneti kilichokaa Ijumaa iliyopita na kikao cha jana cha Baraza la Chuo, kilichohitimisha suala hilo lililochunguzwa chini ya mfumo wa Student Academic Recording System (SARS).

  Aliwataja wahadhiri waliofukuzwa na nafasi zao katika mabano ni Saimon Kitila (Mhadhiri Msaidizi, Kitivo cha Uongozi na Biashara); Jovin Mwehozi (Mhadhiri Msaidizi, Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii); Juma Kanuwa (Mhadhiri Msaidizi, Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii) na Jamal Mwasha (Mkufunzi Msaidizi, Kitivo cha Sheria).

  Mtumishi mwingine aliyefukuzwa kazi ni Richard Ngwalida, ambaye ni mtaalamu wa kompyuta ambaye amedaiwa alipokea hongo na kumsaidia mwanafunzi kujaribu kughushi matokeo.

  Hata hivyo, Profesa Mbwette hakuwa tayari kueleza ni hongo ya kiasi gani na hatua zilizochukuliwa kwa mtoa hongo.

  Kuhusu wahadhiri hao, Mbwette alisema, "Uchunguzi uliofanywa na kamati maalumu iliyoundwa na chuo kuchunguza suala hilo, ulibaini kuwa walihusika kughushi matokeo ya wanafunzi kwa kuyaingiza katika vitivo mbalimbali

  bila idhini na huku ni kughushi na ni kosa, Baraza la Chuo halikupendezwa na suala hili na hatupo tayari kuvumilia haya."

  Akifafanua kuhusu wanafunzi, Profesa Mbwette alisema uchunguzi wa chuo ulioanza Oktoba mwaka jana, uliwezesha kuandikiwa barua wanafunzi 278 kutoka ofisi ya Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Taaluma ikiwataka wafike katika kamati maalumu ya Baraza la Seneti kuhojiwa kuhusu tuhuma hizo, ambapo 207 waliitikia mwito.

  "Kati ya hao 207 waliofika, mpaka Januari 8, mwaka huu, wanafunzi 120 walishajieleza na kuonekana hawana makosa yoyote, 31 vitivo vyao vimeagizwa vihakikishe takwimu za matokeo yao kwa upya, 36 takwimu tuna mashaka nazo na vitivo vyao vinachunguza ambapo Baraza la Seneti la Februari mwaka huu, litatoa uamuzi dhidi yao, lakini 20 tumewafutia matokeo na 71 tumewapa muda, wasipotokea mpaka keshokutwa (kesho) tunajua wamejifuta wenyewe," alisema Makamu Mkuu wa OUT.

  Katika hatua nyingine, wanafunzi 50 ambao majina yao hayakuwemo katika orodha ya wahitimu mwaka jana kutokana na uzembe wa chuo, watashiriki mahafali ya mwaka huu na kwa mujibu wa Profesa Mbwette, matokeo yao watapewa wakati wowote kuanzia sasa ili wayatumie katika kazi na ajira zao.

  Oktoba mwaka jana, uongozi wa OUT ulibainisha kuhusu kuwepo kwa wanafunzi wanaotuhumiwa kufanya udanganyifu katika matokeo ya mitihani, ambapo gazeti hili pia lilibaini kuhusu wahadhiri hao wanne kuhusika pia katika sakata hilo.

  Pamoja na mambo mengine, Profesa Mbwette amevishauri vyuo vingine kufanya uchunguzi kama huo ili kulinda hadhi ya elimu nchini.

  SOURCE: http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=5205
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Jan 12, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Wapelekwe kortini kwa kudhalilisha taaluma na ubunifu. Hizi chunguzi zisiishie hapo.
   
 3. October

  October JF-Expert Member

  #3
  Jan 12, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwa mwendo huu tutafika kweli?
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Jan 12, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Haya mambo ni mazito ndugu!
   
 5. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #5
  Jan 12, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyo juma kanuwa namfahamu personally, anaonekana kijana mzuri, mtulivu na anayejiheshimu. nimesikitika sana kwa utou wa maadili aliofanya.
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Jan 12, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Simba mpole ndo mla nyama ati. Si unajua wahenga tena, na huwa hawakosei.
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Jan 12, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Huyu dogo wa Kitivo cha Sheria namfahamu, sikujua kama naye ana vijimambo!
   
 8. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #8
  Jan 12, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli mkuu nimeamini!!!!!!!!!!
   
 9. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #9
  Jan 12, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Lakini system nzima ya chuo nafikiri ni ya kulaumiwa. Unajua unapokuwa unaweka fedha zako nyingi katika sehemu ambazo zinaonekana unaleta ushawishi wa kuziiba hata kama mtu hakuwa na nia ya kufanya wizi. Kwa upande wa OUT systems ziko loose mno, Just imagine wanafunzi hawaonyeshi vitambulisho vyao wakati wanaingia kwenye mitihani. Assignments nasikia kuna watu waliunda timu za kusolve assignments za wanafunzi wa OUT, wewe ni kupeleka mshiko wako tu na maswali, unajiondokea na kurudi baada ya maswali kufanywa na timu hiyo unayachukua na kwenda kukusanya. Kwa upande wa kuingiza matokeo kwenye kompyuta ni kwamba system haikuwa tight enough kiasi kwamba mtu anaweza kuhonga ili atengenezewe matokeo yawe "mazuri." Sasa naona asilaumiwe mwizi tu, bali hata aliyemfanya mtu kuiba naye alaumiwe!
   
 10. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #10
  Jan 12, 2010
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  Open chuo chote kinabidi kisafishwe,kuanzia ma TA paka VC.kinamapungufu mengi sana.....hususan watu kufanyiwa assignments na UEz.
   
 11. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #11
  Jan 12, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Sure!
   
 12. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #12
  Jan 12, 2010
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  1. Kuingia kufanya mitihani wanacheki vitambulisho (walau nilishaona ikifanyika Temeke Regional Centre), teketi ya mtihani (au test) na picha ya mhusika.

  2. Kuhusu 'assignments' ni kweli. Kuna wanafunzi (hasa wale wenye hela) hawataki usumbufu na wanawashawishi wengine ili 'assignments' zao zifanywe na 'teacher' na 'teachers' wenye njaa hawakatai.

  3. Ni kweli 'system' nzima na 'functining' ya OUT haijakaa sawa. Bado kuna 'loopholes' nyingi sana! Nashangaa kwa nini Prof Mbwette na wakuu wengine wasiende kujifunza kutoka vyuo vingine vyenye programu za 'Distance Learning' kama London University na kuona wao wanafanyaje.

  4. OPEN inatakiwa ifanyiwe marekebisho mengi sana na pia staff wajifunze customer care na siyo kufanya kazi kama wamelazimishwa (kwa kununa na kutotaka kuwaelekeza wanafunzi/wateja vizuri)!
   
 13. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #13
  Jan 12, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  1. Huko kuonyesha vitambulisho na picha sio kila sehemu na kama kuna sehemu wanaonyesha vitambulisho lwakati wanaingia kwenye papwe abda hiyo system imeanza hivi karibuni, hasa baada ya wanafunzi kuanza kucheat.
  2. Kuhusu customer care, kwa kweli hawa watu customer care yao ni very poor, utafikiri wamelazimishwa kufanya kazi, wamenuna utafikiri kuna mashindano ya kununa!
   
 14. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #14
  Jan 12, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Chuo chenyewe kinaitwa "Open Uni" unategemea nini kama mambo sio "Open"??
   
 15. bht

  bht JF-Expert Member

  #15
  Jan 12, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  hahaaa wewe ngoshwe!!!

  pesa msema kweli!!!! unanunua madesa vichwa mpaka na grades!!!

  uko wapi ubora wa elimu sasa?????????? na hii na imani si open uni tu hata vyuo vingine itakuwepo.

  wat a dirty game!!!!!!!!!
   
 16. kkakuona

  kkakuona Member

  #16
  Jan 12, 2010
  Joined: Jan 12, 2010
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Hii ni serious issue. waneweza kujifunza toka Sweden pia kuna vyou vinatoa programme kama hizo lakini wana control system kuona kuwa mtu anastahili kupata hicho cheti. mfano BTH, LTU (LuleƄ).
  Na la kufanyiwa assignment nishalisikia hata mlimani especially kwa programme za MBA. Watu wanafanyiwa hadi thesis. Kazi ipo kwa Tanzania.
   
 17. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #17
  Jan 12, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Nchi hii kuna eneo ambalo kuna control system ambayo ni tight?
   
 18. m

  madule Senior Member

  #18
  Jan 12, 2010
  Joined: Aug 22, 2009
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni aibu sanaaa! mwaka jana zilipatikana scholarship nyingi za kwenda kusoma Ubelgiji lakini baada ya kyfatilia ikaonekana asilimia kubwa ya walipata walipeleka vyeti vya kufoji!! wakatupiliwa mbali na sasa wanafanya hali ya kupata hata kwa wanaostahili kuwa ngumu zaidi, Tunaelekea kubaya saaaana.
   
 19. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #19
  Jan 12, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Whaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaat?
   
 20. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #20
  Jan 12, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mzee sio utani,

  Haya mambo "huria" na "Ubinafsi" tulipaswa kwanza tujifunze kwa wale waliotutaka tufanye. Wenzetu walioendelea wana mfumo mzuri wa kudhibiti ujinga kama huu.

  Hivi unategemea nini kama Mhadhiri wa chuo kikuu huria anaishi maisha huria, mhadhiri kasoma kiujanja, ujanja tu kwa kuiba mitihani na kudesa!.

  Huyo hawezi kuacha tabia yake. Vigezo vinavyotumika katika vyuo vyetu kupata wahadhiri ni "just awe" na "Upper second" nzuri au "1st Class" Hilo sio shida kwa sasa kwenye mfumo wa elimu huria na ya kununua. Hii ni tofauti na walimu wa kawaida wanavyuo vya ualimu, wanajifunza pia maadili ya kazi na jinsi ya kufundisha.

  Hizi digrii za "chupi" na "rushwa" siku hizi zimeua kabsaaa taaluma.

  Nimewahi kufanya kazi na jamaa ana "first class" ya chuo kimoja binafsi (...) tuliajiriwa siku moja, masikini jamaa mkichwa alikuwa ni "o" kabsaaa, anaangalizia mpaka kuandika barua ya kiofisi (mimi na "ka lower 2nd" kangu tu). Jaama alikuwa hawezi kujieleza kwa kingereza wala kiswahili, kujibu hoja kwenye jalada atakutafuta kokote ulipo hata kama umesafiri atasubiri mpaka urudi, huyo jamaa sasa ni mhadhiri katika chuo fulani! kudadadeki, unategemea nini hapo??

  Zamani nilijua ni product ya vyuo binafsi tu vinavyofanya biashara, hivyo havisiti kutoa "first class" za kumwaga ili kuvutia wateja, kumbe sasa hata vile vya umma vimeingia kwenye wimbi la udanganyifu mkubwa!.Nilipata kusikia tatizo hilo la kugawana digrii "kufanya biashara ya mabadilishano ya "digrii na sehemu za siri" au "digrii na fedha" katika chuo kimoja cha umma kule Morogoro....Baada ya kuwauliza waliosoma hapo, walithibitisha kuwa ni jambo la kawaida tu kwa sababu wahadhiri wengi ni vijana wanafundisha "part time" na wananatafuta maisha "chap chap" .......
   
Loading...