Wahadhiri wamekuwa kimya wakati wa saga za wenzao, naamini nao pia wataunganisha nguvu na jamii nzima ili kuunganisha nguvu.
Mheshimiwa nashukuru kwa kutambua umuhimu wa Wahadhiri japokuwa nitofautiane nawe kuhusiana na sualala ukimya la wahadhiri (wa Tanzania). Ukiona nchi ambayo Wahadhiri wa vyuo vya umma wanamigogoro ya kimaslahi na Serikali basi ujue nchi husika ina matatizo ya kisiasa au imejaa wanasiasa wasiojua mambo muhimu ili Taifa liendelee!
Nina hakika utakubaliana nami kwamba hakuna mfumo wa maisha ya kijamii, kisiasa au kiuchumi ambao hauhitaji kufanyiwa utafiti wa mara kwa mara kwa maendeleo endelevu. Ni wazi kwamba wanasiasa (ambao tumewapa kipaumbele kimaslahi) hawawezi kufanya utafiti au/na kutoa maamuzi ya kuisaidia nchi bila kufanya utafiti! Haiwezekana, hata kama unaongoza vichaa, kuendesha maisha ya watu pasipo kuweka miongozo ya kupambanua dira inayokuwezesha kutimiza majukumu yako kwa ustawi endelevu. Swali ni kwamba utawezaje kupambanua mambo kama huna hata 'statistics' za masuala muhimu yanayohusu jamii na uchumi? Hebu jiulize maswala yafuatayo:
- ninyi kama Wabunge mnapata wapi takwimu za kuongea 'facts' mnapokuwa Bungeni iwapo kitengo kama
NBS kimechoka na wala hakina 'fund even to outsource researches to keep it up to date'?
- kama NBS imechoka na wahadhiri wanalalamika ninyi mnapata wapi 'guts' za kukaa na kuongea Bungeni ilhali mkijua 'no facts no talk'?
- ain't you, 'in normal sense', gluttonously milking poverty-stricken citizens of URT maana mnachoongea hakina tija kwa ustawi wao?
Swala la wahadhiri kuongea kuhusu "saga za wenzao" sijui unamaanisha nini!!? Lakini, jukumu la kuwafanya wahadhiri waongee mnalo ninyi wanasiasa wa Tanzania hasa ukizingatia kwamba mmejipa nguvu kukiwezesha chombo mnachoona kinafaa. Awali mliamua TRA iwe na nguvu ili isimamie kodi zitazowezesha upatikana wa 'allowances' zenu, tumeona jinsi ilivyofanikiwa. Mkaamua Jeshi liwe na maslahi mazuri kusudi kulinda mkate wenu; uwezi kusikia minong'ono Jeshini tena labda aje mwanasiasa mwendawazimu. Sasa nitajie mahala pengine zaidi ya Bunge ambapo unadhani watumishi wake wanafanya kazi pasipo mkwamo na msuguano wa kimaisha hapa Tanzania?!
Mnatakiwa kuyaongea haya huko Bungeni maana linawafanya hata ninyi muonekane malofa.