Hii ni hatari sana na watu wengi wanakaa nyumbani bila matibabu.
Dar es Salaam. Baadhi ya vitengo vya UKIMWI, TB na selimundu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili vilivyokuwa vikisimamiwa na miradi ya wafadhili vimemaliza mikataba yao, hivyo wagonjwa wameanza kulipia gharama za matibabu tofauti na hapo awali.
Baadhi ya wagonjwa waliokuwa wakihudhuria katika kliniki hizo wamelazimika kuanza kuchangia huduma za matibabu, huku wagonjwa wa msamaha wakilipia asilimia 10 ya gharama halisi.
Hatua hiyo imefuatia agizo la Rais John Magufuli kutaka kila mgonjwa anayefika kutibiwa katika hospitali za umma ikiwamo Muhimbili kuchangia huduma za afya ili kuhakikisha kila mgonjwa anapata dawa na huduma nyinginezo kwa gharama nafuu.
Ashura Athuman anayehudhuria kliniki ya huduma za UKIMWI amesema kwa miaka 12 sasa amekuwa akihudhuria bila kukosa, lakini tangu waanze kulipia baadhi ya wagonjwa hajawaona wakihudhuria kwa kipindi kirefu sasa.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma (MNH), Aminiel Aligaesha amesema hospitali ya Muhimbili inatekeleza agizo la Rais la kuhakikisha kila mgonjwa anayefika kutibiwa anapatiwa dawa na huduma nyingine kwa gharama nafuu.
Kutoka gazeti la mwananchi