PISTO LERO
JF-Expert Member
- Mar 8, 2011
- 2,819
- 1,455
Wanajamvi tofauti na mtu mmoja mmoja ndani ya vyama hivi vya siasa wanaoutaka uraisi kwa udi na uvumba. Wewe binafsi ungependa chamagani kichukue madaraka hapo mwaka 2015, na kwasababu zipi?
Wanajamvi tofauti na mtu mmoja mmoja ndani ya vyama hivi vya siasa wanaoutaka uraisi kwa udi na uvumba. Wewe binafsi ungependa chamagani kichukue madaraka hapo mwaka 2015, na kwasababu zipi?
Sio utabiri,ni maono. Hawa watatu ndio watakaokuwa Wagombea wa Urais wa Tanzania wenye nguvu 2015. Makwarukwaru ya kila aina yatapita vyamani mwao. Wao ndio watakaogombea. Ni hawa: 1. Dr. Wilbrod Peter Slaa- CHADEMA 2. Edward Ngoyai Lowassa-CCM 3. Prof. Ibrahim Haruna Lipumba-CUF. Ni vyema tukajielekeza kwao na kuandaa kura zetu za Oktoba 2015. Ndivyo itakavyokuwa...
Sio utabiri,ni maono.
Hawa watatu ndio watakaokuwa Wagombea wa Urais wa Tanzania wenye nguvu
2015. Makwarukwaru ya kila aina yatapita vyamani mwao. Wao ndio
watakaogombea. Ni hawa: 1. Dr. Wilbrod Peter Slaa- CHADEMA 2. Edward
Ngoyai Lowassa-CCM 3. Prof. Ibrahim Haruna Lipumba-CUF. Ni vyema
tukajielekeza kwao na kuandaa kura zetu za Oktoba 2015. Ndivyo
itakavyokuwa...
Slaa ana miaka mingapi ? Halafu amemtelekeza mkewe ,kwa ufupi hafai kuwa Raisi kutokana na tabia hio na tukio hilo.
Wewe hutaki mtu atajwe lakini unataka vyama vitajwe (na umefanya hivyo). Kwani aliyekuambia vyama pekee ni CCM, CUF, au Chadema ni nani? Kwamba ndivyo pekee vinavyostahili kupewa madaraka ya nchi hii? Nci hii ni ya kila mtanzania na kila mmoja iwe binafsi au kupitia vikundi vyao (wengine wanaviita vyama); au kwa kuungana wana haki ya kutupatia viongozi wa taifa hili. Hakuna kikundi (chama?) chenye haki au hodhi ya uongozi wa nchi yetu.
Hivyo basi, badala ya "chama gani" ningependa iwe ni "sifa gani" anazotakiwa kuwa nazo yeyote mwenye kuomba ridhaa ya kuongoza watanzania iwe anapitia vikundi, muungano wa vikundi, au binafsi. Sorry, binti yangu mdogo katumwa na mama yake - lunch tayari - nitarudi baadaye kukupatia sifa za hao watu na vikundi vyao.
Sasa angalia majimbo anayopokewa SLAA kwa wingi kwa mtazamo wako, subiri kinyume chake hiyo 2015, SLAA atalia vizuri sana kuliko alivyomlilia mtu ambaye chama chake ni chanzo cha kifo chake. Hivi kwanza MBOWE anajisikiaje kuwekwa kando na urais wa 2015? acheni kugombanisha watu jamani vibaya hivyo. Huyu ZITTO tuachane naye kisha washinda. Mnataka tena bifu ianze kati ya SLAA na MBOWE, yaani mnamfanya Mwenyekiti anakuwa kama mti wa kutupia jongoo.