Wagombea Ubunge Mbeya Mjini kupitia CCM watia Aibu

Uongo uliokithiri. Eti akichaguliwa atatafuta wafadhili? Kama anawajua wafadhili si angewatafuta kabla? Uongo wa kitoto watu wameshaijua! Watanzania sisi sio wajinga. Hii mijitu inatupigia magoti alafu inakwenda kuishia kusema ndiooooooooo kwa kila kitu huku sisi tunaumia. Mwisho wenu maccm umewadia.
 
Hao sasa wamekuwa omba omba kwa ajili ya matumbo yao na sio kuwatumikia wananchi. Kiongozi mwadilifu na alietayari kuwatumikia wananchi sio lazima kugaragara katika kuomba kura. HAO WANAOMBA KULA NA SIO KURA!!
 
Wamenichekesha sana Aise yan kura zinaombwa kwa magoti hawana jipya hawa wachumia tumboni hivi hawajui mwisho wa ccm ni October?
 
Ingekuwa mimi ndio hawa wananchi badala ya kukaa na kuwacheka ningekata fimbo na kuwatimua mbio hawa wanaoleta aibu kama hii ya kujidhalilisha mbele ya watoto wadogo, hivi kweli ndani ya nyumba uwe na mtu kama huyu eti ndiye Mkeo au mumeo utajisikiaje ukimkuta anapiga magoti au kugalagala mbele za watu eti anaomba Kura.
 
Hawa jamaa wana style nyingi..
 

Attachments

  • 1437735594866.jpg
    1437735594866.jpg
    58.7 KB · Views: 194
Back
Top Bottom