Wagombea Ubunge Mbeya Mjini kupitia CCM watia Aibu

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,739
4,732
DSC_1006.JPG

MWENYEKITI wa UVCCM mkoa wa Mbeya, Aman Kajuna, naye akipiga magoti kuomba kura

DSC_1022.JPG

MWENYEKITI wa Jumuia ya Wazazi ya CCM mkoa wa Mbeya, Fatuma Kasenga akiomba kura kwa mtindo wa kujigalagaza ardhini

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida baadhi ya Watia nia ya Ubunge katika Jimbo la Mbeya mjini kwa tiketi ya CCM wamelazimika kuomba kura kwa aina tofauti kwa wanachama wao.
Makada hao walilazimika kupiga magoti, kugalagala ardhini, kulazimisha kuulizwa maswali, ili mradi wapiga kura wawaonee huruma na kuwachagua. Hayo yalijiri wakati makada hao, wanaowania kuomba kuteuliwa na CCM wilaya ya Mbeya mjini,walipokuwa wakijinadi kwa wana-CCM wa kata ya Nsalagha,ili kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuipeperusha bendera ya CCM.

Vituko hivyo vilileta bashasha na burudani ndani ya kata hiyo, na kuwafanya baadhi ya viongozi waliokuwa meza kuu kulazimika kusimama ili kwenda kumuinua Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mkoani hapa, Fatuma Kasenga, aliyekuwa anagalagala ardhini kuomba kura Fatuma ambaye hii ni mara yake ya pili kujitokeza kuwania ateuliwe na CCM kuwania ubunge jimbo la Mbeya mjini, alisema mwaka 2010 kura zake hazikuweza kutosha hivyo kuwaomba wana-CCM wasimuangushe mwaka huu.

Aliongeza lengo la kujitokeza kuwania nafasi hiyo ni kutaka kurudisha heshima ya jimbo la Mbeya, ambayo hivi sasa imepotea baada ya jimbo hilo kuwa chini ya mbunge wa kutoka chama cha upinzani kwa miaka mitano sasa.

Fatuma ambaye alikuwa akijinadi huku akiwa amepiga magoti, ambapo mara baada ya kumaliza dakika zake tatu alizokuwa amepewa pamoja na kujibu maswali aliyoulizwa, ndipo alipoanza kugalagala huku akiomba kura kwa wana-CCM.

Hatua hiyo iliwafanya baadhi ya viongozi waliokuwa meza kuu, kulazimika kusimama na kwendakumsaidia kumuinua kasha kumsindikiza walipokuwa wamepangiwa kukaa wagombea wenzake.

Naye Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Mbeya, Aman Kajuna, alisema wakati anachaguliwa kushika nafasi hiyo mwaka 2012, alikuta asilimia kubwa ya vijana ndani ya jiji la Mbeya wakiwa wamekata tamaa na kuhamia upinzani. Kajuna alisema kazi yake ya kwanza ilikuwa ni kuwafikia vijana hao akianzia na wale wa CCM, kukaa nao na kuwauliza sababu iliyopelekea wakate tamaa na Chama, ambapo aliwaomba warudi kukitumikia na kukitetea Chama.

Mara baada ya kumaliza kujinadi kwa wana-CCM hao, Kajuna aliamua kupiga magoti na kuomba kura akiwaahidi wanachama hao kuwa anao uhakika wa asilimia nyingi kuwa anao uwezo wa kulikomboa jimbo hili, kwani ametoa misaada mingi kwa vijana, wanawake na wazee.

Kwa pande wake Mkurugenzi wa kituo cha radio Generation Fm, kilichopo jijini Mbeya, Shadrack Makombe, alisema yeye ni kijana wa viwango, hivyo kuwaomba wana-CCM wamchague ilikuipeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Makombe alisema akipewa ridhaa hiyo anao uhakika wa kulikomboa jimbo la Mbeya mjini, na baada ya kutekeleza hilo atahakikisha anatafuta wafadhiri watakaojenga viwanda ili viweze kutoa ajira kwa vijana mjini Mbeya.

11224060_1081455351881974_7547486702622040934_n.jpg
 
Hapo hakuna anayewawkilisha wanambeya na hizo style wanazotoa wakishapata wanambeya mtakoma kwa kupigiwa matope na ma vx v8 yao.
 
Cha kusikitisha na kutia aibu wananchi wanawacheka kwa dhihaka ya hali ya juu.
 
Mary Mwanjelwa hajaomba kuteuliwa kupeperusha bendera ya Mafisadi wa CCM?

Muda mrefu alionekana kulimezea sana jimbo hilo lot lililo chini ya Rais wa Mbeya Joseph Mbilinyi a.k.a "wanamwita Sugu a.k.a Mr II"

Au kapima upepo, kaona atapoteza kiinua mgongo chake bureee na kutesa watoto wake maana CCM kama huna na hutoi mkwanja, sahau kuchaguliwa achilia mbali hata kusikilizwa tu!!
 
mwaka huu lazima suluali ziwashuke ccm, na leo hii ukimwambia mwana ccm akupe mke wake ili umpigie kura

atakuletea mke wake mpaka nyumbani kwako umrudishie kesho
 
Hapo hakuna anayewawkilisha wanambeya na hizo style wanazotoa wakishapata wanambeya mtakoma kwa kupigiwa matope na ma vx v8 yao.

Kazi ya wabunge wa ccm ni kulala na kupiga makofi hata kwa mambo ya kipumbavu........Wamelala sana, wamepiga sn makofi, wametetea sn chama kuliko watz kwa miaka zaidi ya 50.
SASA NATOSHA.....ccm TUPA KULE WEKA MASLAHI YA TAIFA KWANZA
 
Hahaaaaa kipindi hiki ndo maana nakua nazunguka na mafuta ya mgado maana naweza pata kazi ya dharura kwa moja ya hawa wagombea ili nimpe kura
 
Kiongozi gani unalialia. Badala ya kumwaga sera unagalagala chini huyo ndo hafai hata kidogo pigachini
 
DSC_1006.JPG

MWENYEKITI wa UVCCM mkoa wa Mbeya, Aman Kajuna, naye akipiga magoti kuomba kura

DSC_1022.JPG

MWENYEKITI wa Jumuia ya Wazazi ya CCM mkoa wa Mbeya, Fatuma Kasenga akiomba kura kwa mtindo wa kujigalagaza ardhini

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida baadhi ya Watia nia ya Ubunge katika Jimbo la Mbeya mjini kwa tiketi ya CCM wamelazimika kuomba kura kwa aina tofauti kwa wanachama wao.
Makada hao walilazimika kupiga magoti, kugalagala ardhini, kulazimisha kuulizwa maswali, ili mradi wapiga kura wawaonee huruma na kuwachagua. Hayo yalijiri wakati makada hao, wanaowania kuomba kuteuliwa na CCM wilaya ya Mbeya mjini,walipokuwa wakijinadi kwa wana-CCM wa kata ya Nsalagha,ili kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuipeperusha bendera ya CCM.

Vituko hivyo vilileta bashasha na burudani ndani ya kata hiyo, na kuwafanya baadhi ya viongozi waliokuwa meza kuu kulazimika kusimama ili kwenda kumuinua Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mkoani hapa, Fatuma Kasenga, aliyekuwa anagalagala ardhini kuomba kura Fatuma ambaye hii ni mara yake ya pili kujitokeza kuwania ateuliwe na CCM kuwania ubunge jimbo la Mbeya mjini, alisema mwaka 2010 kura zake hazikuweza kutosha hivyo kuwaomba wana-CCM wasimuangushe mwaka huu.

Aliongeza lengo la kujitokeza kuwania nafasi hiyo ni kutaka kurudisha heshima ya jimbo la Mbeya, ambayo hivi sasa imepotea baada ya jimbo hilo kuwa chini ya mbunge wa kutoka chama cha upinzani kwa miaka mitano sasa.

Fatuma ambaye alikuwa akijinadi huku akiwa amepiga magoti, ambapo mara baada ya kumaliza dakika zake tatu alizokuwa amepewa pamoja na kujibu maswali aliyoulizwa, ndipo alipoanza kugalagala huku akiomba kura kwa wana-CCM.

Hatua hiyo iliwafanya baadhi ya viongozi waliokuwa meza kuu, kulazimika kusimama na kwendakumsaidia kumuinua kasha kumsindikiza walipokuwa wamepangiwa kukaa wagombea wenzake.

Naye Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Mbeya, Aman Kajuna, alisema wakati anachaguliwa kushika nafasi hiyo mwaka 2012, alikuta asilimia kubwa ya vijana ndani ya jiji la Mbeya wakiwa wamekata tamaa na kuhamia upinzani. Kajuna alisema kazi yake ya kwanza ilikuwa ni kuwafikia vijana hao akianzia na wale wa CCM, kukaa nao na kuwauliza sababu iliyopelekea wakate tamaa na Chama, ambapo aliwaomba warudi kukitumikia na kukitetea Chama.

Mara baada ya kumaliza kujinadi kwa wana-CCM hao, Kajuna aliamua kupiga magoti na kuomba kura akiwaahidi wanachama hao kuwa anao uhakika wa asilimia nyingi kuwa anao uwezo wa kulikomboa jimbo hili, kwani ametoa misaada mingi kwa vijana, wanawake na wazee.

Kwa pande wake Mkurugenzi wa kituo cha radio Generation Fm, kilichopo jijini Mbeya, Shadrack Makombe, alisema yeye ni kijana wa viwango, hivyo kuwaomba wana-CCM wamchague ilikuipeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Makombe alisema akipewa ridhaa hiyo anao uhakika wa kulikomboa jimbo la Mbeya mjini, na baada ya kutekeleza hilo atahakikisha anatafuta wafadhiri watakaojenga viwanda ili viweze kutoa ajira kwa vijana mjini Mbeya.

11224060_1081455351881974_7547486702622040934_n.jpg

Ni mnafiki pekee hasiyejua maana ya uongozi anayeweza kuomba kura kwa style hii. Wananchi lazima wawakatae watu wa aina hii na mara nyingi baada ya kuchagulia husahau na kutaka kuhabudiwa!
 
Back
Top Bottom