Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,215
- 3,587
Dhana ya ugombea binafsi ni tamu masikioni lakini chungu kutekelezeka. Kenya yenye sheria hiyo imetoa ushahidi, funzo na alarm kwamba ni dhana ngumu kutekelezeka baada ya IEBC na wapigakura kuchanganyikiwa na kutamani ugombeaji kupitia mfumo wa vyama. Takwimu za IEBC zilizotolewa jana kwa umma zinaonyesha kwamba kuna zaidi ya wagombea binafsi 1500 na wale wa kiti cha urais wanafika 47.
Msingi wa hofu ni nini:-
1. Wamegundua kuwa wapigakura wamechanganyikiwa kwa kushindwa kujuwa historia za wagombea binafsi hao Kenya kutokana na idadi hiyo kubwa na inayozidi kuongezeka kila uchao; ili kura za wananchi zisikose target.
2. IEBC imepata kazi ngumu ya kuwafanyia vetting idadi hiyo ambayo inazidi kuongezeka.
3. Kuna hatari ya matapeli kugombea (kumbuka nahau ile kwamba: hakuna ajuaye kiungurumacho kwenye kifua cha Simba)
4. Kuna hatari ya Mahakama kupokea kesi nyingi za kuchezeana rafu na kwamba mzigo wa idadi kubwa ya kesi za uchaguzi huenda ikavunja rekodi na kuipa IEBC gharama kubwa za chaguzi za marudio kama Mahakama itaamuru hivyo.
5. Kuna sintojuwa kwamba matapeli wenye njaa wanaweza kutumia mwanya wa ugombea binafsi ili wakikosa ushindi basi wanafungua madai ya kuhujumiwa na kudai ama kupewa ushindi au fidia ya gharama za kuendesha kesi (ujasiriamali wa uchaguzi).
6. Kuna hofu kuwa baadhi ya wagombea binafsi wanatumia mwanya huo kama chambo/mtego kwa wale wenye vyama ili kwamba wenye vyama wanapohisi hawana wafuasi wengi katika ngome fulani basi watoe ela ndefu kwa wagombea binafsi ili wawaachie wafuasi wao kwenye ngome hizo.
7. Wananchi na asasi husika na uchaguzi wamekubaliana kwamba kumbe mfumo wa ugombeaji kupitia tiketi za vyama ni mzuri kwa maana chama ndicho kwa niaba ya wapigakura kinamfanyia vetting ya msingi (kabla ya ile ya IEBC) mgombea na kumuuza kwa wapigakura.
NB.
Kenya hivi sasa mpigakura ni bidhaa-adimu, vyama ni vitega uchumi-adhimu.
Kenya imesajili vyama 90 na takriban 40 maombi yao yako mezani kwa Msajili wa Vyama vya Siasa. County ya Mlima Kenya inaongoza kwa idadi kubwa ya vyama vya siasa 10 vikubwa na vidogovidogo zaidi ya 10.
Mwaka 2007 Kenya ilikuwa na vyama vya siasa 160 vyenye usajili wa kudumu.
Kuna maeneo Kenya ambayo chama cha kisiasa kiko hai kwenye wilaya/county moja tu au tarafa/division moja tu au kata/sub-division moja tu.
Hii ukichanganya na ukabila inafanya Kenya kuwa na biashara ya binadamu kama ya utumwa vile.
Wasomi wengi waliokosa ajira wameingia kwenye biashara ya siasa ya kuanzisha na kusajili vyama na kurubuni wasio na ajira kuwa wafuasi wao kwa malengo hayo ya kuvuna pesa za ama ruzuku au za uchaguzi ambapo wengine hawagombei lakini wanaweka wafuasi wao sokoni kwa ajili ya vyama vikubwa kuwanunua au kumuahidi mwenye chama cheo katika serikali endapo chama-mnunuzi kitashinda na kuunda serikali.
Wenzetu wame-advance.