pingli-nywee
JF-Expert Member
- Sep 16, 2015
- 11,923
- 13,344
Wagombea ubunge 18 wa chama tawala(CCM) waingia kwenye kinyanganyiro bila wapinzani. Mgombea urais wa chama cha upinzani, Chadema, Tundu Lisu amesema kwamba kuna njama ya kuhujumu upinzani baada ya 30% ya wagombea udiwani wa chama chake kutupiliwa mbali na tume ya uchaguzi kwenye usajili.
Aliongeza kwamba wagombea ubunge 53 pia kati ya 244, hawakuorodheshwa na tume ya uchaguzi, huku hatma yao ikiwa ya sintofahamu. Taswira ni hiyo hiyo kwenye chama cha upinzani ACT.
Ambayo mgombea urais wake Bernard Membe alieleza kusikitishwa kwake na habari kwamba hakutakuwa na upinzani wowote dhidi ya wagombea ubunge wa CCM kwenye maeneo bunge 18.
Hivi majirani sheria zenu zipoje kwenye suala hili? Rufaa za wagombea walioenguliwa lazima ziwasilishwe kwa mbwa mwitu huyu huyu aliyevalia ngozi ya kondoo? Au ni ruksa kuwasilisha malalamishi mahakamani kama ilivyo nchini Kenya?
Tanzanian opposition alleges irregularities in candidates' enrollment