kwa-muda
JF-Expert Member
- Sep 5, 2018
- 2,101
- 5,442
Katika maisha nimejifunza kutojitia mstari wa mbele marafiki wanapo gombana maana wakipatana we uliyekuwa mstrari wambele unabaki ndo adui.
Mfano naona RC na Clouds sasa urafiki umerudi full promo kila siku wanarusha interview yake na haipiti nusu saa bila kusikia ile promo yake ya fiesta kesho.
Najiuliza watu kama le mabebz aliyekuwa mstari wa mbele kuliko RC mwenyewe anawaza nini? Najiuliza akina Soudy nao wanaonaje?
Mara nyingi watu wakigomabana wanakuwa wana ugomvi binafsi au wa kimsalahi na watu wengi hujikuta wanatumiwa nao wanauvaa mkenge. Ni bora kuwa makini kabla ya kujiunga kwenye ugomvi.
Mfano kuna wasanii kibao waligombana na mawingu wakiunga harakati za antivirus japo zilianzishwa na watu wengine lakini Sugu alipojiunga ndipo zikapta moto na wasanii wengi wakajiunga kumuunga mkono. Kumbe mwenzao kiukweli hakuwa akipigania maslahi ya wasanii ila ilikuwa ni kama revenge kwa Ruge kumzunguka na alipoitwa wakamalizana na Ruge hata hakukumbuka kuwataarifu wenzake kuwa harakati zimekwisha.
Wengi wakabaki wanaumia hadi wengine kwa aibu wakaenda kuomba msamaha na hili ni jambo ambalo mashabiki wa damu wa Sugu uwa hawapendi kulisikia kabisa.
Watu wakigomabana kabla ya kuchagua upande kuwa na hakika kama kwenye harakati ni za utetezi kweli au unataka tumiwa kama daraja tu la kuongeza nguvu ya kudai maslahi binafsi.