Hicho ndio kiswahili fasaha WAZAWADIE, kama huoni tatizo liko wapi basi kiswahili chetu bado kina safari ndefuTatizo lipo wapi kwani,mfano ndiyo wangeandika "wazawadie" ingeleta faida gani?
Lugha haiwezi kukuzwa kwa vitu kama hivyo.
Idd NingaTangazo la mwezi wa 12 la king'amuzi cha Startimes lilikuwa tangazo lililokosa weledi kwenye lugha ya kiswahili na kwakweli linarudisha juhudi nyuma za kukiweka kiswahili kwenye ramani ya dunia
Sioni sababu kwanini lisingetumika neno WAZAWADIE na badala yake wakatumia neno la Kiingereza lililochakachuliwa na kiswahili yaani wagiftishe
Wakati wenzetu wakiwa makini na lugha zao sisi tunafanya mizaha
Safi saana Idd NingaIdd Ninga
JF-Expert Member
#1
Dec 26, 2015
1)enyi makampuni
simu,mbona lugha
mwachafua.
Kusema yanilazimu,lugha
yenu nachukia.
Kiswahili si kigumu,vipi
mnakibomoa.
Tena mnakipa sumu,kife
huku chakodoa.
Ningewa kifimbo
cheza,bakora ningetembeza.
2)kwenye wenu
usahili,kingereza haribika.
Mwaona ujahili,wala
tujaelimika.
Vipi hiki kiswahili,mnataka
kukizika.
Hivi kweli mnajali,kwamba
sisi twaudhika.
Ningewa kifimbo
cheza,bakora ningetembeza.
3)kama lugha
hamjui,simuwafate wajuzi.
Ama hamkitambui,kiswahili
si cha juzi.
Utakipata shelui,hata
kwenye king'amuzi.
Kama nyinyo hamjui,vipi yu
mchunga mbuzi.
Ningewa kifimbo
cheza,bakora ningetembeza.
4)matangazo redioni,lugha
mwaivunja vunja.
Nu mbaya masikioni,mbona
mwaikunja kunja.
Kwa zawadi za
dukani,mbovu mwapigia
mbinja.
Yakera masikioni,lugha
mnavyoipunja.
Ningewa kufimbo
cheza,bakora ningetembeza.
5)msijifanye vipofu,katika
lugha za watu.
Lugha mwaitia hofu,tena
mwazidisha kutu.
Hiyo si nyama ya
pofu,muipake ukututu.
Msiifanye nyamafu,ije nuka
kama kutu.
Ningewa kifimbo
cheza,bakora ningetembeza.
Shairi:KIFIMBO CHEZA.
mtunzi:Idd Ninga wa
Tengeru Arusha.
0655519736.
Idd Ninga umeharibu ladha hapo kwenye poem hebu ondoa hilo uweke neno stahiki yaani shairiwatu mpaka tukaandika poem kuhusu hilo na lipo hapa jukwaa la lugha kwa jina la KIFIMBO CHEZA.
lakini mwisho wa siku wale tuliosemwa ndio tukawa wa kwanza kupewa vidonge na wenye lugha.
hivyo hata watanzania wenyewr huwa wanapenda lugha yap iharibiwe
mshana jr ukisema sana watanzania wanakuona mshamba
watu na lugha yao lakini hawaithamini,shida tu.
Mabadiliko yanaazia kwetu mimi na wewe hata katika mada zetu hiziHaya mnayoyafanya humu ni maigizo matupu,kile mnacho kitaka kiwe ni mbali na mnacho kilalamikia humu.
Mnataka watu waongee kiswahili fasaha(kama inawezekana) lakini ajabu mnalalamikia vitu vidogo vidogo vilivyoanzishwa juzi tu hali ya kuwa kwa asilimia kubwa wenyewe tunaongea kiswahili kisicho fasaha mbali na hivyo viswanglish vilivyoanza juzi.
Wenzetu gani labda wako makini?Tangazo la mwezi wa 12 la king'amuzi cha Startimes lilikuwa tangazo lililokosa weledi kwenye lugha ya kiswahili na kwakweli linarudisha juhudi nyuma za kukiweka kiswahili kwenye ramani ya dunia
Sioni sababu kwanini lisingetumika neno WAZAWADIE na badala yake wakatumia neno la Kiingereza lililochakachuliwa na kiswahili yaani wagiftishe
Wakati wenzetu wakiwa makini na lugha zao sisi tunafanya mizaha
Mkuu hata mie nahitaji kuwajua hao wenzetu waliyo makini.Wenzetu gani labda wako makini?