Wageni wengine bhana ni kero tupuu!

Wageni wengine bhana ni kero tupuu!

KARIMUU

Member
Joined
Sep 7, 2014
Posts
28
Reaction score
6
Habari wana JF.

Kuna usemi usemao "mgeni njoo mwenyeji apone" lakini kuna baadhi ya wageni sio wote ukiwakalibisha home inakua ni kero mpaka unatamani siku za kuondoka zifike asepe zake.

Kuna baadhi ya wageni tunaowakaribsha majumbani kwetu au gheto kwa sisi vijana kusema kweli ni wavivu alafu wachafu yaani unakuta mtu analala alafu akiamka hata kutandika kitanda anashindwa. We unaamka unamwacha bado kalala alafu anaacha kitanda hivyo hivyo we ndo unakuja kutandka alafu hata haya hana.

Pili hata vyombo mlivyolia chakula anashindwa hata kuvisuuza yeye bngwa wa kuamka na kucheki tv alafu unarudi toka may be kazini unakuta ndio hana mpango wa kuwasha hata jiko alafu sasa ye ndani ndio anakuwa bingwa wa kujua kila kitu mara utaona yeye ndio bngwa wa kubadili channel kwenye tv, bingwa wa kupakua wa kwanza msosi ukiwa tiyari, bingwa wa kubadili CD yaani utadhani yeye ndio mwenye nyumba yaani mpaka kero.
 
wa hivyo sikufugi...unapewa vidonge vyako live bila chenga na ushahidi juu ukinuna ondoka nenda walikozoea huo uchafu kwa hiyo mlango ulioingilia ndio utakaotokea.
 
Mkuu KARIMUU, mwambie anitembelee na mimi huyo mgeni kama bado yupo kwako.
 
Last edited by a moderator:
Kwa nini unawakaribisha? Kwani hoteli hamna?
 
Kama ni rafiki yako kwa nini usimwambie hasa hayo ya kutandika kitanda, kupika na kuosha vyombo, unaweza ukafanya hivi: wakati wewe unapika unamwabia yy aoshe vyombo, mnakuwa mnagawana majukumu kidogokidogo anazoea ukikaa kimyaa ataona ni kawaida tu kutofanya lolote.
 
Thread nzuri tatizo huo uandishi wako hapa jf umepigwa marufuku, sana huwa ukiandika hivyo tu tunajua uko na shida sana yaani hivi kweli"bngwa"

Kwanini usiandike vema, bingwa, kubadilisha?
 
Kwangu mimi hili neno Bhana sijui asili yake wapi!,tubuni vya msingi!.
 
Dah! Mchizi wa design ile namlia ganja stick 3 halaf nkinachofuata .......LOADING
 
na wale mnaosafiri kikazi mfano semina au mafunzo muwe munafikia gesti sio kwasababu tu nipo mkoa huo ulazimishe uje kulala kwangu.
 
Kama huwezi kupokea na kukaa na mgeni bora uwaambie watafute pa kufikia...

Kama unamkarbisha halafu baadae unanung'unika haina maana yoyote.

Kila mtu anastaili yake ya maisha ambayo ameizoea. Pengine kwake hajawahi tandika kitanda wala kuosha vyombo hawezi kuja kujifunzia kwako hasa kama hajaambiwa afanye hivyo
 
na wale mnaosafiri kikazi mfano semina au mafunzo muwe munafikia gesti sio kwasababu tu nipo mkoa huo ulazimishe uje kulala kwangu.

Mkuu hapaa umenena .unakuta ofisini kwao kapewa helaa ya kulalaa hotel na kufanya kila kitu mpk semina iishe lkn anakuja kujibanabana kwako inaboaa hii
 
Thread nzuri tatizo huo uandishi wako hapa jf umepigwa marufuku, sana huwa ukiandika hivyo tu tunajua uko na shida sana yaani hivi kweli"bngwa"

Kwanini usiandike vema, bingwa, kubadilisha?
cc: KARIMUU
 
na wale mnaosafiri kikazi mfano semina au mafunzo muwe munafikia gesti sio kwasababu tu nipo mkoa huo ulazimishe uje kulala kwangu.

siwezi kubali alale kwangu labda kama tutagawana hiyo hela ya semina.
 
Sio siri mimi mgeni akifika tu dk. 10 nyingi baada ya salam swali linalofuata utaondoka lini? siku mbili kabla ya hiyo tarehe namkumbusha akakate tiketi, akisema hana nauli nampa aondoke, ndivyo tulivyozoea. hata mimi sishangai nikienda kwa ndugu yangu kukutana na hilo swali ni kitu cha kawaida kabisa. siku ikipita unatimuliwa, ukienda kusema nyumbani wazazi wanamtetea kwamba si uliahidi mwenyewe? Maisha ya sasa sio ya kukaa na mtu zaidi ya siku tano atakukera tu.
 
Kuna point kwenye tread yako lakini uandishi wako sasa wakifesibuku, hutapungukiwa kitu ukiandika neno lililokamilika, mfano bingwa....
Huyo mgeni wa hivyo kwangu sidhani kama anaweza kumaliza hata siku mbili

Habari wana JF.

Kuna usemi usemeo "mgeni njoo mwenyeji apone" lakini kuna baadhi ya wagen sio wote ukiwakalibisha home inakua ni kelo mpaka unatamani siku za kuondoka zifike asepe zake.

Kuna baadhi ya wageni tunaowakaribsha majumbani kwetu au gheto kwa sisi vijana kusema kweli ni wavivu alafu wachafu yaani unakuta mtu analala alafu akiamka hata kutandika kitanda anashindwa. We unaamka unamwacha bado kalala alafu anaacha kitanda hivyo hivyo we ndo unakuja kutandka alafu hata haya hana.

Pili hata vyombo mlivyolia chakula anashindwa hata kuvisuuza yeye bngwa wa kuamka na kucheki tv alafu unarudi toka may be kazini unakuta ndio hana mpango wa kuwasha hata jiko alafu sasa ye ndani ndio anakuwa bingwa wa kujua kila kitu mara utaona yeye ndio bngwa wa kubadili channel kwenye tv, bngwa wa kupakua wa kwanza msosi ukiwa tiyari, bingwa wa kubadili cd yaani utadhani yeye ndio mwenye nyumba yaani mpaka kero.
 
Back
Top Bottom