Wageni wanapita njia za panya kuingia nchini wengine wanalipa bodaboda 1000 kwenda vituo vya mabasi. Kipindi hiki Serikali imulike mipaka yetu

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,400


Huyu mwanamke amekutwa na wananchi akiwa hoi kwa kuumwa kifua karibu na mpakani Makuyuni.

Nikiwa nimiejituliza naangalia runinga kuna taarifaya habari ambayo inahusu wageni ambao wanaingia nchini kupitia njia za vichochoroni au njia za panya.

Katika taarifa hiyo ya habari, wakuu wa mikoa ya Kilimanjaro na Rukwa wamesisitiza kuimarisha ulinzi kwenye mipaka yetu na wamewataka poli na idara ya uhamiaji kuwa makini.

Njia hizi ni zilezile ambazo hupitisha bidhaa za magendo kama sukani na kadhalika na wakati mwingine hutumiwa na raia wanaotaka kuhujumu mfumo wa uhamiaji au wanaotumia mfumo wa biashara ya kusafirisha binadamu.

Nchi yetu ina mipaka ya Horohoro, Tunduma kwenda Zambia, Namanga kwenda Kenya, Rusumo kwenda Rwanda,

Njia ramsi ya kupita mpakani kuelekea Burundi ni ile ya Nanyovu na ile ya darajani Kobero kati ya Ngara na Muyinga.

Pia tusisahau kuna njia ya barabara ya kutoka Ngara hadi Mwanza ambayo inachukua kama masaa 7 hivi. Na ingine ni ile ya kutoka Bujumbura au Kigoma kwenda Manyovu na hii huchukua kama masaa 9 hivi.

Pia mtu anaweza kukodi gari kutoka Nayakanazi hadi Ngara safari ambayoi huweza kuchukua masaa 4 hivi.

Kuna mpaka wa Tanznaia na Malawi ambapo ni lazima uvuke mto Songwe kwenye daraja la Kasumulu hivyo ukiwa Mzuzu au Karonga waweza kuchukua basi hadi mpakani na Tanzania.

Hali kdhalika kuingia nchini Msumbiji unapaswa kuvuka daraja la Umoja kwenye mto Ruvuma sehemu yaitwa Magomano ambapo pana kamji kanaitwa Momoni.

Kutokea hapo Msumbiji kwenda mpakani na Tanzania waweza kutokea kwenye miji ya Palma na Paqimboa da Praia ili kuvuka mpaka wa Namiranga.

Ukivuka kwa mtumbwi kuzingatia na ujazo wa maji ya mto basi utaweza kuingia mpakani sehemu yaitwa Kilambo na hapo utachukua basi hadi Mtwara.

Ipo mipaka mingine Zaidi kama Mutukula kaskazini mwa mji wa Bukoba na kituo cha Nkurungu.

Hivyo mtu anaekwenda Arusha au Moshi akitokea Uganda na pia akielekea Kenya.

Pia msafiri anaweza kuchukua basi kutoka Kampala hadi Arusha kupitia Nairobi na pia unaweza kuchukua basi kutoka Kampala hadi Bukoba au kutoka Kampala kwenda Mwanza.

Mpaka wa Tanzania na Zambai ni ule wa Tunduma kutokea wilayani Mbozi na kule SUmbawanga kuna kivuko cha Kiseya kwenda mji wa Mbala. Pia kuna garimoshi la Tazara kutoka Kapiri Mposhi hadi Dar-es-Salaam.

Pia upo usafiri wa gari au basi na huchukua muda mrefu Zaidi.

Hivyo habari hiyo ya kwamba kuna wageni wanaingia nchini kupitia njia za panya halafu wanalipa shilingi 1000 kwa bodaboda kwenda mijini si habari nzuri.

Tukiwa katika kiindi hiki kigumu cha kupambana na ugonjwa wa kuambukiza wa COVID -19 , kila mtanzania anapaswa kuwa mlinzi wa nchi yetu.

NI kipindi hiki cha kuisaidia serikali kwa kutoa taarifa kwenye vituo vya polisi pale tunapohisi kuwa abiria au mtu anaepita tu njia na haeleweki na anaonekana na mgeni na sehemu hiyo na ametokea sehemu ya mpakani.

NI klpindipia kuangalia biashara zeru kwa wale bodaboda na kwa kutambua mchanog wao kwenye sekta ya usafiri khasa kwenye maeneo tatanishi, tunapaswa wote kuwa waangalifu.

Tukumbuke kunakawa mikono.
Tuepuke misongamano
Tutumie vitakasa mikono bila kuiba tunapotumia za wenzetu.

Kheri ya Pasaka.
 
Back
Top Bottom