Waganga wa mapenzi wana msaada wao kwenye mapenzi jamani

Habari zenu wakuu, Poleni na Majukumu ya kutafuta Mkate wa kila siku.

Haya maisha yana mambo mengi sana na watu tuko wengi sana yapata Bilioni 7 duniani nlivyotazama mara ya mwisho, Maisha yanahusisha Familia, Pesa na Mapenzi.
Leo nimekuja kwa jambo moja kuu, nalo ni la Mapenzi na Lengo ni ku'share' uzoefu baina yetu

**Ninaipongeza sana JF kwa kutupa ruhusa ya kutumia ID feki ili tu kuzungumza kwa uwazi
Maana wengine huko kwenye jamii zetu tumejijengea picha za watu Wastaarabu kweli kweli

Watu tunatofautiana katika mambo mengi, Tupo ambao tukijaribu na kukosa huwa hatukubali tunajaribu tena na tena pasina kukata tamaa, na wapo ambao wakijaribu na kukosa wao hushukuru na kuacha.

Katika harakati za kimaisha nmekuwa na Mahusiano na wasichana kadhaa (suala la wengi au wachache inategemea na utavyotazama) kiukweli mambo yalikuwa rahisi tu, nilipata nilichotaka kwa wakati niliotaka

Lakini nmefika mahali nmekwama, Nimekutana na Binti nmempenda kwa dhati yangu yote nae ameonesha mapenzi.... Baada ya muda fulani wa Kudate naona mambo yanabadilika taratibu na kila nikichungulia huko mbeleni naona kama meli itatia nanga ndani ya miezi michache

Sasa kama Waswahili wasemavyo 'Kinga ni bora kuliko tiba'
Nimefanya jitihada zote za kibinadamu (kuongea nae) kumuweka mwenzangu kwenye mstari na kuliepuka balaa linaloendea kutukuta lakini hizi jitihada hazinipi tumaini la kubadili hatma mbaya iliyoko mbeleni.

Suluhu ya matatizo ulimwenguni ni nyingi sana na Mungu ametupa uhuru wa kuchagua tuyatakayo yawe mabaya yawe mazuru lakini pia katueleza gharama (athari) zake.... Kwahyo katuacha huru Wanaadamu hapa duniani kila mmoja kuchagua njia anayoona inamfaa (binafsi namshukuru sana kwa hiii nafasi ambayo mbuzi hakupewa).

Hivi karibuni limenijia wazo, Nmefikiria kutumia njia za jadi katika kubadili hatma ya penzi langu....(na si kwa lengo baya)
Kwa maneno mengine nataka kwenda kwa Mtaalam/Mganga/Sangoma (vyovyote umuitavyo) ila ndo nataka kwenda kwa huyu mtu mwenye profession hii ya kiroho nijaribu ku'dili' na hatma yangu kiroho zaidi.

Lengo la kuleta hapa bandiko hili ni kupata uzoefu kwa watu (Wanaume/Wanawake) ambao aidha kwaajili ya kunusuru ndoa au mahusiano yao walichukua maamuzi kama yangu ya kwenda kwa Tabibu wa kiroho...

Itafaa zaidi kutueleza Tatizo ulokuwa nalo (kama linatofautiana na hili) mpaka likakupelekea kwenda huku maana tunajua mpaka umeamua hivyo tatizo halikuwa dogo,
Dawa uliyopewa na masharti yake,
Uharaka na Ufanisi wa utendaji kazi wake (yaani ni kwa kiasi gani ilitatua tatizo lako) yaani matokeo na mabadiliko uliyoyaona baada ya kwenda kwa mtaalam
na Gharama ulizotumia au kupoteza.

**Ruksa kuja na ID feki, Lengo ni kuchangia uzoefu wa kwa Wataalam/Sangoma/Waganga tuuuu

NAWASILISHA....View attachment 1696904
Hii id sometimes unakua mwanamke sometimes mwanaume, jinsia yako ni ipi tafadhali
 
Brother hakuna uchawi kwenye mapenzi. Niamini mimi yakiisha yameisha ht uloge vip.
 
Nakushauri uhame kwanza hapo kwa shemeji yako utafute maisha yako,maana unakoelekea huwazi kujitengenezea maisha yako kwanza,ila unawaza kudinya tu ,huyo bint kaona huna muelekeo ndio mana ameamua kujiondoa taratibu
 
Yaaani jinsi ambavyo Sina hela...Siwezi Wala sifikirii kumpelekea mtu kuku...sijui mbuzi..nikamloge mtu...NO WAY...

DUA NI FREE KABISA...Tena Kama umedhulumiwa au umedanganywa...UNAMPIGA DUA TU...

Sasa Wewe unataka.lazimisha upendwe solution...Ni Kutafuta mwingine
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom