Waganga wa kienyeji mnaoishi mjini kwanini mnapenda tiba za guest?

Kudo

JF-Expert Member
Nov 2, 2017
1,809
6,081
Hapa nchini kwetu nimekuwa ni mzururaji mzuri sana, jambo linalopelekea niwe mtumiaji mzuri wa nyumba za wageni, lakini nimekuwa nikikutana na kesi nyingi za waganga wa kienyeji kufanya tiba kwenye nyumba hizo.

Mfano, sasa nipo hapa Dodoma sasa hivi kuna mtu anapiga kelele za kuaguliwa majini na mganga wake kwenye hii nyumba niliofikia jambo lilizua kero nyingi miongoni mwa wapangaji kwenye guest hii.

Sio hivyo tu, wiki jana nilikuwa Dar napo guest ya jirani kuna mganga kakutwa anamtibia mteja wake usiku wa manane nje ya vyumba vya wapangaji wengine uchi wa mnyama na hizo ni baadhi tu japo ni nyingi kweli.

Lakini kubwa ni kuwa katika matukio mengi ya hivi wanaokutwa ni wanawake kuliko wanaume na kwanini wanawake ndo wengi waendao kwa waganga kuliko wanaume? Ukitaka uthibitishe hilo tembelea vijijini utaona waliopanga foleni kwenye nyumba za waganga ni wengi wanawake kwanini?

Asalaaam kudo
 
wanawatibia hasa wanawake wakipagawa wanamalizana kiutuuzima na malipo yanaishia hapohapo
 
Back
Top Bottom