Wafungwa nao Wakapate Kikombe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafungwa nao Wakapate Kikombe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ndallo, Mar 28, 2011.

 1. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,127
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Namnukuu Babu wa kule Samunge Loliondo kama alivyosema wakati anatoa tiba ya kikombe cha dawa kwa wagonjwa waliokwenda kupata tiba akiwapo mimi mwenyewe kuwa alikua akisema kama umekuja mwenyewe kupata tiba basi ukirudi nyumbani kamlete na mwenzako na pia na wengine waje kupata kikombe ili watu
  wapate kupona mwisho wa kumnukuu.

  Sasa tumeshashuhudia hata viongozi wa serikali wakiwapo wakuu wa mikoa wastaafu hata na mawaziri wameshakwenda kupata vikombe vya dawa na watu bado wanazidi kumiminika japokua zoezi hili limesitishwa kwa muda mfupi kidogo kutokana na wingi wa watu pamoja namiundo mbinu kuwa mibovu.

  Wazo langu kwa serikali ni kua kwakua Babu anatoa tiba hadi ya ukimwi na hii ni habari njema kwa wale waadhirika wa ukimwi basi serikali kupitia sekta zake za afya kwanini basi wasiwaruhusu na wafungwa pia kwenda kupata dawa ya kikombe kwa Babu? kwakua kama tunavyojua kule magerezani kuna magonjwa lukuki ya kuambukiza likiwapo gonjwa sugu na hatari la ukimwi? hii itasaidia sana kwa taifa hili kuondokana na magonjwa sugu ili hapo baadae tuwe na taifa ambalo halina magonjwa huku tukizingatia kuwa Tanzania bila ukimwi inawezekana! Nawasilisha.
   
Loading...